Msaada: Jinsi gani ninaweza kutuma mzigo mdogo kwa kupitia shirika la posta kwenda Finland

PastorA

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
361
275
Wakuu habari za leo
Ninaomba msaada wa taarifa kutuma bahasha ndogo nchi za nje hususani nchi ya Finland kwakutumia shirika la Posta naomba taarifa mwenye taarifa zozote nimewapigia simu bila mafanikio naomba kwa wazoefu.. Bahasha yenye uzito wa nusu kilo.
Naomba kujua Gharama zake
 
tuma kwa ems, nenda ofisi yeyote ya posta. Mi nshawahi tuma belgium, haiwezi zidi 40
 
tuma kwa ems, nenda ofisi yeyote ya posta. Mi nshawahi tuma belgium, haiwezi zidi 40
Mkuu haiwezi zidi 40 yaani elfu 40,000/= au?
Alafu
Nashindwa kwa sasa coz wamefunga ndio maana naomba mdaada
 
Kwanza unatuma kitu gani? Maana kuna vitu huwezi tuma mpaka uwe na kibari... mfano vitu jamaa ya chakula, ngozi za wanyama hata wafugwao
 
nenda posta kaulize utaratibu, hapa sidhani kama kuna mtu anajua gharama hizo,
kwa maana wanatoza kutokana na uzito na mahala mzigo unapokwenda, niliwahi kupeleka kilo 29 posta kutoka mkoa hadi mkoa walinichaji hela nyingi mpaka nikaahirisha na kuamua kutuma kwa basi, sikumbuki ilikuwa sh ngapi, ila ilikuwa kama sh 60000
 
Back
Top Bottom