Msaada jinsi ya kupika bata

Fata njia zote, lakin ushauri huu wa kumchemsha bila kumkausha achana nao, iyo nyama hautaila. Bata ana shombo flani na kaarufu kabaya sana, kanaishaga mpaka umkaushe kwanza kwa oven au ata mkaa, taratibu moto mdogo at least masaa 3.
Kumbee, asante ndugu
 
Nyama ya mbele ya bata ni kavu halafu ya nyuma ina mafuta! Upishi wake ni kama kuku tu,ila usimchemshe bila kumkausha kidogo..sio kwamba hatalika la hasha! Ila ile taste itakua tofauti kidogo.. BTW mpe hongera dogo kwa ushindi.
Asante sana najifunza
 
Huyu kwenye mataifa yote yaliyotawaliwa na mreno huwa wanamchemsha na pombe au wine ili kuikata ile shombo
Nalog off
 
Baada ya kupitia Michango ya WADAU nimegundua kuwa kumbe BATA shughuli yake ni kubwa
 
Mimi binafsi huwa nampika kama anavyopikwa kuku tofauti ni pale ukimpasua bata ni vizuri kumbanika kukausha mafuta na ile damu kabla ya kumchemsha na ni vzuri awekwe viungo kama tangawizi, limao na kitunguu saum kukata shombo.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom