Msaada: Jinsi ya kumuhamisha mwanafunzi wa Kidato cha Tano

MeruA

JF-Expert Member
Aug 9, 2017
1,391
2,124
Habarini za mchana ndugu zangu,kuna kijana wangu amechaguliwa kujiunga na shule ya Kamagi Sekondari, kidato cha tano (HGL) iliyoko wilaya ya Sikonge mkoani Tabora na kama mnavyojua mwezi ujao wanatakiwa kuripoti shuleni, nimefatilia matokeo yao siyo ya kuridhisha kabisa na hata mazingira pia mtoto naona kama hajavutiwa kabisa kwenda huko,nataka kumtafutia shule nyingine ya serikali hasahasa kanda ya ziwa Mwanza, Geita, Shinyanga.

Kwanini Kanda ya Ziwa?

Ana changamoto ya kiafya hivyo nataka awe mikoa ya karibu ili hata inapotokea dharura iwe rahisi kufika na kumpa msaada.

Taratibu za uhamisho kwa shule za kidato cha tano zipoje??
Naombeni msaada, Natanguliza shukrani zangu.
 
Wahi shule aliyopangiwa ili ukaonane na mkuu wa shule then ufanye taratibu kabla hajaainishwa kweny usajiri wa shule.
 
Naomba msaada nimehitim kidato Cha 6 mwaka huu 2020 na nimepata CHEMISTRY E, BIOLOGY E $ GEOGRAPHY D Naweza kwenda chuo kikuu chochote
 
Back
Top Bottom