Msaada juu ya barua ya uhamisho Chuo

lamar69

Member
Jan 13, 2018
42
20
Habari zenu ndugu zangu,

Naomba nipate muundo wa barua ya uhamisho kutoka Chuo kwenda Chuo kwa mtu yoyote anayefahamu. Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza ninayehitaji kuhama kutoka Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) kwenda University of Dar es Salaam (UDSM). Naombeni msaada wenu ndugu zangu.

Ahsanteni.
 
Udsm wazinguzi sana kuna kasecretary kao kanaeleza upuuzi afu akajui kuongea na watu sa ndo maana nmeona bora nfupishe swala kwakuwauliza nyie wadau
Nenda kwa director wa undergraduate studies form utazikuta huko af utaenda kwenye idara unayotaka kuhamia
 
Habari zenu ndugu zangu,

Naomba nipate muundo wa barua ya uhamisho kutoka Chuo kwenda Chuo kwa mtu yoyote anayefahamu. Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza ninayehitaji kuhama kutoka Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) kwenda University of Dar es Salaam (UDSM). Naombeni msaada wenu ndugu zangu.

Ahsanteni.
Nilipewa maelekezo kipindi nataka kuhamia MUST nikiwa nimechaguliwa DIT. Kwa maelezo ya watu wa admission pale MUST ambapo unaweza kutumia mfumo huo kwenye vyuo vingine;
1. Unaandika barua ikiwa inaelekea TCU kupitia chuo husika unachotaka kuhamia.
2. Ambatanisha admission letter au matokeo kutoka chuo unachotoka.
3. Ambatanisha na vyeti au uthibitisho uliokufanya ukachaguliwa hicho chuo unachotaka kuhama.
U
 
Mkuu , uliandika
kwa kiswahili , ama kiingereza .?

Hivi kupitia kwa (k.k) kwa kiingereza huwa inaandikwaje ?
 
Ni aibu Mwanafunzi wa chuo kutojua jinsi ya kuandika Barua ya Kiofisi
Aibu sana.
Afu unakuta alifaulu mtihani wa Form Six.

@FaizaFox njoo uone wanaosomea ujinga shuleni
 
Walimu wa lugha primary mna shida sana
 
Ni aibu Mwanafunzi wa chuo kutojua jinsi ya kuandika Barua ya Kiofisi
Aibu sana.
Afu unakuta alifaulu mtihani wa Form Six.

@FaizaFox njoo uone wanaosomea ujinga shuleni
bibi FaizaFoxy unaitwa , huku na mjukuu wako Root .
Ni aibu kusema kweli.

Aandike hivi...

Baada ya anuani (asinambie na hizi hafahamu pa kuziweka).

Maombi ya kuhamishwa chuo.

Utaanza kwa kujitambulisha wewe ni nani na unasoma "course" zipi na mwaka wa ngapi.

Naomba kuhamishwa chuo .... kwenda chuo.......

Sababu za kuomba kuhamishwa ni......

Utasema unataka kuhamishwa lini.

Ahsanteni.

Pia fanya tafiti kidogo kama chuo unachotaka kuhamia kina nafasi za masomo yako kabla hujapeleka maombi.
 
Ndio maana nimejiwekea kamsimamo kangu bora nimpeleke mtu veta kusomea umeme wa magari kuliko kulipia mtu akasome A level na Chuo kikuu, wengi wanatoka wanajua kuibia mitihani,
kuvaa modo,
kunyoa kiduku,
Kutongoza vitoto.

Yaani hawana tofauti na sisi ambao hatukumaliza
 
Ni aibu Mwanafunzi wa chuo kutojua jinsi ya kuandika Barua ya Kiofisi
Aibu sana.
Afu unakuta alifaulu mtihani wa Form Six.

@FaizaFox njoo uone wanaosomea ujinga shuleni

Hivi huu muda wakulaumu siungeutumia kufanya mambo yako uoni ingesaidia
 
Ni aibu Mwanafunzi wa chuo kutojua jinsi ya kuandika Barua ya Kiofisi
Aibu sana.
Afu unakuta alifaulu mtihani wa Form Six.

@FaizaFox njoo uone wanaosomea ujinga shuleni
Mkuu

Ule mtihani wa form six wa general studies, physics, chemistry, mathematics au biology kunakuwaga na format ya kuandika barua????????
 
Back
Top Bottom