Bokohalamu
Member
- Mar 13, 2012
- 94
- 8
Habari wakuu! Baada ya kukaa na hii private kampuni kwa miez zaidi ya probation period waliyonipa wakiwa wananipa allawance tu, leo wamenipa barua ya kazi rasmi niisome nikiridhia ni sign. Hii kampuni ni ndogo na bado inaoperate at loss, tatizo ni kwamba wanataka kubana matumizi hivyo wameni title kama Accounts assistant wakati mimi nina Advanced Diploma in Accontancy na Postgraduate Diploma in Accontancy,kwangu nahisi si sawa wamenishusha ili ni dai zaidi. Nililalamika juu ya hili nikapewa nafasi ya kwenda kutafuta source zitakazo onyesha ni kiasi gani haswa mtu mwenye sifa zangu anayeanza kazi anapashwa kulipwa,ni kawaambia wajaribu kucheki na utumishi wakaniambia nitafute mwenyewe hawaijiu! Sasa ombi langu kwenu ni ushauri na pia wapi naweza pata hizo details za viwango vya mishahara ya serikari vitakavyo washawishi, ingawaje najua serikalini pia imegawanyiaka kutokana idara mbalimbali, na hapo ndipo pana nichanganya sasa, kweli kazi ni ngumu! Pia nilikua hapa town ila kwa sasa wanataka kunipeleka huko kijijini kwenye operation zenyewe! Akhsanteni kama nitakua nimeeleweka!