Msaada jinsi ya kupika bata

Kwa kifupi bata hapikwi siku hiyo hiyo...... Hii ni kutokana na miiili yao kuwa na maji mengi sana.... Au kama utampika siku hiyo hiyo basi hakikisha unamchinja asubuhi na anapikwa jioni... Nini Cha kufanya...
Bata ukishamnyonyoa na kutoa utumbo bata anaanikwa kwenye jua kali ama kama hakuna jua basi unamtundika jikoni pembeni kwenye jiko la mkaa ama jiko la kuni mpaka maji yote yaishe mwilini...
Wewe mmasai na bata wapi na wapi?
Subiria tukitaka kuchinja ng'ombe ndipo uje kutoa huu uzushi wako!
 
hapo utakaa nje hadi akaukemaana KUNGURU WAKE SI MCHEZO, unaweza kimbizana nao hadi KAWE
Kunguru wanaweza kupeleka mpaka mlandizi.
Isitoshe jamaa anaongea kwa asicho kifahamu.
mimi nafuga bata, nachinja hapo hapo na hapo hapo bata anapikwa vizuri kabisa na analiwa kama kawaida. Sasa yeye hii njia ya kuanza kumshindisha juani bata wa watu kaitoa wapi?
 
Habari zenu machef wa jf naombeni msaada njia gani rahisi ya kumpika bata awe mtamu.Sijawahi kula bata kabisa wala kumuandaa.Mwanangu kashinda mashindano ya michezo huko shule akapata zawadi ya bata sasa sijui pa kuanzia maana nasikia hapikwi kama kuku.

Naombeni msaada kuanza kumnyonyoa vipi aishe manyoya maana ana vimalaika sana.
Fuata utaratibu huu;
1. Mchinje.
2. Mtie katika maji ya moto,kwa muda usiopungua dakika kumi.
3. Mtoe na uanze kumnyonyoa,hakikisha unatoa manyoya yote makubwa.(yanayoonekana kiurahisi).
4. Mpake unga na umsugue polepole au mbanike kwenye moto wa mkaa (ili kuondoa mabaki ya vinyoya vidogodogo).
5. Mpasue tumbo mtoe vya ndani kama huwa huli kama unakula vitoe na uvisafishe.
6. Katakata vipande tenga jikoni bila kuongeza maji,mpike hadi akauke kama anataka kuungulia.
7.Badilisha chombo cha kupikia then tia maji endelea kupika kawaida hadi aive kisawasawa.
8. Malizia kwa manjonjo yako tayari kwa kula.
 
Hana tofaut na anavyopikwa kuku ila tu kumnyonyoa ndio kaz weka maji ya moto mtie humo kwa mda wa dak 5 hiv mpaka 10 toa manyoya yote vitabak vimanyoya vidogodogo tumia unga kusafisha akiwa mkavu unga wa sembe,,then kwny mapishi ni uwanja wako tu sasa mchemshe kisawasawa maana anaugum flan hiv.... ukishindwa nikaribishe nije nikusaidie kumpika km Shem hayupo lkn itakuwa vyema
Hivi ni kweli ukimnyonyoa ukamuacha kidogo,manyoya yanaota mengine? Au uzushi tu
 
Kwa kifupi bata hapikwi siku hiyo hiyo...... Hii ni kutokana na miiili yao kuwa na maji mengi sana.... Au kama utampika siku hiyo hiyo basi hakikisha unamchinja asubuhi na anapikwa jioni...
Nini Cha kufanya...

Bata ukishamnyonyoa na kutoa utumbo bata anaanikwa kwenye jua kali ama kama hakuna jua basi unamtundika jikoni pembeni kwenye jiko la mkaa ama jiko la kuni mpaka maji yote yaishe mwilini...
Asante mkuu nimekupata
 
Fuata utaratibu huu;
1. Mchinje.
2. Mtie katika maji ya moto,kwa muda usiopungua dakika kumi.
3. Mtoe na uanze kumnyonyoa,hakikisha unatoa manyoya yote makubwa.(yanayoonekana kiurahisi).
4. Mpake unga na umsugue polepole au mbanike kwenye moto wa mkaa (ili kuondoa mabaki ya vinyoya vidogodogo).
5. Mpasue tumbo mtoe vya ndani kama huwa huli kama unakula vitoe na uvisafishe.
6. Katakata vipande tenga jikoni bila kuongeza maji,mpike hadi akauke kama anataka kuungulia.
7.Badilisha chombo cha kupikia then tia maji endelea kupika kawaida hadi aive kisawasawa.
8. Malizia kwa manjonjo yako tayari kwa kula.
Asante sanaa
 
Fata njia zote, lakin ushauri huu wa kumchemsha bila kumkausha achana nao, iyo nyama hautaila. Bata ana shombo flani na kaarufu kabaya sana, kanaishaga mpaka umkaushe kwanza kwa oven au ata mkaa, taratibu moto mdogo at least masaa 3.
Hana tofaut na anavyopikwa kuku ila tu kumnyonyoa ndio kaz weka maji ya moto mtie humo kwa mda wa dak 5 hiv mpaka 10 toa manyoya yote vitabak vimanyoya vidogodogo tumia unga kusafisha akiwa mkavu unga wa sembe,,then kwny mapishi ni uwanja wako tu sasa mchemshe kisawasawa maana anaugum flan hiv.... ukishindwa nikaribishe nije nikusaidie kumpika km Shem hayupo lkn itakuwa vyema
 
Aisee nomaa,sasa inabidi umfanyaje ili upate nyama isiyo na vimanyoya

Tafuta kwenye supermarket kitu inaitwa "duck wax". Ndio suluhisho la vinyoya vidogo. Unampaka hiyo wax baada ya kumnyonyoa manyoya makubwa. Unamuweka kwenye freezer, wax ikiganda unaibandua, inatoka na vinyoya vidogo vyote. Wax hiyo ni re-usable.
 
Nyama ya mbele ya bata ni kavu halafu ya nyuma ina mafuta! Upishi wake ni kama kuku tu,ila usimchemshe bila kumkausha kidogo..sio kwamba hatalika la hasha! Ila ile taste itakua tofauti kidogo.. BTW mpe hongera dogo kwa ushindi.
 
Back
Top Bottom