Msaada: Desktop haioneshi chochote kwenye monitor nikiwasha, baada ya muda feni inazunguka sana

Shin Lim

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
7,004
12,473
Habari waungwana!
Kuna muda nilikuwa nafanya kazi then umeme ukakatika.
Baada ya umeme kurudi nilipojaribu kuwasha, monitor ikawa haioneshi chochote. Baada ya ya karibu dakika moja hivi, feni ikaanza kuzunguka kwa kasi sana. Hilo tatizo lilijirudia kila nilipojaribu kuwasha.
Je, tatizo ni nini waungwana?
 
Hakuna beep yoyote ile. Kuna muda kilikuwa kinatokea kimwanga chekundu ila sasa hivi kinatoke kile kimwanga cha kawaida.
Kama upo comfortable ifungue isafishe, toa cooler Eka thermal paste kama unayo, rudisha cooler ibane vizuri, Hakikisha waya wa feni umechomekwa vizuri, etc...

Huwa desktop zinasema tatizo lake kupitia beep ama huo mwanga ungeweza kusoma ingekuwa rahisi zaidi,

Niliwahi pata tatizo kama hili la feni kuzunguka kwa kasi sana full speed Sababu sensor ya mobo ilikua ambayo hucontrol feni kutokana na Joto la cpu.
 
Habari waungwana!
Kuna muda nilikuwa nafanya kazi then umeme ukakatika.
Baada ya umeme kurudi nilipojaribu kuwasha, monitor ikawa haioneshi chochote. Baada ya ya karibu dakika moja hivi, feni ikaanza kuzunguka kwa kasi sana. Hilo tatizo lilijirudia kila nilipojaribu kuwasha.
Je, tatizo ni nini waungwana?

Fungua hiyo CPU piga picha ya motherboard, especially kwenye capacitors kama kuna ambayo imevimba.
 
Nashukuru nimeifungua ingawa nilikuwa sijawahi kuifungua.
Nimefungua feni nimesafisha na kurudishia, nimechomoa hizi sijui ndio RAM au Hard disk (zinakuwa 2 zenye urefu sawa kwenye slot 4 nyeupe na nyeusi) nimesafisha na
kurudishia na sasa imewaka.
Nawashukuru sana kwa mchango wenu.
 
Back
Top Bottom