Msaada: Jinsi ya kuagiza gari la mizigo kutoka UK

Mzalendowadamu

JF-Expert Member
Jul 10, 2016
219
500
Natoa salamu za heshima kwenu nyote wadau wa jukwaa hili pendwa. Mwaka 2016 niliomba ushauri humu na kusadiwa kuhusu kuagiza gari toka Japan na kufanikiwa kwa asilimia mia, nasema asanteni sana kwa mara nyingine.

Sasa nimerudi kwenu kuomba tena msaada wa ushauri wenu kuhusu namna ya kuagiza gari toka barani Ulaya. Lengo langu ni kununua gari la mizigo lenye uimara na ikiwezekana liwe na unafuu wa bei. Katika kuzungumza na wadau kadhaa hasa madereva wa haya magari makubwa ili kupata machache ya awali, wengi wao wamenishauri kununua Scania, Pia iwe ya kichwa kinachovuta trailer(wakimaanisha ndizo zinaweza kubeba mzigo mkubwa) na vilevile upatikanaji wa vipuri.

Ombi langu kwenu wanajukwaa hili ni hasa kujua Makampuni ya kuagizia gari hizi toka UK, pia kujua website ya makampuni hayo hasa yaliyo salama na fanisi ikiwezekana yenye mawakala hapa Tazania kama ilivyo kwa beforward. Kwa yeyote mwenye kujua lolote kuhusu gari gani ni imara au inayofaa kwa kazi za mizigo mizito kwa ubora wowote kuanzia uimara, matumizi ya mafuta na sifa zingine basi nawaomba sana mnitoe ujinga. Pia ningependa kujua namna ya kupata trailer imara kwa hapa Tazania.

Natagemea msaada wenu.

Asanteni sana na karibuni sana.
 
Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,385
2,000
Natoa salamu za heshima kwenu nyote wadau wa jukwaa hili pendwa. Mwaka 2016 niliomba ushauri humu na kusadiwa kuhusu kuagiza gari toka Japan na kufanikiwa kwa asilimia mia, nasema asanteni sana kwa mara nyingine...

Mkuu, ingia website ya autotraderuk na utafute hizo chasis za Scania.

Nenda sehemu ya tracks.
1540048717982.png

1540048870132.png

Kama hii imekimbia kilomita 124420 na ni ya 2003

Yatumia diesel na imetumiwa na watu wawili yaani 2 owners.

Inabidi ujipange kwelikweli.
 
Teknologist

JF-Expert Member
Oct 20, 2018
675
1,000
Babu kama kweli unataka Truck tuwasiliane PM,

Kumbuka unataka gari ya mwaka gani? hii ni muhimu kwenye ushuru! sababu gari ikiwa nzee zaidi ya miaka nane toka imeuundwa, utalipa ushuru mkubwa! japo kuwa gari itakuwa bei rahisi kununua.

Je kiasi gani? hata hii inaumuhimu kwenye ushuru! Pia uwe na hela ya usafirishaji,mimi nataeenda kukuangaliazia na kuvideo gari live kuwasiliana na wewe.

Na hela hunitumii mimi, Lazima uhakikishe kampuni inayouza ni ya kweli ndio unatuma kwenye akauti yao. Lakini lazima unilipe hela yangu ya kwenda kukuangalizia gari na marupurupu yangu
 
Mzalendowadamu

JF-Expert Member
Jul 10, 2016
219
500
Babu kama kweli unataka Truck tuwasiliane PM,
Kumbuka unataka gari ya mwaka gani? hii ni muhimu kwenye ushuru! sababu gari ikiwa nzee zaidi ya miaka nane toka imeuundwa, utalipa ushuru mkubwa! japo kuwa gari itakuwa bei rahisi kununua
Je kiasi gani? hata hii inaumuhimu kwenye ushuru!
Pia uwe na hela ya usafirishaji,mimi nataeenda kukuangaliazia na kuvideo gari live kuwasiliana na wewe,
Na hela hunitumii mimi, Lazima uhakikishe kampuni inayouza ni ya kweli ndio unatuma kwenye akauti yao
Lakini lazima unilipe hela yangu ya kwenda kukuangalizia gari na marupurupu yangu
Wazo zuri Asante sana, lakini ngoja kwanza tupate mawazo zaidi ili tujue hata tunachagua gari kwa vigezo gani.
 
KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
May 17, 2018
246
500
Natoa salamu za heshima kwenu nyote wadau wa jukwaa hili pendwa. Mwaka 2016 niliomba ushauri humu na kusadiwa kuhusu kuagiza gari toka Japan na kufanikiwa kwa asilimia mia, nasema asanteni sana kwa mara nyingine...
Usipate tabu Mkuu, KIMOMWE MOTORS ni suluhusho la hitaji lako. Hii ni kampuni ya Kitantania iliyoingia mkataba na kampuni zaidi ya 12 za Japan na Ulaya.

Tunabeba dhamana ya pesa yako kuhakikisha gari uliyoikusudia inakufikia ikiwa katika ubora.

Karibu ofisini kwetu Magomeni Mapipa jengo lenye bank ya DTB tupo ghorofa ya kwanza. Au piga 0754 455865
 
Mzalendowadamu

JF-Expert Member
Jul 10, 2016
219
500
Usipate tabu Mkuu, KIMOMWE MOTORS ni suluhusho la hitaji lako. Hii ni kampuni ya Kitantania iliyoingia mkataba na kampuni zaidi ya 12 za Japan na Ulaya.

Tunabeba dhamana ya pesa yako kuhakikisha gari uliyoikusudia inakufikia ikiwa katika ubora.

Karibu ofisini kwetu Magomeni Mapipa jengo lenye bank ya DTB tupo ghorofa ya kwanza. Au piga 0754 455865
Asante kwa taarifa, lakini ungeeleza kiundani zaidi ili tujue kama ninyi mnauza magari au ni madalali. Pia ungeweka link za hayo makampuni ili watu watoe ushuhuda kwa faida ya wengi na biashara yako pia. Ni vema ukaenda deep kidogo kwani naamini wapo weni wenye hitaji kama langu.
 
Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,385
2,000
Asante kwa taarifa, lakini ungeeleza kiundani zaidi ili tujue kama ninyi mnauza magari au ni madalali. Pia ungeweka link za hayo makampuni ili watu watoe ushuhuda kwa faida ya wengi na biashara yako pia. Ni vema ukaenda deep kidogo kwani naamini wapo weni wenye hitaji kama langu.

Mkuu, umetembelea tovuti mubasahara kabsa ya www.autotrader.co.uk?
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,708
2,000
30m unapata gari nzuri tu scania ukiangalia kwenye web za uk
Makampuni ni mengi yanayouza
Hapo ni kutafuta mpaka usafirishaji mpaka Dar
 
KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
May 17, 2018
246
500
Asante kwa taarifa, lakini ungeeleza kiundani zaidi ili tujue kama ninyi mnauza magari au ni madalali. Pia ungeweka link za hayo makampuni ili watu watoe ushuhuda kwa faida ya wengi na biashara yako pia. Ni vema ukaenda deep kidogo kwani naamini wapo weni wenye hitaji kama langu.
Message Body
Jina la kampuni ni Kimomwe Motors Tanzania Limited. Kampuni hii imesajiliwa kama Mwagizaji wa Magari mapya na yaliyotumika kutoka Japan na Ulaya pia.

Tulichofanya ni kuingia makubaliano ya kuwakilisha baadhi ya makampuni ya kijapan na Ulaya lengo kuu likiwa ni kumrahisihia mtanzania aweze kupata gari kwa gharama nafuu zaidi kutoka na ushindani unaokuwepo kwenye kampuni tunazofanyanazo kazi. Pia mteja anakua na wigo mpana zaidi wa kufanya chaguo la kilicho bora zaidi. Faida nyingine ukiagizia kupitia sisi unanafasi ya kupata punguzo la bei tofauti na ukiagiza mwenyewe ambapo punguzo laweza kua dogo au lisiwepo kabisa.

Ili mteja awe na uhakika na usalama wa pesa yake, kuna mikataba ambayo tunasainishana chini ya mwanasheria au mahakama kwamba sisi Kimomwe Motors tunabeba dhamana ya mteja mpaka tutakapomkabidhi gari yake ikiwa kwenye ubora uliokusudiwa.

