Msaada jinsi ya kupambana na waturutumbi/wachawi

Koala

Member
Aug 28, 2011
97
107
Jamani mwenzenu nimehamia kwenye ka jumba kangu huku goba,ila toka nimehamia ni shida,kila siku usiku ni fujo tu juu ya bati,mara kama mtu anang'oa misumari mara vitu vinatembea batini.Yani ni tabu tupu. Naombeni ushauri maana sielewi ni wachawi au ni kitu kingine kinasumbua,maana kuna siku mpk nimetoka nje kuangalia batini sioni kitu ila nasikia tu kelele zinaendelea. Kama ni wachawi dawa yao ni nini?
 
Kama ni muislam nyumba isomee ruqya,,
Na wewe ukiwa unalala soma dua za kulala na ayatul kursy.. Mchawi hata akija hakugusi ni kinga tosha..na pia usiache kulala na udhu.
Hapo kama wewe ni muislam.
 
Kabla hujalala tafuta ndulele 7 alafu zitoboe na pini zile za kushonea nguo, kila pini na ndulele yake. Panda juu ya paa fanya uwezavo uzipachike ndulele 3 hapo juu, nyingine tupa nje ya uwanja wako hapo nyumbani. Ukisikia hizo kelele za wachaw juu ya paa usiku amka utamwona mubashara
 
Wakati unaamia kwenye nyumba kwa mara ya kwanza ni vzr kufanya maagano yote yaliyofanyika kwenye ardhi na anga ambapo ipo nyumba yako ni muhimu sana. Kama huwezi kufanya mwenyewe unaweza kuwaita watumishi unaowaamini. Je ulifanya ivyo?
 
Hao ni wachawi,mimi iliwahi nitokea kwenye nyumba yetu moja hivi sehemu moja inaitwa Mtowisa,Sumbawanga,kila ikifika saa saba usiku juu ya bati kunakua kelele na vitu kama vinatembeatembea,kuna siku niliamka nikakuta mlango wa sebuleni umefunguliwa wakati nilifunga kwa komeo kabisa.Hii hali iliendelea ikafika kipindi mama akaanika unga ndani,sebuleni,asubuhi tunaamka tukakuta mguu wa mtu kakanyaga kwenye unga ukionyesha alikua anaelekea chumbani kwa wazazi wetu,asubuhi yake wazazi wakatuita tukaangaliwa miguu yetu,hakuna aliyekua na mguu kama unaofanana na unyayo ule.Kilichokuja kutokea ni kifo cha mzee wangu kwa kuugua,baada ya hapo tulihama tukaenda kijiji kingine,hakika katika kile kijiji tulishangaa sana kwani hatukuwahi kusikia chochote na tulikua tunalala vizuri kabisa tofauti nakule Mtowisa.Kwahiyo mkuu nikuhakikishie kua hao ni wachawi,kuna vitu vingi sana ningeandika hapa kukudhibitishia kua hao ni wachawi kwani hadi ilifika kipindi mimi na baba tulimkamata mmoja.
 
Kwani wanang'oa bati na kuondoka nazo, au wanaziharibu kwa kucheza juu yake?.
Hizo kelele ni nyingi mno? Kama si nyingi sana zipotezee tu.
Mtu angeweza kukuloga au kukuua katu hizo kelele usingezisikia zaidi ya mara moja.Zaidi ya yote okoka na ujazwe Roho mtakatifu, na kama tayari umeokoka basi ondoa hofu.
Kelele hizo unazozisikia si ushara ya kwamba wamekushinda.
.
 
Hao ni wachawi,mimi iliwahi nitokea kwenye nyumba yetu moja hivi sehemu moja inaitwa Mtowisa,Sumbawanga,kila ikifika saa saba usiku juu ya bati kunakua kelele na vitu kama vinatembeatembea,kuna siku niliamka nikakuta mlango wa sebuleni umefunguliwa wakati nilifunga kwa komeo kabisa.Hii hali iliendelea ikafika kipindi mama akaanika unga ndani,sebuleni,asubuhi tunaamka tukakuta mguu wa mtu kakanyaga kwenye unga ukionyesha alikua anaelekea chumbani kwa wazazi wetu,asubuhi yake wazazi wakatuita tukaangaliwa miguu yetu,hakuna aliyekua na mguu kama unaofanana na unyayo ule.Kilichokuja kutokea ni kifo cha mzee wangu kwa kuugua,baada ya hapo tulihama tukaenda kijiji kingine,hakika katika kile kijiji tulishangaa sana kwani hatukuwahi kusikia chochote na tulikua tunalala vizuri kabisa tofauti nakule Mtowisa.Kwahiyo mkuu nikuhakikishie kua hao ni wachawi,kuna vitu vingi sana ningeandika hapa kukudhibitishia kua hao ni wachawi kwani hadi ilifika kipindi mimi na baba tulimkamata mmoja.
Duh!!!hatari sana.
 
Kama ni muislam nyumba isomee ruqya,,
Na wewe ukiwa unalala soma dua za kulala na ayatul kursy.. Mchawi hata akija hakugusi ni kinga tosha..na pia usiache kulala na udhu.
Hapo kama wewe ni muislam.
Hiyo ni dawa toshaaaa hope hatasikia tena maajabu hayo
 
Back
Top Bottom