Msaada: Jinsi ya kuwa Wakala wa Tigo pesa, Mpesa na mitandao mingine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Jinsi ya kuwa Wakala wa Tigo pesa, Mpesa na mitandao mingine

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mrekebishaji, Jan 20, 2011.

 1. M

  Mrekebishaji Senior Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 168
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wana jukwaa,

  Naomba maelezo ya namna ya kuwa wakala wa M-PESA pamoja na uuzaji wa luku.

  Ikiwezekana kama kuna mtu anayehusika moja kwa moja naomba kumuona. Nipo Dar es Salaam

  wapalepale post
  Heshima kwenu,
  1. M PESA
  2. Tigo pesa
  3. Airtel money
  4. CRDB fahari huduma
  5. Kifaa cha max malipo kwa ajili ya luku etc


  jamani ndugu yenu nafikiria kuanzisha hii biashara ya u-wakala wa m-pesa. Mwenye details kidogo kuhusu hii biashara anijuza hasa nataka kufahamu kuhusu;
  1. Kiwango cha chini cha mtaji unao hitajika
  2. Jinsi faida inavyopatikana
  3. Jinsi ya kujisajiri (hili nadhani sio issue sana naweza kwenda kwa voda wenyewe) itanirahisishia zaidi
  nawasilisha
  ======================================================,Mimi ni wakala wa M-Pesa kitambo sana sijawahi tapeliwa,inalipa sana kama tu goli lako lipo sehemu yenye mchanyiko wa watu wengi na kama unaielewa vizuri biashara hiyo.Unahitaji kuwa na laini,TIN na eneo la kufanyia biashara
  kumsajili mteja ni Tsh 500/- kamishen

  mteja aliyesajiliwa akiweka pesa kwa mara ya kwanza unapata tsh 2000 kamisheni akituma pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh 300/- hadi tsh 5000/- inategemeana ametuma kiasi gani
  akitoa pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh500/- hadi tsh 5000/- inategemeana katoa shilingi ngapi

  akinunua airtime kwako unapata karibia 10% kamisheni ya airtime aliyonunua
  akinunua Luku unapata kamisheni kadhaa
  Biashara hii ili ufanikiwe zaidi unaweza kuichanganya na biashara nyingine kama kuuza luku, na vinywaji baridi kama soda na juisi ambavyo havihitaji mtaji mkubwa au kama una biashara yako tayari halafu ukaongezea hii biashara kama ziada

  Yaani kwa kijana wa kitanzania wa kawaida akiwa serious inaweza akatolewa na biashara hii kwa ufupi ZAP,M-pesa na Tigo Pesa kama una magoli matatu au maanne kipato cha mwezi ni net 2m, yanini kuajiliwa sasa?
  ================


  Faida yake inategemea yafuatayo:

  Ufanisi wako (via Operator) wa kazi;
  Kama service ni nzuri hasa in unavyowasikiliza na kuwashughulikia wateja, hii inahusisha mhudumu wako kua haraka na kujua huduma zote.
  Mfano: mteja anaweza asijue jinsi ya kutumia akaunti yaM-pesa, hapo ina maana Mhudumu awe mpole amsaidie.

  uwe na mtaji wa kutosha ili kuhakikisha mteja akija kutoa au kutuma pesa anapata
  hii itasaidia kuptopoteza miamala kwa kukosa pesa na pia itamfanya mteja awe anaiamini sehemu yako hata siku nyingine kuja kwenye banda lako,

  1. Hakikisha jioni unafunga mahesabu pesa yako mkononi na kwenye laini. Kama jumla ilikuwa milioni mbili asubuhi jioni inatakiwa iwe hio hio milioni mbili
  2. Unapata pesa ya commission mwisho wa mwezi. Kama mtaji wako ni Million 5 kwa siku na inazunguka ipasavo na hio sehemu ina shughuli nyingi, kamisheni inaweza fikia hata milioni moja au zaidi

