msaada:jinsi ya kufanya donations kuwa endelevu kwa wanafunzi wasiojiweza

snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,407
1,110
habari wanaJF,nina swali langu na ningependa sana kupata maoni yenu.naomba uchukulie kama ingekuwa wewe ungetumia njia gani.tuseme unataka kutoa ufadhili kwa watoto wasio na uwezo wa kukidhi gharama za masomo yao hadi hapo watakapofikia,ukawakusanya katika kituo na wakajua kwamba ni wewe unayewalipia gharama za chakula,stationery na malazi wawapo shuleni,na baada ya kumaliza kwao masomo,ungependa wao pia wasaidie watoto wengine ambao watakuwa hawana uwezo wa kujisomesha kwa kipindi hicho,je utafanyaje ili wawe dedicated kujitolea kwa watoto wa kizazi kijacho wasio na uwezo?......tafadhali comment ungefanyaje,au ungetumia njia gani,nashukuru sana kwa mchango wako.
 
asante kwa swali zuri,
Nimekuwa nikisaidia wanafunzi lakini ni via mwalimu anayefanya kazi huko umasaini Arusha,
Changamoto nayoiona ni kuwa watakiwa kupata mtu mwaminifu, kwani hawa wanafunzi wengine shida yao sio malazi watalala kwao shida ni ada, ada za mitihani, na vifaa. Pia some sight ya kuwasaidia wasome kwa bidii kwani wengine wanafanya ni mazoea, hawalipi swala la shule uzito kutokana na ignorance iliyopo kwenye jamii wanayoishi.
Kuna watu wanaitwa Global Partners, huwa wanasponsor wanafunzi lakini nao huwa wanatumia middle man,
Hivi hivi huwezi kwani wewe utakuwa huishi kule kwenye maeneo ambayo wanafunzi wanaishi.
Sijui kuPM tungejadili vya kutosha.
 
Sijakupata vizuri uliposema kuwakusanya pamoja kwa maana ya kuanzisha kituo kama shule ama kituo cha kuwalelea huku wakisoma shule tofauti tofauti. Ila kama ukianzisha shule ni rahisi zaidi kwa maana ya kiasi cha kutafuta eneo na kujenga madarasa japo utakuwa na gharama nyingine ya kulipa walimu na wafanyakazi wengine ila ni njia rahisi zaidi kuwapata watoto. Au ujenge kituo cha kulea watoto ambao wakuwa wanasoma shule tofauti tofauti na hapo itabidi uwe na gari la kuwapeleka mahali husika wakakokuwa wanasomea,ila pia unaweza ukaongea na mameneja wa shule husika wakawa wanakuja kuwachukua ktk kituo chako. Kingine ni kutoa matangazo yanayotaka kuwasaidia kuwasomesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu wakiwa majumbani kwao,hapa unaweza kuandaa fomu ambazo zitaainisha lengo lako na hatima ya wanafunzi pale watakapokuwa wakubwa. Na hii itakuwa rahisi endandapo utakuwa na website yako ambamo utaweka kila kitu unachotaka ikiwa ni pamoja na fomu. Ila sijajua kama unatoa hiyo kwa watoto wadogo tu au hata watu wazima? Maana tatzo liko hata kwa wakubwa pia!
 
Msenyele,hii ni kwa watoto wa elimu ya msingi na wa sekondari wasio na uwezo wa kujilipia shule,na wale ambao kipato cha familia yao hakikidhi gharama za shule.sio lazima wasome shule moja,wanasoma shule tofauti tofauti na wanarudi nyumbani jioni,kwa wale wakubwa wanapelekwa kwenye boarding schools ili wapate exposure zaidi,kituo kipo ila sio sehemu yao ya kujifunzia,ni kwa watoto wadogo tu na wale ambao ni orphans...swali langu ni kwamba,,kama wakisaidiwa sasa mpaka watakapomaliza elimu yao,watawezaje kusaidia wenzao kama imi nilivyowasaidia?nitumie njia gani?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom