Msaada: Jeshi likichukua nchi huduma za kijamii zinatolewaje? Mishahara pia inakuwaje?

IBRAHIM KAUKI

JF-Expert Member
Jan 14, 2014
542
210
wakuu,naombeni kujua ikiwa jeshi limetwaa madaraka nchi Fulani je huduma za kijamii hutolewaje?
mishahara kwa watumishi n.k?
na kodi hukusanyweje?
 
Jeshi likichukuwa nchi wanaoondolewa ni wana siasa. SWatendaji na wataalamu huendelea na kazi kama kawaida. Ni kama vile Chadema ikichukuwa nchi anaingia rais mwingine. Mabenki, TRA, Viwanda, Mahospital nk huko hawaendi. Ila ukifanya ufisadi wakati wa utawala wao wanakuuwa.
 
Kama ni kwa nia njema hakuna kitakachobadilika zaidi ya utawala tu.

Ila kama ni kwa urafi wa mtu binafsi,huwa ni vurumai mambo yote huwa yanapoteza utaratibu.maana kinachofuata huwa ni fukuza fukuza/kamata kamata na kupachika wanajeshi kila eneo.
 
Jeshi likichukuwa nchi wanaoondolewa ni wana siasa. SWatendaji na wataalamu huendelea na kazi kama kawaida. Ni kama vile Chadema ikichukuwa nchi anaingia rais mwingine. Mabenki, TRA, Viwanda, Mahospital nk huko hawaendi. Ila ukifanya ufisadi wakati wa utawala wao wanakuuwa.
Umemaliza kila kitu mkuu.
 
Kila kitu kinaendelea kama ipasavyo vile, wanaopindua huwa wanataka kupachika kibaraka wao tu! hawataki machafuko na ndio maana utasikia kuitishwa upya uchaguzi wa kidemokrasia zaidi. Na ndio maana mapinduzi huwa yanatega upepo wa raia, raia.
 
Mambo huendelea kama kawaida na watumishi wanaotoa huduma huendelea na ajira zao japo uongozi wa serikali kuu ndiyo hubadilika. Pia kutakuwa na mabadiliko hapa na pale yawe mazuri au mabaya.
 
wakuu,naombeni kujua ikiwa jeshi limetwaa madaraka nchi Fulani je huduma za kijamii hutolewaje?
mishahara kwa watumishi n.k?
na kodi hukusanyweje?

HABARI,
"IBRAHIM KAUKI,
Huduma zotehuendelea kama kawaida ila huwa kunakuwa na mtikisiko kidogo kutokana na mabadiliko ya uongozi ila huduma zote ulizoziulizia huendelea kama kawaida.Ila tu kama kusipo kuwa na machafuko katika mpito huo.Ila kama machafuko yakitokea hapo tofauti huwa makubwa hasa huduma za afya ndio mashirikia mengi ya kimataifa huingilia kati na kutoa ila huduma nyingine huyumba mishahara huwepo kwa wanajeshi na vyomba vya usalama hasa wale walioshikilia dola.

LUMUMBA
 
Jeshi likichukuwa nchi wanaoondolewa ni wana siasa. SWatendaji na wataalamu huendelea na kazi kama kawaida. Ni kama vile Chadema ikichukuwa nchi anaingia rais mwingine. Mabenki, TRA, Viwanda, Mahospital nk huko hawaendi. Ila ukifanya ufisadi wakati wa utawala wao wanakuuwa.
Nzuri hiyo nzuri sana
 
asante mkuu
 
HABARI,
"IBRAHIM KAUKI,
Huduma zotehuendelea kama kawaida ila huwa kunakuwa na mtikisiko kidogo kutokana na mabadiliko ya uongozi ila huduma zote ulizoziulizia huendelea kama kawaida.Ila tu kama kusipo kuwa na machafuko katika mpito huo.Ila kama machafuko yakitokea hapo tofauti huwa makubwa hasa huduma za afya ndio mashirikia mengi ya kimataifa huingilia kati na kutoa ila huduma nyingine huyumba mishahara huwepo kwa wanajeshi na vyomba vya usalama hasa wale walioshikilia dola.

LUMUMBA
asante Mkuu kwa ufafanuz
 
Back
Top Bottom