Jinsi ya ku-tangaza Biashara yako kwa Facebook (sponsered ads) - P.01

Oct 19, 2020
75
232
Habari, I hope u mzima wa afya unavyopitia thread hii. na kama hauko poa, i pray urudi katika afya yako mapema.

To cut the story short, Leo nitaelezea jinsi ya kutangaza biashara yako kwa Facebook ads (matangazo ya Facebook), kama haufahamu Facebook ads ni nini basi fanya hivi :- Fungua instagram yako, utagundua kila ukiscrol baada ya posts tano za watu/page ulizofollow utaona post iliyoandikwa sponsered chini ya jina la hiyo account/page, na hauijafollow account/page hiyo.

Si lazima kuwa na biashara tu kutangaza kwa FB ads, unaweza kukuza personal account (IG na FB) yako pia kupitia hii njia.. Na mostly important ni elimu ya bure ambayo itakusaidia sana kujiajili au kuajiliwa maana makampuni/watu wengi wanahitaji huduma hii na wengi wao hawajui wapi pa kuanzia.

Watu wengi wamekuwa waki-boost matangazo au account zao bila kutumia Facebook ads buit-in business feature, Ambapo si effective au sahihi. Tofauti yake ni kwamba, unaweza uka-boost matangazo yako kwa Facebook au instagram kwa simu Lakini huwezi ku-set Facebook ads kwa simu, so kama ulishawahi kutumia simu (smart phone) yako kufanya hivo, Basi hujakosea bali hukutumia platform ipasavyo kupata matokeo chanya zaidi.

Umuhimu wake ni nini haswa?
kwa kutumia Facebook ads, haijalishi uwe biashara ndogo ama kubwa, utapata uwezo wa kufikia kwa kutarget watu specific wenye uhitaji au interest na bidhaa yako popote pale duniani, nchini, au mkoa husika, pia unaweza kukuza brand awareness ya biashara, event au chochote kile unachohitaji kiwafikie watu wengi kwa mda mchache. Ukifahamu startegies nzuri za kutarget watu uliokusudiabasi utafikia wateja/watu wengi ambayo wataochukua action ya ulichokusudia katika tangazo lako.

Pia, Facebook ads inakupata uwezo wa kuelewa data au behaviour za wateja wako bila kubashiri au kukisia, Utaona ni nini au mkoa/sehemu gani inayokuletea wateja wako zaidi hivyo utalenga kinachofanya kazi na sio kujaribu jaribu. You’re provided with metrics about your weekly reach, post engagement, page likes, and which posts have the best performance kitu ambacho kitasidia biashara yako kukua zaidi kuliko kutumia traditional ways of marketing. ( kuweka mabango, redioni nk)

Faida ni nyingi, tuaendelea kudiscuss more na pia bila kusahau cons zake...

Facebook inawezaje kuwapata/kuwafikia wateja wangu haswa?
Kila mwezi Facebook ina zaidi ya 2.5 Billion active users ambao huonyesha interests ya vitu mbalimbali vinavyozunguka katika mtandao huo, Lets say wewe ni mfatiliaji mzuri wa bidhaa za nguo na ume-like page mbalimbali za maduka ya nguo au designers. Facebook huchukua data hiyo na kukuonyesha zaidi matangazo ya nguo ili ununue au ufollow/ulike (kulingazo na action ya tangazo husika) . Na matangazo hayo ndio facebook ads, Hivyo basi ukifahamu namna ya kuset up matangazo haya facebook itakupatia data kamili/nzuri itakayokufanya uwafikie wateja wako husika.


Unahitaji nini kuanza na Facebook Ads?
1) Facebook account: - Ni LAZIMA uwe na Facebook account uweze kupromote/kufanya matangazo haya, Instagram si lazima ila ukiihitaji basi utaiconnect na Facebok account yako. Hii ni kutokana na kuwa Facebook ndio parent company katika makampuni yote ikiwemo instagram, whatsapp, messenger, marketplace n.k. Hivyo account yako ya Facebook kama Markerter au mfanya biashara ina umuhimu mkubwa sana. Na kama utahitaji kuonyesha matangazo yako Instagram tu na si Facebook bado utahitaji acc yako ya Facebook.

2) Facebook Business Manager: - Hii ni built-in feature ambayo inakupatia uwezo wa kuorganize kila kitu kuhusiana na Facebook ads/matangazo yako, Ndani ya FB business manager kuna ads account, Pages (IG & FB), Pixels, Users (watu watakao endesha matangazo hayo, kama mtashirikiana), Catalogs, Domains, Event manager na assets nyingine nyingi. - Kila mtumiaji wa Facebook anayo hii feature ila si wote wanaofahamu au kutumia. Kucreate Facebook Business manager ni bure na simple.

3) Payment credit/debit card:- Biashara yako kufikia maelfu ya watu ambao hawajakufollow ama kukufahamu haiwezi kuwa bure, Hivyo Ku-run Facebook ads si bure, na utahitaji card yoyote inayokubali malipo ya mtandaoni kulipia matangazo hayo.

Malipo ya Facebook ads hulipwa kulingana na unavyotumia, na haikupangii kutumia kiasi gani kwa masaa, siku, wiki au mwezi. unaweza kuanza na $3 (7,000 TZS) kwa siku, hivyo siku ikiisha utatumia $3 nyingine siku ijayo. Kama bajeti yako si rafiki basi unashauriwa u-set starting time/date to ending time/day kuepuka kutumia zaidi ya ulichotegemea ama ukiona haitoshi weka spending limit.

Hii topic ni kubwa sana thus siwezi maliza kila kitu kwa thread moja therefore stay in touch nitaendelea kupost more, na ukihitaji kufahamu zaidi unaweza kuuliza swali lolote kenye comments na kwa watakaohitaji kuona practically, nimeupload video Youtube kwa kiswahili. Kuna resource nyingi za kufahamu zaidi juu ya hii topic si lazima kwangu tu.

That's it for today! Have a Blessed weekend! - Thanks.
 
Hivi karibuni nimefungua biashara uchwara ambayo imekuwa ikinipatia pesa ya kubadili mboga na kutunza familia.

Kwa sasa nimeona ni vyema kama nitaifanyia promo kwenye social media hasa facebook ili kupata wateja wengi. Tatizo linakuja namna gani naweza lipia tangazo (kufanya malipo). Msaada tafadhali kwa yoyote mwenye ujuzi
 
Bonjour

Naomba msaada wa kufanya malipo ya kulipia Matangazo ya biashara Facebook ( Fb ads) Kwa kutumia Mpesa Master card

Nimejaribu nimeshindwa,

Msaada wenu, wazoefu
 
Malipo ya Facebook ads hulipwa kulingana na unavyotumia, na haikupangii kutumia kiasi gani kwa masaa, siku, wiki au mwezi. unaweza kuanza na $3 (7,000 TZS) kwa siku, hivyo siku ikiisha utatumia $3 nyingine siku ijayo. Kama bajeti yako si rafiki basi unashauriwa u-set starting time/date to ending time/day kuepuka kutumia zaidi ya ulichotegemea ama ukiona haitoshi weka spending limit.
Aisee 😁
 
Back
Top Bottom