Msaada; Je,Naweza kutumia bamia na supu ya makongoro kama dawa kwa viungo kuacha kulialia

Bacyclerbacy

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
1,744
3,019
Habari zenu wakuu
Naimani hapa wengi mmenizidi umri (shikamoon)

Me ni binti (24)Nina tatizo la kuumwa na viungo kama
Viungo vya mikono
Miguu
Kiuno
Mgongo
Yapata miez kama miez minne sasa

Lkn wiki moja iliyopita naona magoti yameanza kuuma saana na nikichuchumaa ndo yanazidi
nimejaribu kuyachua na kunywa dawa as kupunguza maumivu naona angalau yamepungua bali kuna milio milio tu ya Mara kwa mara kwenye magoti,kiuno na mikono

Ila nimeambiwa na mtu ambaye sio Dr kwamba nile saana bamia na supu ya makongoro
Japo mm na bamia ni babamkwe

Je wakuu kuna ukweli wowote kuhusu hayo mabamia katika kusaidia viungo?
Ahsanten.
 
Mm nliambiwa niwe nakunywa juice ya bamia kuna wakati sukari yangu ilikuwa inapanda....sasa imagine unazikata bamia unaziloweka kwny maji mpk asbh halaf unakunywa yale maji yake.
Uuuuuuuwiiiii jamn mm
 
Mm nliambiwa niwe nakunywa juice ya bamia kuna wakati sukari yangu ilikuwa inapanda....sasa imagine unazikata bamia unaziloweka kwny maji mpk asbh halaf unakunywa yale maji yake.
Hiyo ndo dawa yake. Bamia ina saidia kulainisha sehemu zanye joint so ukinywa itakusaidia kwa kiasi flan japo nashauri umuone daktareeeee
 
Back
Top Bottom