Msaada (HESLB): Kuna mdogo wangu baba yake amefariki lakini anapata ugumu kupata cheti cha kifo

MWITA100

Senior Member
Jul 9, 2015
165
225
Habari,

Naomba msaada kwa mwenye ufahamu na hili, kuna dogo hana baba (amefariki) na cheti cha kifo kimekuwa na mzunguko mrefu, hadi muda huu bado hajakipata na siyo rahisi akipate hivi karbu kutokana na mambo ya urithi na mambo ya ukoo.

SWALI
Leo alikuwa anajaze form ya mkopo imefikia kipengele cha wazazi ameandika hana baba system ikaomba namba ya cheti cha kifo.

Je, afanye nini na system haiwezi kuruka nafasi, na ukizingatia hana baba kweli?

Msaada kwa mwenye ufahamu na hili asanteni.

NAWASILISHA.
 
-mseto_

Member
Jul 30, 2017
93
125
Nilifanyaga mistake hiyo kwa kuandika baba mlemavu, systeam ikadai barua, nilidata.

Haikutakiwa afanye hivo kabla ya kua na Cheti, hapo kilichobaki ni kukamia cheti kipatikane, hakuna kinachoshindikana tatizo inakuaga hela.
 
Kaudunde Kautwange

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
1,321
2,000
1. Cheti cha kifo hakina mahusiano na mambo ya urithi na ukoo.

2. Je, analo tangazo la kifo!?

3. Mwambie aende kwa msajiri wa vizazi na vifo wa wilaya, aongee naye atamsaidia

4. Mwisho kabisa, hapo mchawi pesa, ukiwa na pesa hata siku 3 hazimaliziki unakuwa umeshapata cheti
 
MWITA100

Senior Member
Jul 9, 2015
165
225
1. Cheti cha kifo hakina mahusiano na mambo ya urithi na ukoo.

2. Je, analo tangazo la kifo!?

3. Mwambie aende kwa msajiri wa vizazi na vifo wa wilaya, aongee naye atamsaidia

4. Mwisho kabisa, hapo mchawi pesa, ukiwa na pesa hata siku 3 hazimaliziki unakuwa umeshapata cheti
Uhusiano upo mkuu ni story ndefu but asante kwa ushauri
 
Arch.katunzi

JF-Expert Member
Sep 18, 2014
215
225
Nakupa muongozo wa ku process cheti cha hati ya kifo

Kupata hicho cheti inabidi familia ikae kikao na kuandaa muhtasari wa kikao kwa taratibu zifuatazo.

1.Waliohudhuria
Hapo wanaolodheshwa waliohudhuria kikao hicho,uhusiano wao na marehemu,wadhifa wao kwa marehemu mfano kama ni mke wa marehemu,ataandika mke,kama ni Mjomba wa marehemu ataandika Mjomba wa marehemu,kama ni mtoto wa marehemu ataandika mtoto wa marehemu

2.Wasiohudhuria
Kama wapo,na kama hawapo hakuna haja ya kipengele hiki.

3.Agenda
a.kufungua kikao
Kikao kilifunguliwa saa 10.00 na wajumbe wate kwa pamoja tumemchagua juma kasinde warioba kuwa mwenyekiti wa kikao na katibu wake ni shilingi hamsini mustafa.

b.kutambua Mali za marehemu
Marehemu hamisi juma ameacha nyumba tano,Viwanja vitatu na gari mbili.

c.kuteua msimamizi wa mirathi
Familia kwa pamoja tumemteua ndugu jamila hamisi juma kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu,hamisi juma.msimamizi wa mirathi ndiye atakaye process hicho cheti,hapa sasa ni vizuri akawa muhusika anaye kihitaji hicho cheti.

d.kutambua wategemezi wa marehemu
Kuorodhesha wategemezi wote wa marehemu.

e.kufunga kikao.
Kikao kilifungwa mnamo saa 12:30 jioni kwa dua fupi na kuwashukuru wanafamilia kwa kuhudhuria kikao hicho,na kuwaomba washirikiane kwa kila jambo.

Mwisho anasaini mwenyekiti na katibu wake.

Baada ya hapo,muhutasari huo utasainiwa na mwenyekiti wa mtaa au kijiji na afisa Mtendaji wa kata.

Utaambatanisha na kiapo cha hati ya kifo,kinatolewa mahakamani,kadi ya mpiga kura ya yule anaye process, pamoja na Vyeti vyake vya shule.Baada ya hapo atapeleka kwa msajiri wa vifo na vizazi wa rita wa wilaya.mala nyingi ofisi zao zipo ofisi ya mkuu wa wilaya na kulipia sh.10,000/=.
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,004

Huu ni ushauri kuntu kabisa. Mtu akifariki unatakiwa kupata uthibitisho wa kifo kwa maandishi kutoka hospitali/ doctor husika aliyethibitisha kifo. Hii karatasi ndio hutumika kwenda kuandikisha kifo (RITA) na kupata cheti cha kifo. Utaona hapa hakuna uhusiano na mirathi.

Mkuu ulicho eleza ni process ya mirathi na siyo ya kupata Cheti cha Kifo. Ni kweli hakuna mirathi kama cheti hicho hakipo.

Uhusiano upo mkuu ni story ndefu but asante kwa ushauri
Pitia hapo juu.
 
MWITA100

Senior Member
Jul 9, 2015
165
225
Huu ni ushauri kuntu kabisa. Mtu akifariki unatakiwa kupata uthibitisho wa kifo kwa maandishi kutoka hospitali/ doctor husika aliyethibitisha kifo. Hii karatasi ndio hutumika kwenda kuandikisha kifo (RITA) na kupata cheti cha kifo. Utaona hapa hakuna uhusiano na mirathi.

Mkuu ulicho eleza ni process ya mirathi na siyo ya kupata Cheti cha Kifo. Ni kweli hakuna mirathi kama cheti hicho hakipo.

Pitia hapo juu.
Asante mkuu
 
Hapo sijabuni wala kutoa kichwani,nilicho kieleza hapo juu ni utaratibu niliyo pewa na Rita wenyewe wakati nashughurikia Vyeti vya vifo vya wazazi kwa ajiri ya kuomba mkopo.Nilifanikiwa na Vyeti nipo navyo mkononi...!Wakati mwingine mnapo shauri tumieni experience na siyo mihemko...!
 
Arch.katunzi

JF-Expert Member
Sep 18, 2014
215
225
Nenda ofisi za Rita za wilaya upewe utaratibu wa kufata,maana ukikosea haupewi cheti...!Labda kama utapitia nyuma...!
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,004
2,000
Hapo sijabuni wala kutoa kichwani,nilicho kieleza hapo juu ni utaratibu niliyo pewa na Rita wenyewe wakati nashughurikia Vyeti vya vifo vya wazazi kwa ajiri ya kuomba mkopo.Nilifanikiwa na Vyeti nipo navyo mkononi...!Wakati mwingine mnapo shauri tumieni experience na siyo mihemko...!
Kuna walakini hapo. Cheti cha kuzaliwa unakipata ukipeleka notification of birth kutoka pale mtoto alipozaliwa. Cheti cha kifo unapeleka tu certification of death. Mwaka jana tulipita njia hiyo ya moja kwa moja na cheti kilipatikana.
Sioni issue ya mhemko inatoka wapi. Hapa tunaelekezana hivyo tuvumiliane hadi tufikie maelewano. Inawezekana kukawa na njia tofauti za kupita. Labda niulize kwenye mchakato wenu mlikuwa na certification of death/burial permit?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom