Msaada jamani mradi unaangamia

wiseboy

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
2,931
3,299
HELLOW G.T...Jamani nilikuwa nimefanikiwa kununua tetea 80 na jogoo 8, lengo langu ilikuwa kununua tetea 150 wa kuku wa kienyeji, na hao kuku nilikuwa nshawapa chanjo ya mdondo (new castle) ila katika khali ya kuendelea kuongeza matetea nilinunua tetea wawili kama wiki mbili nyuma, hawa tetea mmojawapo alipofika tu akaanza kuharisha mharo mweupe nikampa antibiotic, hakupata nafuu na akaanza kukoroma yaani kupumuwa kwa shida ilibidi nimchome pen strep, hakupata nafuu akafa, yule mwenzake naye akakaa kama wiki nae akafa......nikawafukia, sasa ajabu wakafuatia vifaranga wakubwa wakubwa nikaamuka asubuhi na kukuta wamekufa 15 gafla, 20 wakaonyesha dalili zile za kuku mgonjwa na wakafa, sasa kwa kuku wakubwa 15 wako crius wanakoroma, wanaharisha mharo mweupe na wamezubaa, sasa naomba kuuliza nitumie dawa gani hapa? je ni kideri? je ile chanjo haikufanya kazi japo nimechanja mara 2....... nasikitika nitapoteza utitiri wa kuku wangu.
 
Pole sana kuku wanachangamoto zao, mie sio mtaalamu wa mifugo ila nimeona hizi dalili kuwa ni Kuharisha Kinyesi Cheupe (Bacillary White Diarrhea) dalili zake zinafanana na hizo, nimekuwekea attachment uisome
ushauri wangu: epuka kuchanganya kuku kutoka kwa wafugaji wengine bila kuwaangalia kwa muda kwanza kama wana dalili za magonjwa. wish you all the best, usikate tamaa

 

Attachments

  • 17-04-2012-keepers.pdf
    932.3 KB · Views: 174
Pole sana Ndg, natamani sana ningekuwa na uzoefu na ufugaji nikushauri maana inauma sana unapoona malengo yako yakipotea hivihivi. Ila nikutie moyo kwa mambo machache.

1. Changamoto za ujasiriamali ni nyingi. Kikubwa hapo ni kuchukua somo ni wapi ulipokosea ili usirudie tena kwa kipindi kingine. Ndivyo wajasiriamali tunavyosonga mbele. Unaweza ukaanguka mara nyingi tu ila hatukati tamaa, tunajifunza kila shemu iliyotufanya tukajikwaa na kuanguka na tukishafahamu safari inasonga mbele kwa ushindi.

2. Chukua somo; Kwa mfano, hapo inawezekana kuku wageni uliowaleta walikuwa wagonjwa. Ni vyema ukawa na mabanda mawili. Moja ukatunzia kuku ambao unajua umeshawapa chanjo na ni wazima. Banda lingine ukatunzia kuku wageni ambao hujui kama ni wazima au siyo wazima. Ukisha waangalia kwa muda ikiwa ni pamoja na kuwapa chanjo na kujiridhisha kuwa ni wazima ukawachanganya na kuku wengine uliokuwa nao

3. Pia banda la pili unaweza ukatunzia kuku wote ambao una wasiwasi kuwa ni wagonjwa badala ya kuwaacha na wengine wazima wakaendelea kuambukiza wengine.

4. Mwisho: Nakushauri umwone daktari wa mifugo aliye karibu, au wauzaji wa madawa ya mifugo wanaweza wakakushauri utumie dawa ipi kuokoa mradi wako wa kuku.

Usikate tamaa mbele ni kuzuri zaidi ya hapo ulipo.
 
Pole sana mdau...Jifunze kutokana na makosa...inawezekana hii ikawa ni moja ya mara nyingi ya kuanguka lakini kamwe usikate tamaa...rekebisha makosa then songambele...mimi hapa nilipo nimeshayaona mengi sana kama hayo katika maisha yangu ya ujasiriamali....mpaka sasa nimekuwa sugu...na siogopi kupambana kwenda mbele!!!!
 
thanks wadau wote kwa michango yenu, asanteni kwa kunitia moyo, sitakata tamaa kwani kuna sehemu nilisoma kwamba we are olways fail to meet our goals coz we are easily giving up, staa giv up for real
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom