gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,283
- 3,271
Vifaranga kama vinapewa chanjo zote kama nilivyokwambia,ukawa unavipa multi vitamin,lakini pia uzingatie dawa ya minyoo,baada ya hapo mara nyingi sana tatizo hua ni magonjwa ya matumbo ambayo dawa yake ni ant biotic vifaranga hawawezi kufa.Kinyesi chao unatakiwa ukifuatilie mara kwa mara kwani magonjwa ya matumbo huo utayatambua kupitia kinyesi.Mfano ukiona wanaharisha kinyesi cha rangi ya brown jua hilo ni tatizo la ugonjwa wa coccidiosis na dawa ni ant biotic kama otc 20%.Kikubwa upende kujifunza na kuwa nao karibu.samahani mkuu umenigusa sana....naomba maelekezo kidogo juu ya kutoa hiyo chanjo,vifaranga wangu wamekufa wote
Nakumbuka mwaka juzi nilinunua tetea 12 na jogoo moja mwezi wa pili lakini ndani mwaka ule nilikua na kuku wasio pungua 200 badae nilipata matatizo ya usimamizi shamba baada ya kua na mambo mengi nikaacha kufuga.Hili ni rahisi sana pia kwani mimi sijahadithiwa kwani nilifanya mwenyewe tena nikiwa na vifaa dunu kabisa.
Nilitengeza vibanda vyenye wastani wa futi tatu kwa tatu na urefu wakawaida hata futi mbili nikaziba sehemu zote nakuacha sehemu ya mbele niliweka nyavu.Lakini huku kwenye nyavu niliweka kitu mithili ya pazia kuniwezesha kufunga na kufungua ili ku control joto na mara nyingi usiku nilifunika kwasababu ya baridi.
Vibanda nilifanya vidogo hivyo kwani nilitumia taa za kandili/chemli kama chanzo cha joto hivyo kama eneo litakua kubwa ni vigumu kupata joto lakutosha.lakini pia nilitumia vyumba hivi vidogo kwani uzalishaji wangu wa vifaranga nilitumia kuatamishia kwa mama kuku hivyo ilikua ni kidogo.
Nilichokua nafanya kuku anapototoa nampokonya vifaranga siku hio hio nakuviweka kwenye hivi vitunzio vyangu wataalamu wanaita(bruda),Unapofanya hivi kama huyu kuku utampatia chakula akashiba ndani ya siku 20 anaanza kutaga tena hivyo mzunguko wakuzalisha unakua mkubwa.
Vifaranga nilikua navipatia chakula cha starter hii huvifanya kukua haraka lakini pia hua na afya bora pamoja na uwezo wakuhimili magonjwa.
Kikubwa kila kitu kinawezekana chamsingi kua makini na wafuatilie kwa ukaribu utafanikiwa