MSAADA : Jinsi ya Kuingiza Piano Kwenye Beat kwa Kutumia Fruit Loops (FL Studio)

Mkuu, kuliko kuhangaika na hiki kitu kimoja kwa nini usidevelop passion ya muziki na ukajifunza from scratch, ukafanya makosa machache ambayo yatakufanya uwe producer mzuri zaidi. Utajipatia kazi yenye malipo mazuri na kukutana na watu wanaopenda muziki kama wewe.
Ingia Youtube pitia walkthrough ya fl studio. Lakini usitake kukariri vitu just angalia vitu muhimu na jinsi ya kuvipata. Kama Piano roll, drum kits, installing VST plugins, effects, baadhi ya mbinu katika piano roll n.k.
Baada ya hapo ukajifunza Music Theory, kuna youtube channel ya Hack Music Theory wako vizuri sana, watakupa na free ebook ujifunze music theory. Baada ya hapo unaweza ukajifunza hata instrument moja ili kupanua wigo wa ujuzi wa muziki. Then ukaanza kutengeneza beats.
Cha muhimu kuwa experimental sana. Jaribu kutengeneza vitu original na vya kwako mwenyewe. Utafurahia sana na itakuongezea hata ubora wa maisha yako. Muziki ni tiba nzuri sana. Imagine unaamka asubuhi unatengeneza kitu ambacho hakikuwepo bado, thats creativity.
Nikipata muda ntatupia baadhi ya kazi zangu uzisikilize.

Niache Nteseke

Mkuu unachosema ni sahihi kabisa kiongozi ila kuna beat nilitaka niifanyie kazi ila katika uandishi kuna piano flani nilitaka niiweke ili iweze kunipa vibes zaidi katika kuandika na kupita mipito pia mkuu.

That's why nikasema uniulize wadau tuone jinsi gani mnaweza mkanisaidia mkuu.

Pia itakuwa baab kubwa ukitupia ladha tukapata vibes kiongozi. Shusha nondo mkuu.
 
Sanaaaaa.....yaani nikija balaa lake nakuja kuwa msanii mkubwa Zaid ya Diamond....namkubali Sana Dj Premier,Dre,Pete Rock,Appolo Brown,Duke,P Funk na wengine wengi
Duke The Tanchez, Pallah, Daz Naledge, P-funk, J-Ryder, Hawa jamaa midundo yao sio ya kawaida aisee jamaa wanajua kusuka ngumu! Sijui washaishia wapi tu baadhi yao kama Pallah na Daz Naledge 😢
 
Duke na .Palllah wapo....Bin laden naye noma
Ebana kama una pini za Bin Laden nisaidie mkuu make ninazo chache sana (majina tu ya nyimbo yanatosha), Namkubali mno yule mwamba, Bila kumsahau Marco Chali daah nae si haba kwenye kuunda beats nzuri za kuimba ana radha flani hivi kwenye beats zake.. Na kuna RashDon yule!
 
Hiyo delay huwa inajitokeza unapoweka mp3 song kwenye FL mkuu...? Na huwa inakuwa kwenye mp3 uliyoiweka au kwenye instruments utakazozipiga juu ya hiyo beat kiongozi...?
Huwa kwenye mp3 file na huwa xported kama silence kwenye DAW nyingi unapoexport mp3, kwasabu kitendo cha ku export track kwenye DAW Kama mp3 ni sawa na kupunguza size na quality ya track nzima, ilihali vifaa vingi vinaplay mp3 files.
Huku ku-calculate track bpm kwa google ni kwa kutumia software, website au una-search name of the track kupitia google mkuu...?
Angalia google jinsi ya kucalculate bpm ya tempo unayoipenda, then unapofanya mixing unacross multiply delay yako na delay unayoifanyia kazi then utaweza pata details zote za hiyo tempo unayoifanyia kazi.

Details gani nitazi-miss kiongozi wakati wa kufanya rendering...?. Piano sio mtaalam saaaaan ila kwa kutumia sikio naweza kujua tu kuwa kuna kitu kipo mje ya key mkuu.
Instrument zitakuwa compressed kwenye same wav hivyo zitakuwa hazijajitenga kila moja kivyake, hautokuwa huru kufix detail ya kila sauti.

Don't forget to route into different mixer tracks, unaweza kunifafanulia hapo kiongozi...?
Unaporoot ktk different mixer track manaake kila kifaa kitakuwa na mix track yake, hivyo utaweza icontrol hiyo beat kama ilivyo na instrument utakazoongeza kama zilivyo
Natanguliza shukran kwako mkuu.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom