Msaada: Hili jiwe la kawaida au ni aina ya madini?

Hilo jiwe linaitwa Obsidian. Halina thamani sana kama gem. Jaribu ku google hilo jina utapata details.
Usipende ku Google na kuamini kila jina ndio jiwe lenyewe kwanza unatakiwa kujua mawe yanafanana rangi aina nyingi kinachotakiwa ni kuangalia tabia ya jiwe na mpangilio wa nyama zake na lilipopatikana ni wapi hilo jina ulilotaja ukiulizwa yanapatikana wapi hutaweza kujibu najua utaenda ku Google lakini pia sio madini aina zote yanapatikana tanzania
 
Isije ikawa ni kipande cha mkaa umekigonga gonga vizuri kwel?

Maana juz kati kuna mtu kafa kwa mstuko siku ya mazishi yake.
 
Usipende ku Google na kuamini kila jina ndio jiwe lenyewe kwanza unatakiwa kujua mawe yanafanana rangi aina nyingi kinachotakiwa ni kuangalia tabia ya jiwe na mpangilio wa nyama zake na lilipopatikana ni wapi hilo jina ulilotaja ukiulizwa yanapatikana wapi hutaweza kujibu najua utaenda ku Google lakini pia sio madini aina zote yanapatikana tanzania
Sawa geologist.
 
Aaaah basi hapo hamna kitu
Kama ndio hili ulilonalo basi hii ni thamani yake sokoni

20210915_185812.jpg
 
Umeokota hapo Kariakoo, unategemea nini zaidi ya mabaki ya bidhaa ya mchina iliyoungua.
Nimeokota wakati mafundi wanachimba msingi, by the way usijibu kila kitu kuonyesha mjuaji au kutafuta sifa uonekane umechekesha
 
Nafikiri kiustaarabu hili sio jibu hata wewe unaweza kuuliza kitu au jambo lolote ambalo hulifahamu vizuri na ukajibiwa kistaarabu sio vema kumkejeli mtu anayetaka kujua jambo
Naomba nikusaidie maana haujaelewa, jambo la muhimu ulitakiwa utueleze ulikoliokota yaani mji, kijiji au pori la mkoa fulani, vinginevyo ngumu kupata jibu sahihi.
 
Nimeokota wakati mafundi wanachimba msingi, by the way usijibu kila kitu kuonyesha mjuaji au kutafuta sifa uonekane umechekesha
Nimekufafanulia vizuri sana, nikujulishe tu kuwa watu wanachoma chupa na huweza kufanana na almasi au madini mengine.
 
Nadhani ikijulikana limepatikana maeneo gani huenda ukapata mwanga zaidi kujua ni aina gani (ingawa na hio ina hatari sababu kama lina thamani unaweza kuambulia asante tu kwa mwenye mali kwa kumuokotea mali yake)

Neno kuokota lina ukakasi....
 
Back
Top Bottom