  3. Changamoto
  4. Kama sehemu haina mzunguko wa pesa wa kutosha unaweza kupoteza muda wako, wateja wapo wa kutosha ni nadra kupata hasara. More inakua out of mistakes kama kutuma pesa mahala ambako sio husika kwa bahati mbaya.
  5. Unaweza ukatuma pesa kwa mtu mwingine ambaye sio mteja kwa bahati mbaya, japo pesa hii unaweza kupiga simu kwa vodacom halafu wakarudisha muhamala huo mara nyingine unaweza usiupate kama uliyemtumia atakuwa haraka kwenda kutoa
  6. Noti feki kama kuna wateja wanaweza wakakuletea mabunda ya pesa huku wakiwa wamechanganya na mabunda ya noti feki, kabalaya kuweka pesa kwenye droo yako hakikisha unaziangalia, kama unafanya hadi usiku nunua tube light ili kuwe na mwanga wa kutosha kugundua noti feki.
  7. Kuna vikwazo pia katika biashara hii, na kubwa likiwa ni suala zima la usalama kuna vibaka au majambazi wanaweza wakakutegea ukiwa unatoka wakakukaba, ni bora kuwa na sefu lako imara, kwenye fremu yako pia kunatakiwa kuwe na grili imara kuzunguka dirisha na mlango
   
 2. m

  muzachai Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hi Wote,

  Kazi ya kuuza chai na kashata imenishinda. nimechanga vijisenti vidogo nataka kuwa agent wa M-PESA. Naomba details

  mfano pesa ya kujaza kwenye simu ni sh ngapi na float ya kulipa wateja wanaowithdraw ni shilingi ngapi.
   
 3. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  nenda nearby vodashop na tanesco kwa maelezo zaidi...hapa utapata 'hearsay'
   
 4. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mkuu kuhusu LUKU nenda Tanesco kwa bwana mmoja anaitwa Mzava (Marketing manager) utapewa maelezo. Ukimkosa Mzava mtafute Ms Sana.
   
 5. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  pls wenye data zaidi watujuze tupate mwanga wakuanzia na mm nahitaji kujua
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  nenda selcom posta ndo utapata full data wale mashine zao zinafanya kazi kibao lakin hii m-pesa sifahamu
   
 7. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Hii ni kutoka chanzo cha kuaminika.
  Lazima uwe na leseni ya biashara halali na pia uwe na utambulisho wa mlipa kodi yaani TIN inayotolewa TRA.
  Ukiwa navyo utaenda vodacom na utasaini mkataba baada ya kutimiza vigezo vingine vidogo lakini muhimu.
   
 8. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mkuu ukitumia machine za selcom au maximalipo huesabiki kuwa moja ya wakala wa Tanesco. Hao jamaa (selcom na maximalipo) ndio wenye mkataba na Tanesco. walicho fanya ni subcontract kama mkataba wa Tanesco unavyo sema. Yaani Tanesco aliwakubalia selcom na maximalipo to subcontract under one condition. This condition is that lazima wateja wote watakao wa subcontract wauze Luku kwa bei ya Tanesco. Na mkataba unasema wasipo fanya hivyo then Tanesco kama mwajiri wa selcom na maximalipo will cancel their contract. Tanesco wanatoa commission ya 3% sasa selcom na maximalipo they decided to share this profit with their customers. Wale wote wenye machine za maximalipo na selcom wanapata 1.5% na wajiri wao wanabakiza 1.5%. There4 ukizingatia hayo utajikuta kwamba unawafanyia kazi selcom au maximalipo.
  Nivyema kwenda Tanesco kwa marketing manager Mr Mzava (huyu jamaa nimzuri sana) atakupa maelezo. Na kwa vile uko Dar atakwambia maeneo gani ambayo wanaitaji mawakala. Ukisha pata huo uwakala pia unaweza kufanya kazi kama selcom or maximalipo. Kuna routers za 3G unaweza kutumia moja kwenye 50 POS kama za maximalipo. ila hii router bei yake iko juu sana lakini inafanya kazi nzuri sana. Hutotakiwa kuingia gharama kama za maximalipo au selcom.
   