Baadhi ya kampuni tunazoshirikiana nazo ni kama Beforward Japan, SBT Japan, Tradecarview, Cardealpage, Sakura Motors, Real Motors Japan, Enhance Auto, Autorec, Car Junction, na Law Exports UK.

Hapa chini naambatanisha na baadhi ya nyaraka zetu za kisheria zinazoturuhusu kufanya kazi hizi pamoja na moja ya Tuzo ambazo Mkurugenzi wetu amekua akipata kutoka Beforward kabla hajaamua rasmi kusajili kampuni hii Kama Kimomwe Motors Tanzania Limited.

Makao makuu ya ofisi zetu yapo Dar es Salaam maeneo ya Magomeni Mapipa mkabala na kituo cha Mwendo kasi, ilipo bank ya DTB, sisi tuko ghorofa ya kwanza. Ofisi ndogo zipo Kurasini mkabala na Chuo cha Uhasibu, jengo la Masangula ofisi namba 3.

Kwa mawasiliano zaidi, piga sim namba 0754 455865

Kimomwe Motors- Save Money, Save Time
award.jpg

TIN.jpg
license0.jpg
CERT.jpg
 
Mzalendowadamu

JF-Expert Member
Jul 10, 2016
219
500
Message BodyJina la kampuni ni Kimomwe Motors Tanzania Limited. Kampuni hii imesajiliwa kama Mwagizaji wa Magari mapya na yaliyotumika kutoka Japan na Ulaya pia.

Tulichofanya ni kuingia makubaliano ya kuwakilisha baadhi ya makampuni ya kijapan na Ulaya lengo kuu likiwa ni kumrahisihia mtanzania aweze kupata gari kwa gharama nafuu zaidi kutoka na ushindani unaokuwepo kwenye kampuni tunazofanyanazo kazi. Pia mteja anakua na wigo mpana zaidi wa kufanya chaguo la kilicho bora zaidi. Faida nyingine ukiagizia kupitia sisi unanafasi ya kupata punguzo la bei tofauti na ukiagiza mwenyewe ambapo punguzo laweza kua dogo au lisiwepo kabisa.

Ili mteja awe na uhakika na usalama wa pesa yake, kuna mikataba ambayo tunasainishana chini ya mwanasheria au mahakama kwamba sisi Kimomwe Motors tunabeba dhamana ya mteja mpaka tutakapomkabidhi gari yake ikiwa kwenye ubora uliokusudiwa.

Baadhi ya kampuni tunazoshirikiana nazo ni kama Beforward Japan, SBT Japan, Tradecarview, Cardealpage, Sakura Motors, Real Motors Japan, Enhance Auto, Autorec, Car Junction, na Law Exports UK.

Hapa chini naambatanisha na baadhi ya nyaraka zetu za kisheria zinazoturuhusu kufanya kazi hizi pamoja na moja ya Tuzo ambazo Mkurugenzi wetu amekua akipata kutoka Beforward kabla hajaamua rasmi kusajili kampuni hii Kama Kimomwe Motors Tanzania Limited.

Makao makuu ya ofisi zetu yapo Dar es Salaam maeneo ya Magomeni Mapipa mkabala na kituo cha Mwendo kasi, ilipo bank ya DTB, sisi tuko ghorofa ya kwanza. Ofisi ndogo zipo Kurasini mkabala na Chuo cha Uhasibu, jengo la Masangula ofisi namba 3.

Kwa mawasiliano zaidi, piga sim namba 0754 455865

Kimomwe Motors- Save Money, Save Time View attachment 908014
View attachment 908000 View attachment 908003 View attachment 908011
Sawa mkuu, tutawasiliana kiofisi.
 
kiraremapojoni

JF-Expert Member
Nov 30, 2018
389
500
MAJINA YANATOFAUTIANA KATI YA TIN NA NYARAKA NYENGINE HAKIKISHA UNABADILISHA MAPEMA KUONDOA USUMBUFU HUKO SIKU ZA MBELENI
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom