Msaada jinsi ya kutunza taa za mbele

concious mind

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
984
580
Habari za asubuhi wakuu, nimeangalia taa za mbele za gari nyingi hususani toyota naona nyingi zinaukungu, nishawahi kwenda gereji moja wakaziosha ila ndani ya miezi 3 naona zinarudia ile hali.
Na je zile bulb nyeupe ni bei gani kuna fundi aliniambia pair moja ni 170 je ubora wake ukoje?
 
Kwanini usijaribu kuiosha kwa kuisugua nje. Unatumia maji na mswaki na dawa ya mswaki. Sugua taratibu kwanza kwa dawa ya mswaki na mswaki kisha osha. Sugua kwa kama dakika 10-15 kila taa. Try Colgate
 
Ziko dawa zinauzwa madukani ni mahsusi kwa kazi hii,pita maduka ya accessories za magari utazikuta na bei zake sio kubwa kihivyo.
 
Kuna baadhi ya dawa wanadai zinaharibu ile plastic so itatatkata lakini ukungu utarudi haraka zaidi
 
...........nimeangalia taa za mbele za gari nyingi hususani toyota naona nyingi zinaukungu, nishawahi kwenda gereji moja wakaziosha ila ndani ya miezi 3 naona zinarudia ile hali.........
WP_20160712_11_00_12_Pro_2.jpg

Hiyo taa pichani ina miezi miwili tangu Isafishwe.

Dawa ya kusafishia niyo pichani

Inauzwa tsh 10'000/-, Mahala pa kuipata ni mtaa wa LUMUMBA maduka ya mwanzoni kama unatokea MNAZI MMOJA
WP_20160712_11_01_04_Pro_2.jpg

JINSI YA KUFANYA
- Weka kidogo kwenye kitambaa
- paka kwenye kioo cha taa ya gari yako.
- Acha ikauke kwa dakika 2,
- Kisha sugua sugua kwa kitambaa ili kuondoa hiyo dawa iliyokauka

Mpaka hapo tayari taa yako itakuwa na mngao ule wake halisi.

Ifadhi dawa na utaitumia wakati mwnigine
WP_20160712_11_51_57_Pro_2.jpg
 
Thx Mwl. Hii itatusaidia wengi..
 
Mie natumia colgate tu maana nilioshewa pale Lumumba na dawa zao baada ya mwezi au miezi miwili ukungu ukazidi zaidi ya hapo awali.
 
Habari za asubuhi wakuu, nimeangalia taa za mbele za gari nyingi hususani toyota naona nyingi zinaukungu, nishawahi kwenda gereji moja wakaziosha ila ndani ya miezi 3 naona zinarudia ile hali.
Na je zile bulb nyeupe ni bei gani kuna fundi aliniambia pair moja ni 170 je ubora wake ukoje?
Taa za booster mkuu ni 100k na ufundi humo humo...ingawaje inaweza ikapanda kidogo mpaka 120k kutokana na brand,manunuzi,aina etc...
 
Back
Top Bottom