Msaada haraka tafadhali kichwa kinanikosesha amani ya kuishi

Kuna jamaa nilisoma naye advanced level alikuwa na tatizo la kuumwa kichwa hadi misuli ya damu inaiona ilivyokaza.
Muhimbili aliambiwa ana Amoeba, akapewa dawa zikaisha hali ikawa vilevile, akaenda tena akapewa miwani ya macho ikamsaidia tu kufanya mtihani lakini hali haikubadilika sana.

Mwisho wa Siku akaenda hospital ya mission Peramiho huko Songea, akaambiwa mwili wake unazalisha damu kwa wingi hivyo anatakiwa kuitoa kila baada ya muda fulani. Hadi leo yupo fresh na familia yake huko mbeya, kikazi nadhani bado anaendelea na utaratibu wa kutoa damu.
 
Jamani naombeni ushauri. Nina umri wa miaka 33 kwa sasa na ni mwl sekondari. Ninasumbuliwa sana na kichwa na kimeanza muda mrefu. Kwa kumbukumbu zangu nahisi niliumia utotoni, kuna siku tulikuwa tunacheza nilianguka nikitanguliza kichwa chini na nakumbuka siku hio nililala siku nzima na sikukumbuka na kusema hospitalini. Nimesoma kwa shida sana na naamini nimefika hapa kwa uwezo wa Mungu tu. Maumivu mara nyingi yanahusisha kizunguzungu, makohozi yasiyoisha, vipunje vidogo vyenye harufu( nimegundua vinaitwa tonsil stones) sijui kama vina uhusiano na kichwa, na kibaya zaidi ni usahaulifu kupita kiasi. Mwaka 2008 nilienda kcmc lakini walinipima hawajagundua tatizo na wakati huo nilikuwa najiandaa kwenda chuo kikuu(udom)
Nilikwenda chuoni lakini nasikitika nilishindwa kuendelea na chuo baada ya tatizo kuzidi. Bahati nzuri chuo cha ualimu dakawa ndio kilikuwa kinaanzishwa na rafiki yangu aliyekuwa anajua tatizo langu akanishauri nikajaribu kuomba huko kwani kwa elimu ya diploma naweza kuvumilia na kumaliza tofauti na chuo kikuu. Namshukuru sna rafiki yangu kwani kweli nilifanikiwa kumaliza japo kwa shida sna. Nakosa amani ya maisha kwani hata kazi nafanya kwa shida sana hasa kutokana na maumivu na usahaulifu mambo yanayonifanya nikose kujiamini darasani. Tafadhali sn nisaidieni nifanyaje kwani natamani nianze kufuatilia matibabu tena. Nahisi naweza kupata matatizo zaidi nisipopata ufumbuzi.
DALILI ZA KISUKARI AU TB JE ULISHAKWENDA HOSPITALI NA UKAPTA VIPIMO NA JE VIPIMO GANI?
 
Ahsante kwa mawazo ndg. Nimepima vipimo vingi sna kcmc ct scan kikiwemo yaani mpaka kuna kipimo nilifuata Arusha ambacho hakikuwepo kcmc ila ni muda mrefu sasa. Yaani nilichoamini ni kuwa walipima vipimo vyote muhimu mpaka hiv hakuna walichogundua na ndio maana nilikata tamaa mpaka leo. Kinachonipa matumaini ni kumbukumbu ya kuanguka utotoni ambayo sikuwa nayo kabla na nahisi tatizo litakuwa shingoni karibu na kichwa. Nafanya taratibu za kwenda hosp kwa sasa.
 
Pole sana kwa tatizo lako..
Katika maelezo yako umesema unasahau sahau..je unasahau sahau kwa jinsi/namna gani?
Mfn. MTU akikwambia kitu baada ya muda unasahau mpaka kakumbushe? Au unasahau majina ya vitu ambavyo ni vya kawaida kabisa mfn..Pencil, daftari na nk.?

Kuhusu kuumwa na kichwa, Kuumwa kichwa si ugonjwa Bali ni dalili za ugonjwa fulani.

Cha muhimu nenda Hospital/Daktari tena na tena kwani kuna magonjwa mengine yamejificha yanahitaji uchungunzi wa hali ya juu..
Ahsante ndg yangu. Mfano mzuri ni majina ya wanafunzi, naweza kumbuka wachache sna na wakimaliza shule ndio kabisa, nikikutana nao ni bahati sna kuwakumbuka hasa majina. Pia nilisoma kwa shida mno, ilinibidi kufanya marudio kwa wingi sna. Kwa ufupi sina kumbukumbu nzuri kwa kila jambo kama mazungumzo, majina nk.
Kwa hiyo unaweza kuelewa jinsi gani kazi ya ualimu ilivyo changamoto kwangu.
 
Hivi kumbe kusema chuo kikuu (udom) na kusema mwalimu wa sekondari
Inawezq kuwa sehemu ya tiba
 
Jibu swali tu
Je hayo maelezo yanawezaje kuwa sehemu ya kutibiwaa
Kuwa mwelewa ndg, nimeeleza hayo ili muweze kujua ukubwa wa tatizo au kwa kiasi gani nimeshindwa kufanya mambo ya maana kutokana na tatizo. Wewe unahisi ni sifa kwangu kwenda udom na kushindwa kuendelea?
 
Jamani naombeni ushauri. Nina umri wa miaka 33 kwa sasa na ni mwl sekondari. Ninasumbuliwa sana na kichwa na kimeanza muda mrefu. Kwa kumbukumbu zangu nahisi niliumia utotoni, kuna siku tulikuwa tunacheza nilianguka nikitanguliza kichwa chini na nakumbuka siku hio nililala siku nzima na sikukumbuka na kusema hospitalini. Nimesoma kwa shida sana na naamini nimefika hapa kwa uwezo wa Mungu tu. Maumivu mara nyingi yanahusisha kizunguzungu, makohozi yasiyoisha, vipunje vidogo vyenye harufu( nimegundua vinaitwa tonsil stones) sijui kama vina uhusiano na kichwa, na kibaya zaidi ni usahaulifu kupita kiasi. Mwaka 2008 nilienda kcmc lakini walinipima hawajagundua tatizo na wakati huo nilikuwa najiandaa kwenda chuo kikuu(udom)
Nilikwenda chuoni lakini nasikitika nilishindwa kuendelea na chuo baada ya tatizo kuzidi. Bahati nzuri chuo cha ualimu dakawa ndio kilikuwa kinaanzishwa na rafiki yangu aliyekuwa anajua tatizo langu akanishauri nikajaribu kuomba huko kwani kwa elimu ya diploma naweza kuvumilia na kumaliza tofauti na chuo kikuu. Namshukuru sna rafiki yangu kwani kweli nilifanikiwa kumaliza japo kwa shida sna. Nakosa amani ya maisha kwani hata kazi nafanya kwa shida sana hasa kutokana na maumivu na usahaulifu mambo yanayonifanya nikose kujiamini darasani. Tafadhali sn nisaidieni nifanyaje kwani natamani nianze kufuatilia matibabu tena. Nahisi naweza kupata matatizo zaidi nisipopata ufumbuzi.

intelig-old.png

Nenda Hindu Mandal kama uko Dar, mtafute Dr. Vishal au Dr. Ndosi. Nitakupa no. ya Dr. Vishal

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
 
Ahsante kwa mawazo ndg. Nimepima vipimo vingi sna kcmc ct scan kikiwemo yaani mpaka kuna kipimo nilifuata Arusha ambacho hakikuwepo kcmc ila ni muda mrefu sasa. Yaani nilichoamini ni kuwa walipima vipimo vyote muhimu mpaka hiv hakuna walichogundua na ndio maana nilikata tamaa mpaka leo. Kinachonipa matumaini ni kumbukumbu ya kuanguka utotoni ambayo sikuwa nayo kabla na nahisi tatizo litakuwa shingoni karibu na kichwa. Nafanya taratibu za kwenda hosp kwa sasa.
HUJAPATA VIPIMO VYA KIFUA KIKUU NENDA HOSPITALI YA SERIKALI KITENGO CHA KIFUA KIKUU UONANE NA DAKTARI MAALUM WA KIFUA KIKUU HALAFU MAJIBU UTAKAYO PATA LETE MREJESHO TUKUSHAURI MKUU
 
Asante kwa ushauri mkuu

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
Nenda Hindu Mandal kama uko Dar, mtafute Dr. Vishal au Dr. Ndosi. Nitakupa no. ya Dr. Vishal

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
Asante ndg. Nisaidie

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
HUJAPATA VIPIMO VYA KIFUA KIKUU NENDA HOSPITALI YA SERIKALI KITENGO CHA KIFUA KIKUU UONANE NA DAKTARI MAALUM WA KIFUA KIKUU HALAFU MAJIBU UTAKAYO PATA LETE MREJESHO TUKUSHAURI MKUU
Sawa mkuu

Back
Top Bottom