 9. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  You only need to have Tin no and bness licence! for M-PESA
  At least 1ml is ok to enjoy the service but depends with location as well
  All the best
   
 10. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Man ukifanikiwa kupata Luku also weka M-Pesa, Zap, Tigo pesa. Nitakupa mbinu how to get more business by using M-Pesa, Zap, na Tigo pesa and Luku. Hapo Dar sijaona watoa huduma ya Luku wakiitumia hiyo mbinu. It is too profitable if you are based in Dar.
  I think kupata M-Pesa, Zap na Tigo Pesa ni rahisi sana ugumu uko kwenye Luku, lazima uwe na muda wakutosha na uvumilivu pia unatakiwa.
   
 11. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Yep bro!
  Hebu weka hadharani hizo mbinu na ss wa mashambani tuzione. Huku kwetu watu wanasafiri umbalimrefu, nauli elf10 kufuatilia umeme wa buk5, na mpesa nayo utata!..IDUMU JF!
   
 12. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Prime weka hiyo mbinu hadharani ili tuisaidie jamii!pze
   
 13. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Duh! mkuu it seem hapo mtaani kwako kuna opportunity sana, kutokana na maelezo yako mafupi kuna fedha zimezaga sana hapo. Kwanini usifanye hivi, pata kama Laki 3 or 5. Then weka Tigo pesa elf 50, Zap laki, the rest M-Pesa. Halafu weka bango la huduma ya M-Pesa, Zap, Tigo na LUKU. Kumbuka subject kubwa ni LUKU na M-PESA.

  Let the charges for M-Pesa remain constant as per maelezo utakayo pata from wahusika. Kuhusu kuuza LUKU tumia Zap, umeme wa 1000-3000 charge 300, umeme wa 4000-9000 charge mia tano, umeme wa 10000-14000 charge elf, 15000-20000 charge 1500, na 21000 and above 2000

  In most cases utakuta kwamba katika laki moja you make a profit of elfu 10 within a few hours. Kama mtaani kwako kuna demand kubwa ya Luku you will make alot of money. Ila you have to make sure that unapata mtu wako wa karibu Airtel so that whenever you need Zap anakurushia halafu unampelekea pesa yake kama mtakavyo elewana. Also make sure you become an agent wa Airtel, watakupa line special.

  Normally M-Pesa inasumbua sana wakati wa kununua Luku don't use it kabisa, just use Zap it is the best.
   
 14. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  @prime mkuu ubarikiwe kwa maelezo yenye tija kabisa nimepata mwanga wa kutosha kabisa
   
 15. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35

  Mkuu, moja kati ya hizo mbinu nimeiweka hapo juu. Kama uko na maswali usigope kuuliza.
   
 16. v

  vivimama Member

  #16
  May 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau niaje? pls nisaidieni kunipa info kuhusu biashara ya M-PESA, je inalipa? risk zake ni kama zipi?
  kama kuna yeyote mwenye idea anisaidie pls.
   
 17. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #17
  May 16, 2011
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Dada kapate maelezo yanayojitosheleza toka kwa Vodafone wenyewe.
  Kama uko nje ya nchi watumie email, natumai watakupa maelezo ya kutosha.
  All the best.
   
 18. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  wandugu naombeni kuuliza manake kuna ndg.yangu anataka kuingia hii business ikoje?commission unapata ngap?kwa kuweka,kutuma nk!kwa yeyote anaeifanya naomba ufafanuzi manake sijui lolote!
   
 19. LexAid

  LexAid JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 1,950
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wanajamii naombeni kuuliza, Mimi anataka kuingia hii business ikoje? Capital gani inahitajika? commission unapata ngapi?kwa kuweka,kutuma nk!kwa yeyote anaeifanya naomba ufafanuzi. Asanteni
   
 20. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  nenda kwa wakala wa tigo/M-pesa utapata mchongo mzima, ukipata knye wateje faida ipo!
   
Loading...