Msaada: Jinsi ya kupata mtaji wa 500,000 ili kuanzisha mradi wa kuku

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,019
1,671
Habar wanajamvi mimi ni mjasiliamali mdogo nataka Kuanzisha mradi wa kufuga kuku wa kienyeji aina ya kuroiler. Tayari nimeshajenga banda tayari ila pesa yote imeishia kwenye ujenzi wa banda. Nataka kuanza na vifaranga 200 @2500/=ambapo garama yake ni TSh 500000/=sasa naomba msaada na ushauri wapi nitapata mimi niko Tanga.
 
Pole Sana mkuu,upo Tanga sehemu gani?na unataka kwa mkataba gani huyo pesa?
 
Tatizo wew ni Shekau, ningekupa ila kwa kuwa ni Abubakar shekau. Boko haramu
 
Kuanza na idadi kubwa namna hiyo itakua ngumu sana kwa upande wako.
Ufugaji wa kuku ni zaidi ya kulisha ni somo moja kubwa sana.
 
Shida ni vifaranga tu swala la chakula nimejipanga vya kutosha kwani hata mimi mwenyewe ni Mtaalam naweza kutengeneza Home made Ration mwenyewe
Nakushauri anza na wachache tafuta kibarua upate pesa z kuanzia km una ndugu omba msaada hakuna atakaye kupa laki 5 kwa hali hii hata benki hupewi
 
Mi ningekukopesha bila riba ila niliwahi kutiwa mjini kwa kukopesha hivyo hivyo hadi leo sikuzipata.
 
pesaaaaaaaaa , unapataaaa ! ilaaa kwa mkataba! nafikiri itakuwaaa haitoshi hujawekaa gharama ya chanjo, chakulaa na usafiri kuwatoaaa walipo. dawa kwa ajili ya kupuliziaa kwenye banda mpaka wanakuwaa wakubwaaaaaaa! MWISHO WASILIANA NA NDUGU, RAFIKI WA KARIBU WAKUSAIDIE , HATA KAMA NI KIDOGO KIDOGO. AAF UTAWALIPAAA KIDOGO KIDOGO MAMBO YAKIWA SAFI!
 
Banda lako la kuku 200 umetumia gharama kiasi gani? Nataka kujenga hivi karibuni, nahitaji kufahamu makadirio ya gharama za banda. Je 1m inatosha?
 
Habar wanajamvi mimi ni mjasiliamali mdogo nataka Kuanzisha mradi wa kufuga kuku wa kienyeji aina ya kuroiler. Tayari nimeshajenga banda tayari ila pesa yote imeishia kwenye ujenzi wa banda. Nataka kuanza na vifaranga 200 @2500/=ambapo garama yake ni TSh 500000/=sasa naomba msaada na ushauri wapi nitapata mimi niko Tanga.
Nenda FINCA Microfinance Bank watakuelekeza namna ya kupata pesa kwa njia ya mkopo
 
Back
Top Bottom