Mrekebishaji
Senior Member
- Mar 19, 2009
- 168
- 63
Wana jukwaa,
Naomba maelezo ya namna ya kuwa wakala wa M-PESA pamoja na uuzaji wa luku.
Ikiwezekana kama kuna mtu anayehusika moja kwa moja naomba kumuona. Nipo Dar es Salaam
Nilipata kuulizia M-pesa wao mtaji wa kufungua duka moja la M-PESA wanahitaji 1,000,000 (one million).
Unatakiwa uwe na TIN number, leseni ya biashara, fremu ya kuanzisha mradi, kitambulisho hata cha mpiga kura nadhani kinafaa.
Kwa biashara inalipa I can tell you, brother japo sijawahi kuifanya. Cha msingi uwe na mtaji imara na wateja wako wawe na uhakika kwamba wakati wowote wakija kwa kibanda chako kutaka kutuma au kutoa kiasi flani cha pesa basi watapata huduma hiyo.
Tatizo kubwa ni wengi wanakuwa na mitaji ya kuzuga ukishataka kutoa zaidi ya laki mbili anakwambia hamna network kumbe fedha hana.
Unaweza pamoja na biashara hiyo ukaunganisha na kusajili, kufanya replacement na kutengeneza special number, kuwa wakala wa EVD (kumbuka pia utakua unalipwa na makampuni ya simu commission)... So ukiwa una mix vibiashara vyote hivyo kwa mitandao yote hasa tigo voda na airtel mwisho wa mwezi unaweza kuwa unapiga faida hata 1,000,000 au zaidi.
Changamoto ya biashara hiyo ni wapita njia wa kutosha na ka mtaji kako kukatuliza, ikiwezekana kuukuza pia, ili kuyaongeza maduka yafikie angalau matatu...
TRY IT MKUU, I'M ENCOURAGING YOU
��
Transaction Agent commission model (ex VAT) From To Deposit commission Withdraw commission Total commission 1,000 9,999 200 300 500 10,000 19,999 200 400 600 20,000 49,999 300 400 700 50,000 99,999 400 600 1,000 100,000 199,999 600 800 1,400 200,000 299,999 800 1,300 2,100 300,000 399,999 1,000 1,800 2,800 400,000 500,000 1,000 2,500 3,500 Registration Tshs 500 once off
Hayo ndio mapato ya wakala anaye deposit na anaye withdraw. Hapo vodacom wameshatoa sehemu yao. Hii commission inakusanywa unalipwa kwenye simu yako ya head office kila mwisho wa mwezi. Kama upo chini ya wakala mkuu unakatwa 20% anapewa yeye.
wapalepale post
Heshima kwenu,
1. M PESA
2. Tigo pesa
3. Airtel money
4. CRDB fahari huduma
5. Kifaa cha max malipo kwa ajili ya luku etc
Jamani ndugu yenu nafikiria kuanzisha hii biashara ya u-wakala wa m-pesa. Mwenye details kidogo kuhusu hii biashara anijuza hasa nataka kufahamu kuhusu:
1. Kiwango cha chini cha mtaji unao hitajika
2. Jinsi faida inavyopatikana
3. Jinsi ya kujisajiri (hili nadhani sio issue sana naweza kwenda kwa voda wenyewe) itanirahisishia zaidi
Nawasilisha
================
Mimi ni wakala wa M-Pesa kitambo sana sijawahi tapeliwa,inalipa sana kama tu goli lako lipo sehemu yenye mchanyiko wa watu wengi na kama unaielewa vizuri biashara hiyo.Unahitaji kuwa na laini,TIN na eneo la kufanyia biashara
kumsajili mteja ni Tsh 500/- kamishen
mteja aliyesajiliwa akiweka pesa kwa mara ya kwanza unapata tsh 2000 kamisheni akituma pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh 300/- hadi tsh 5000/- inategemeana ametuma kiasi gani
akitoa pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh500/- hadi tsh 5000/- inategemeana katoa shilingi ngapi
akinunua airtime kwako unapata karibia 10% kamisheni ya airtime aliyonunua
akinunua Luku unapata kamisheni kadhaa
Biashara hii ili ufanikiwe zaidi unaweza kuichanganya na biashara nyingine kama kuuza luku, na vinywaji baridi kama soda na juisi ambavyo havihitaji mtaji mkubwa au kama una biashara yako tayari halafu ukaongezea hii biashara kama ziada
Yaani kwa kijana wa kitanzania wa kawaida akiwa serious inaweza akatolewa na biashara hii kwa ufupi ZAP,M-pesa na Tigo Pesa kama una magoli matatu au maanne kipato cha mwezi ni net 2m, yanini kuajiliwa sasa?
================
Faida yake inategemea yafuatayo:
Ufanisi wako (via Operator) wa kazi;
Kama service ni nzuri hasa in unavyowasikiliza na kuwashughulikia wateja, hii inahusisha mhudumu wako kua haraka na kujua huduma zote.
Mfano: mteja anaweza asijue jinsi ya kutumia akaunti yaM-pesa, hapo ina maana Mhudumu awe mpole amsaidie.
uwe na mtaji wa kutosha ili kuhakikisha mteja akija kutoa au kutuma pesa anapata
hii itasaidia kuptopoteza miamala kwa kukosa pesa na pia itamfanya mteja awe anaiamini sehemu yako hata siku nyingine kuja kwenye banda lako.
- Hakikisha jioni unafunga mahesabu pesa yako mkononi na kwenye laini. Kama jumla ilikuwa milioni mbili asubuhi jioni inatakiwa iwe hio hio milioni mbili
- Unapata pesa ya commission mwisho wa mwezi. Kama mtaji wako ni Million 5 kwa siku na inazunguka ipasavo na hio sehemu ina shughuli nyingi, kamisheni inaweza fikia hata milioni moja au zaidi
- Kama sehemu haina mzunguko wa pesa wa kutosha unaweza kupoteza muda wako, wateja wapo wa kutosha ni nadra kupata hasara. More inakua out of mistakes kama kutuma pesa mahala ambako sio husika kwa bahati mbaya.
- Unaweza ukatuma pesa kwa mtu mwingine ambaye sio mteja kwa bahati mbaya, japo pesa hii unaweza kupiga simu kwa vodacom halafu wakarudisha muhamala huo mara nyingine unaweza usiupate kama uliyemtumia atakuwa haraka kwenda kutoa
- Noti feki kama kuna wateja wanaweza wakakuletea mabunda ya pesa huku wakiwa wamechanganya na mabunda ya noti feki, kabalaya kuweka pesa kwenye droo yako hakikisha unaziangalia, kama unafanya hadi usiku nunua tube light ili kuwe na mwanga wa kutosha kugundua noti feki.
- Kuna vikwazo pia katika biashara hii, na kubwa likiwa ni suala zima la usalama kuna vibaka au majambazi wanaweza wakakutegea ukiwa unatoka wakakukaba, ni bora kuwa na sefu lako imara, kwenye fremu yako pia kunatakiwa kuwe na grili imara kuzunguka dirisha na mlango