Msaada gari ipi nzuri kati ya subaru Forester xt Outlander na Nissan Dualis

Hapo hakuna gari hata moja ya mtu wa kipato cha kawaida.Hapo gharama za services kwa magari yote uliyotaja zipo juu.

Kama wewe ni mpole,una kipato cha kawaida na hutaki makelele na watu go for RAV4 kisha utarudi hapa kunishukuru bila shuruti.
Usharudi hui ni nzuri Sana lakini akumbuke haya na kabla ya kununua
1.nissani ni gari nzuri lakini utakapokuja kuuza kupata mteja shida Sana tofauti na Toyota
2.ghalama za uendeshaji ni kubwa kama service pamoja na vipuli
3.kupata mafundi wazuri lazima wawe na ghalama kubwa kama zile geleji za kichina
Mwisho ukiwa nalo utakufa nalo ni ndoa ya kiroma kila hakuna padri ,kateksta,wala askofu WA kuivunja
 
Unaongea kama hawa wanaoitwaga walengaji japo ni kweli gharama za nissan zipo juu. Ila Kama unamiliki Toyota na unaipenda gharama zake zipo juu pia. Vifaa halisi vya toyota ni gharama.
 
Usharudi hui ni nzuri Sana lakini akumbuke haya na kabla ya kununua
1.nissani ni gari nzuri lakini utakapokuja kuuza kupata mteja shida Sana tofauti na Toyota
Ubora wa Nissan ni upi mkuu kwa sababu mimi naipenda sana ile shepu ya Duals?
2.ghalama za uendeshaji ni kubwa kama service pamoja na vipuli
Hivi mkuu gharama za vipuri vya Nissan ni kama mara ngapi hivi ya gharama za vipuri vya Toyota?
3.kupata mafundi wazuri lazima wawe na ghalama kubwa kama zile geleji za kichina
Mwisho ukiwa nalo utakufa nalo ni ndoa ya kiroma kila hakuna padri ,kateksta,wala askofu WA kuivunja
Gari za Nissan zinadumu kuliko gari za Toyota?
 
Kuna wakati atataka kuuza kununua nyingine kupata wateja ni shida ww huoni dualis zilikuja Kasi saizi nyingi zimepaki
Nitakupa jibu refu kidogo:

Anayewaza kuuza gari wakati wa kununua ni mlengaji.

Gari ni jambo binafsi sana, ukinunua unatengeneza attachment nalo, mpaka uje kuliuza limeshakupa huduma uliyokuwa unahitaji na kulitoa unalitoa kwa uchungu.

Gari lihudumie vizuri kiasi kwamba wanaokuzunguka walitake bila promotion.

Usinunue gari bovu, nunua jipya au used abroad with low km kisha toa huduma takatifu kwa kipindi chote cha maisha yenu.

Kuna wakati wanaokuzunguka wataanza kukusihi uwauzie kabla hata hujatangaza kuuza. Na bado kwa attachment uliyo nayo na gari lako utakuwa mzito maana kama ulilitunza unajua thamani yake.

Nimeshawahi kukutana na Nissan namba A dashboard inasoma km 600000. Na unakuta mtu ana service book. Historia yote ya service na parts replacement ipo kwenye kitabu. Unasoma kama hadithi tangu imenunuliwa mpaka ilipofika hapo ilipo.

Kuna mzee huko Arusha anatoka Asia nadhani, ana Suzuki vitara ambayo alinunua kipindi zimeanza ingia nchini, miaka hiyo. Hiyo gari ukiiona na historia yake na km zake ukiambiwa toa m10 nikupe kama unajua gari unatoa hapo hapo.

Huko Moshi kuna mzee ana benz tangu tupo watoto wadogo leo yeye sidhani kama anaona hata kuona ila benz ni mpyaaaa.

Vijana wa leo unaenda kununua gari unajiuliza siku ya kuuza itakuaje? Kwani unaanzisha biashara ya kuuza gari? Ukinunua na kuuza mambo mengine ya kimaendeleo utafanya sa ngapi? Si utakuwa kazi ni kukimbizana na ununuzi wa gari tu?

Kwa mazingira yetu maamuzi ya kununua gari, ukae nalo miaka m3 sijui uuze, ununue tena ukae miaka m4 uuze ni maamuzi yenye usumbufu wa muda na uchumi wako. Nunua gari, jipe 10 years za kufanya maendeleo mengine unless unasafiri sana na gari linachoka mapema.

Wenzetu wanabanwa na sheria kuendesha gari za zamani au km nyingi, na hii ni kibiashara zaidi sababu usiponunua jipya nani ataendesha mapya? otherwise kuna watu nje wangetunza magari yao na kufanya maintainance kubwa ili yadumu yaendelee kuwahudumia mpaka pale litakapohitajika kuzikwa kwa kufanyiwa recycling, kuyeyushwa na kutengeneza gari jipya.
 
Uamuzi ni wako..
Screenshot_20210806-211857_Instagram.jpg
 
Kuna mahali niliona Mad Max anadai Dualis ni gari ya kike. Sijui kwanini
🤣🤣🤣 Gari pendwa sana Tanzania ilo. Nadhani inaweza kuja kua ya pili after IST.

Ila watakuja diehard fans wa Yota watasema Nissan spare mpaka Kenya vijijini au Dubai.

Ila naona kama aka2030 ameweka options ambazo haziendani kabisa.

Subaru Forester XT​

Ni ya Kibabe, kwa boy racers na wanaopenda magari deeply sio tu wanaotaka gari likutoe Ubungo hadi Kigamboni.​

Outlander​

Ili nalo la kibabe sana.​

Nissan Dualis​

Hii nadhani ni family car. Daily drive ya kazini, home, kanisani, bata kidogo.

Kwa kipato cha kawaida, bora adake Dualis maisha yaendelee tu.
 
Back
Top Bottom