Msaada: Je ni benki gani inafaa kwa kufungua account ya biashara?

Biashara yangu sio ya kifisadi
Mkuu kwa ajili ya biashara kama ni SME, basi fungua akaunti kwenye hizi bank ambazo si kubwa. Kwa mfano Access, DTB, Equity au hata Azania. Haya mabenk makubwa kama CRDB mara nyingi yanakuwa siyo individual customer oriented, wana deposits nyingi mno kiasi kwamba ukiwa na kibalance chako kidogo let say 100m unakuwa ni kapuku tu. Lakini kwa hizo bank nyingine unaweza hata kunegotiate FDR.
 
Habari zenu wana JF. Mimi ni mfanyabiashara. Nina kampuni yangu ambayo nimeianzisha hivi karibuni ambayo ninataka kuifungulia account yake. Ninaomba msaada wenu kwa yeyote mwenye ufahamu wa kutosha kuhusu mambo ya mabenki aweze kunishauri benki nzuri inayofaa kwa kufungua account ya biashara au kampuni. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa yeyote ambaye atajitokeza kunisaidia katika hili. Asante

Usijali kaka nenda AccessBAnk Tanzania limited ( ABT) ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wadogo , akaunti ya biashara utafungua kwa kiasi kidogo kabisa cha shilingi elfu 50, na utaweza kupata kitabu cha hundi kwa shilingi elfu nane(Kurasa 25) au elfu 15 ( kurasa 50).
Mjomba masharti yao ni rahisi kabisa
-MEMART
-tiN CERTIFICATE
-LESSEN ya biashara
-Ids za directors
-minutes za kikao.
nenda kaka ABT watakusaidia kwa maswali mengine zaidi.
 
nimejifunza kitu fulani hapa.....tunahitaji bank ambayo ipo flexible kiasi kwamba ukiwa na accunt kwao unajisikia huru na biashara yako...
 
Back
Top Bottom