Msaada haraka tafadhali kichwa kinanikosesha amani ya kuishi

silence noise

Member
Apr 23, 2017
54
29
Jamani naombeni ushauri. Nina umri wa miaka 33 kwa sasa na ni mwl sekondari. Ninasumbuliwa sana na kichwa na kimeanza muda mrefu. Kwa kumbukumbu zangu nahisi niliumia utotoni, kuna siku tulikuwa tunacheza nilianguka nikitanguliza kichwa chini na nakumbuka siku hio nililala siku nzima na sikukumbuka na kusema hospitalini. Nimesoma kwa shida sana na naamini nimefika hapa kwa uwezo wa Mungu tu. Maumivu mara nyingi yanahusisha kizunguzungu, makohozi yasiyoisha, vipunje vidogo vyenye harufu( nimegundua vinaitwa tonsil stones) sijui kama vina uhusiano na kichwa, na kibaya zaidi ni usahaulifu kupita kiasi. Mwaka 2008 nilienda kcmc lakini walinipima hawajagundua tatizo na wakati huo nilikuwa najiandaa kwenda chuo kikuu(udom)
Nilikwenda chuoni lakini nasikitika nilishindwa kuendelea na chuo baada ya tatizo kuzidi. Bahati nzuri chuo cha ualimu dakawa ndio kilikuwa kinaanzishwa na rafiki yangu aliyekuwa anajua tatizo langu akanishauri nikajaribu kuomba huko kwani kwa elimu ya diploma naweza kuvumilia na kumaliza tofauti na chuo kikuu. Namshukuru sna rafiki yangu kwani kweli nilifanikiwa kumaliza japo kwa shida sna. Nakosa amani ya maisha kwani hata kazi nafanya kwa shida sana hasa kutokana na maumivu na usahaulifu mambo yanayonifanya nikose kujiamini darasani. Tafadhali sn nisaidieni nifanyaje kwani natamani nianze kufuatilia matibabu tena. Nahisi naweza kupata matatizo zaidi nisipopata ufumbuzi.
 
Pole sana, M/Mungu atakujaalia InshaAllah utapona lakini jitahidi kutafuta matibabu hospital kubwa kujua tatizo zaidi usikae na ugonjwa kimazoea tafuta tiba yake as far as una Bima ya Afya kuna hospital utapata huduma nzuri kwa Bima yako
 
Pole sana, M/Mungu atakujaalia InshaAllah utapona lakini jitahidi kutafuta matibabu hospital kubwa kujua tatizo zaidi usikae na ugonjwa kimazoea tafuta tiba yake as far as una Bima ya Afya kuna hospital utapata huduma nzuri kwa Bima yako
Ahsante kwa ushauri wako, nina bima. Naomba unisaidie hosp. nzuri hasa ya private wanaopokea bima kwa sababu serikalini sipaamini. Shukrani sana
 
Ayssee!!*pole sn!, but kw kuwa ushauri ni bure?*Naomba nikupe namba za sim naamini Utasaidika na tatzo lako litakwisha
 
piga namba hizo,, 0754882210* usiogopi kufanya nae mazungumzo, baada ya salam "mueleze homa yako, naamini utapona na utakua imara kabisa,, pia mie alinisaidia sn,
 
Back
Top Bottom