Msaada: Gharama za nyumba ya vyumba viwili

music mimi

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
441
758
Nataka kujenga nyumba ya vyumba viwili vya kulala, sebule, public toilet/bafu, jiko dogo, katika hivyo vyumba viwili kimoja kiwe na choo/bafu ndani.

Kiwanja tayari ninacho 20 *20. Ninaplan kujenga nyumba ya kuanzia maisha maana kwa usawa huu nimeona nikikimbilia kujenga nyumba kubwa haitoisha na nitaendelea kupanga kwa muda mrefu. Nikishaamia kwenye nyumba yangu ndio nitaanza kujenga nyumba kubwa maana naamini uwanja utabaki wa kutosha.

Msaada wa makadirio jamani, naamini kuna watu wanauzoefu na ujenzi humu.
 
Ili kukadiria gharama ya nyumba kwa ujumla kuna mambo mengi sana ya kuzingatia ambayo hayapo wazi sana kwenye post yako. Kwa mfano, sawa, site unayo lakini je ipo wapi (mkoa/wilaya)? - bei ya cement na building materials nyinginezo (eg matofali, mbao etc.) na hata labour charges zinaweza kutofautiana sana kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Na hivyo vyumba, sawa ni vichache, lakini unataka vya ukubwa gani (unataka kuweka nini na nini)? - chumba cha kulala kinaweza kuwa na square mita za mraba kuanzia 9 na kuendelea, sebule labda 16-20 sq.m, choo kama 4 - 6 sq m, jiko nalo 6-10 sq.m. So roughly unaweza kuwa unahitaji angalau 80 sq.m. Ujenzi wa kawaida kabisa unaweza kufikia sh 400,000/sq m ambayo inakupa gharama ya kama milioni 32 hivi. Kama nilivyosema mwanzo, unaweza kukaa na mtaalamu wa ujenzi ili akudodose vizuri na kuweza kukushauri gharama ambayo itakuwa real zaidi.

Kuna "maakitekcha" wengi tu humu ndani!:D:D:D
 
  • Thanks
Reactions: sab
Nataka kujenga nyumba ya vyumba viwili vya kulala, sebule, public toilet/bafu, jiko dogo, katika hivyo vyumba viwili kimoja kiwe na choo/bafu ndani.

Kiwanja tayari ninacho 20 *20. Ninaplan kujenga nyumba ya kuanzia maisha maana kwa usawa huu nimeona nikikimbilia kujenga nyumba kubwa haitoisha na nitaendelea kupanga kwa muda mrefu. Nikishaamia kwenye nyumba yangu ndio nitaanza kujenga nyumba kubwa maana naamini uwanja utabaki wa kutosha.

Msaada wa makadirio jamani, naamini kuna watu wanauzoefu na ujenzi humu.
Wacha tukujibu kama unavyotaka wewe, ili uweze kuamia kabisaa tenga milioni 20
 
milion 10 tu unaamia nyumba ya vyumba viwili kama una kiwanja tayari
Kujenga pagale na kuhamia,hiyo m10 yako inatosha. Lakini kwenda nayo sambamba hadi finish nyumba ya vyumba viwili na sebule pamoja na accessories zake zote alizotaja, kwa mikoa mingi haipungui m30 na kuendelea.
Tena kwa usimizi wako mwenyewe wa kiuchungu na maisha.
 
Milioni 10 inatosha sana... Kupandisha ukuta haifiki million 4 mpaka kwenye lenta.. Milango, bati, kupaua etc tiles, gypsum.. Ndio hiyo million 10.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom