Msaada: Domain ya website yangu inauzwa, nifanyeje

Deejay nasmile

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
5,759
5,287
Wakuu mwaka 2011-2013 nilikuwa na blog website kubwa sana,ambayo ilipata watembeleaji wengi sana kila siku
Ilikuwa inahusu marafiki/wachumba
Muziki,habari,udaku na vichekesho..

Kiukweli hata kwenye search ingine ikikuwa katika top results

Sasa nikanunua domain.name kupitia maddogs domain kwa miak 2 hivi

Baada ya hapo sikuilipia tena kutokana na ubize na changamoto mbalimbali

Juz nikapata wazo niirenew tena
Dah nakuta inauzwa tena mil 6 na ushee hivi..

Na wamebadilisha mpaka umiliki (ukienda kuangalia pale kwenye WHOIS)

Sasa bahati mbaya details za akaunti yangu ya maddog domains inanigomea(nahisi kama imefutwa hivi)
Je nafanyaje kuigomboa kwani ni mimi ndio nimeifanya kuwa juu hivyo coz ni muasisi wake...

Na je ikiuzwa na mimi nitaambulia chochote? Tangu nimeacha kuilipia mimi haijawahi kutumika na mwingine tena..

Naombeni ushauri..nafanyaje

Blog yangu ni nasmiletz.blogspot.com

Na domain niliyoilink nayo ni www.nasmiletz.com

Kwa wale wadau wa 2012 -2013 mtakuwa mnaikumbuka kwani baadhi ya habari zake nilikuwa nazishea humu.. au hata ukienda google utaona jinsi ilivyo famous
 
Huna chako tena hapo.

Taka care, next time.

Domains nzuri ni assets, hazitelekezwi ovyo.

Premium domains zinauzwa mamilioni na ni biashara kubwa.

Domains ni kama ilivyo frequency za radio hapa Dar, kina Kusaga wamechukua frequency nzuri nzuri wamekaa nazo. Hata 88.9 ya Wasafi fm ni yake.
 
Daah yaan najilaumu sana
 
Bora wewe uliitelekeza, mimi Busati.com wale Godaddy walinipiga Fine kubwa na sasa wanaiuza milioni 30..

Kifupi makampuni mengi ya domain ni matapeli matapeli, ukijichanganya kidogo wanakupokonya domain.

Natumia name cheap sasa hivi, so far so good.
 
Ndo basi tena imekula kwako. Navyojuaga domain name ikiisha huwa unapewa siku kama 30 hivi za kuikomboa, zikipita nazo imekula kwako mazima.
 
Bora wewe uliitelekeza, mimi Busati.com wale Godaddy walinipiga Fine kubwa na sasa wanaiuza milioni 30..

Kifupi makampuni mengi ya domain ni matapeli matapeli, ukijichanganya kidogo wanakupokonya domain.

Natumia name cheap sasa hivi, so far so good.
Godaddy wanafanya mpaka brokering. Kama unahitaji Domain fulani na ikaonekana ina mtu na unaitaka, wanawasiliana naye kama anauza.

Ukichelewa kuinunua tu inaingia kwenye mfumo wa Bids na siyo free domain tena.

Ni wahuni sana Godaddy.
 
Bora wewe uliitelekeza, mimi Busati.com wale Godaddy walinipiga Fine kubwa na sasa wanaiuza milioni 30..

Kifupi makampuni mengi ya domain ni matapeli matapeli, ukijichanganya kidogo wanakupokonya domain.

Natumia name cheap sasa hivi, so far so good.
Kama hautojali nipe link ya blog yako/zako niwe natembelea huko.
 
Naombeni ushauri, ukitaka ununue domain na kuiweka kuwa hosted website yako ni jukumu lao pia?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom