Msaada: Hi hali ya kukaa muda mrefu bila kupata hedhi husababishwa na nini?

okiwira

JF-Expert Member
Jul 23, 2018
2,787
2,853
Hi hali ya kukaa muda mrefu bila kupata hedhi husababishwa na nini?

Yaani mfano mwanamke umezaa mtoto baadae unakuja pata hedhi baada ya miaka miwili ukizaa tena kuja kupata hedhi inakuchukua baada ya miaka au mwaka.

Hapa chanzo cha tatizo hili huwa ni nini?

Au ni jambo la kawaida kwa baadhi ya wanawake?
 
Hiyo ni kawaida sana hasa kama unanyonyesha

Kwahyo hilo sio tatizo usiogope
 
Wakati wa kunyonyesha hormone ya prolactin inakuwa juu sana hivyo kuzuia upevushaji wa mayai, ndiyo maana unakosa hedhi. Wengine huwanyonyesha watoto wao kwa muda mrefu na Mara kwa Mara kama njia ya uzazi wa mpango. ( sio Doctor nimejibu kutokana na uelewa, kama kutakuwa na hitilafu doctors watarekebisha)
 
  • Thanks
Reactions: PYD

Uko sahihi ni Lactation Amenorrhea. Hutumika kama njia ya uzazi wa mpango kwa uhakika kwa miezi sita ya mwanzo mara baada ya kujifungua. Baada ya hapo ni vyema ukatumia njia nyengine ya kupanga uzazi hata kama bado hujapata hedhi maana inakuwa sio njia ya kuaminika tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: PYD

Similar Discussions

Back
Top Bottom