Msaada jamani namna ya kukata rufaa

Wa kusoma

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,454
2,975
Ndugu zangu wanasheria naombeni msaada.
Wote mnajua kwamba kesi nyingi za jinai hupelekwa mahakamani na polisi na hivyo wakati kesi inaendeshwa wewe mwenye kesi unakuwa kama shahidi wa jamhuri dhidi ya mtuhumiwa.

Msaada wangu ni kwamba kuna wizi wa mali ulitokea nyumbani kwani nikamkamata mwizi na kumpeleka polisi. Polisi walifanya kazi yao ya upelelezi na mwisho wa siku jamaa alifikishwa mahakamani. Mimi niliitwa kama shahidi na kuthibitisha kama kweli mali iliibiwa kwangu. Kesi imeenda lkn mwisho wa siku jamaa ameshinda kesi na sasa yuko mtaani.
Nachotaka kujua ni kwamba mm nataka kukata rufaa au niombe kesi isikilizwe upya sasa sijui sheria hapa inasemaje maana kwenye kesi ile mm nilikuwa shahidi mlalamikajia alikuwa jamhuri sasa je mm naruhusiwa kukata rufaa au mpaka polisi?
 
Huruhusiwi kukata rufaa maana wewe hukuwa mmoja wa party wa kesi bali ni shahidi tu! Pia kesi haiwezi kurudiwa, otherwise mshtakiwa atakuwa na defense nzuri na atashinda tena.
Cha kufanya: Jaribu kuongea na Polisi ili uwashawishi wakate rufaa, pia zingatia usiwe nje ya muda wa kukata rufaa!
 
Asante kwa ushauri wako, hukumu ilitolewa April 21 vp muda si bado upo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom