Msaada-fidia ya kupata ugonjwa unaohusiana na kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada-fidia ya kupata ugonjwa unaohusiana na kazi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by moto2012, Aug 18, 2012.

 1. moto2012

  moto2012 JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 2,092
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  Dada yangu ni fundi sanifu maabara (Lab. technician) katika hospitali ya Wilaya X, miezi sita iliyopita aligundulika kuwa na TB, alitibiwa na kupona, baada ya hapo alichukua hatua ya kudai fidia ya kupata ugonjwa akiwa kazini. Alipomwandikia barua Mkuu wake kutaka fidia, alijibiwa kwa kuwa anaishi na VVU hawezi kulipwa fidia. Wadau naomba nisaidieni (hasa wajuzi wa occupational health na occupational laws), je ni kweli dada yangu hastahili fidia? Na kama ndio huo sio unyanyapaa?
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,576
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Kama dada yako anaishi na VVU inawezekana TB yake haitokani na kazi yake bali ni ugonjwa nyemelezi kwa sababu immunity system yake ni dhaifu. Mtu anapata fidia kama madhara aliyopata yana uhusiano wa moja kwa moja kuwa yametokana na kazi anayofanya.
   
 3. l

  lusuadam Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama mdau alivyozungumza hapo juu, TB na HIV ni mtu na binamu yake. TB humtokea mtu pale kinga ya mwili inapokuwa imepungua. maana yake ni kuwa katika mazingira yetu haya, wengi wetu tunatembea ama tunaishi na vimelea vya TB, ila kwa kuwa kinga zetu zipo juu, tunafaidika kutopata ugonjwa huu. pale kinga ya mwili inapopungua, ndipo ugonjwa huu unajitokeza. Katika stages za WHO kuhusu watu wanaoishi na HIV/AIDS, mtu akipata TB anaonesha kuwa yuppo katika stage ya 3 ya kuishi na virusi.

  Kwa hiyo ndugu yangu, hapo hakuna fidia. atumie dawa kama alivyoagizwa na daktari, hadi miezi hiyo yote iishe. Mungu atambariki
   
Loading...