Msaada: Hii alama ya duara katika line yangu ya simu inamaanisha kitu gani?

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
37,338
2,000
Kama picha inavyojieleza hapo wakuu unaweza kuona hako kaalama ka duara katika hiyo line ya simu.Wajuzi wa masuala ya tech nijuzeni tafadhali hako ka alama kanamaanisha nini?

Kuna saa kanatokea halafu baada ya muda kanapotea.

635425721.png

1635425905.jpg
 

Lee

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
40,523
2,000
ngoja wataalam waje...au ndo mambo ya kuchunguzana (jokes )
 

MR MAJANGA

JF-Expert Member
Oct 4, 2014
2,349
2,000
Mkuu hiyo ni signal ya mtandao husika unapoweka line tu hiyo alama lazima itokee na isipotokea huwezi kupiga wala kupokea chochote, na kwenye hiyo signal huo ujazo upo nusu kutokana na nguvu ya mtandao kama kakijaa full basi mtandao upo vizuri lakini kakishuka basi mtandao unakuwa upo chini, ila kwenye kila simu kapo huwa vinatofautiana jinsi ya muonekano,

kwenye simu kama yangu kuna mistari imejipanga kuanzia mfupi hadi mrefu, mrefu ukiondoka na kubakia mifupi maana yake signal ni ndogo na ikitokea yote kuanzia mfupi hadi mrefu signal ipo vizuri
 

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
201,774
2,000
Hujaelewa swali mkuu. Anaongelea hio duara sio hizo signal. Hako ka doti
Mkuu hiyo ni signal ya mtandao husika unapoweka line tu hiyo alama lazima itokee na isipotokea huwezi kupiga wala kupokea chochote, na kwenye hiyo signal huo ujazo upo nusu kutokana na nguvu ya mtandao kama kakijaa full basi mtandao upo vizuri lakini kakishuka basi mtandao unakuwa upo chini, ila kwenye kila simu kapo huwa vinatofautiana jinsi ya muonekano, kwenye simu kama yangu kuna mistari imejipanga kuanzia mfupi hadi mrefu, mrefu ukiondoka na kubakia mifupi maana yake signal ni ndogo na ikitokea yote kuanzia mfupi hadi mrefu signal ipo vizuri
 

Champagnee

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
6,430
2,000
Hao wote juu wanakudanganya hio alama inamaanisha sim yako imeanza fikia mwisho wa matumizi kutokana na timeframe ya hio simu. Anza kuandaa bajet ya sim mpya taratibu
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
17,252
2,000
Jaribu kuweka hiyo line kwenye simu nyingine au weka line nyingine kwenye hiyo simu uone kitu gani kitatokea. Hiyo itasaidia kujua tatizo lipo kwenye line au ni simu.
 

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
26,760
2,000
Mara nyingi dot hutokea ikiwa status bar imejaa, sema hio yako imeunganika kabisa na network. Ukiwasha data pia inakuwepo?

Ni custom rom hio?
 

ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
12,897
2,000
Kama picha inavyojieleza hapo wakuu unaweza kuona hako kaalama ka duara katika hiyo line ya simu.Wajuzi wa masuala ya tech nijuzeni tafadhali hako ka alama kanamaanisha nini?

Kuna saa kanatokea halafu baada ya muda kanapotea.

View attachment 1989727
View attachment 1989726
Manake wazee wa kazi wamesha kuzuum bado mda mchache wakutie kibindoni..
Tupa simu tafuta chaka la kukimbilia Sudani huko ama Benin au Togo huko mbali mbali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom