Msaada dawa ya kuua magugu

Bee hive

Senior Member
Feb 22, 2012
146
54
Wana jf kwa yeyote mwenye uelewa kuhusu dawa ya kupulizia shambani kuua magugu naomba anijuze. Ni dawa aina gani inafaa kutumika (kwenye shamba linalotarajiwa kupandwa legumes), kiwango cha uchanganyaji na maji ni kiasi gani na inapatikana wapi, nipo Arusha.
Natanguliza shukurani kwa msaada ntakao upata.
 
Nunua round Up! hiyo spelling zake sina uhakika, kijana wangu shambani yalikuwa yanamsumbua sana hayo madude, kupiga hiyo inakuwa kitu na boksi. ila ninavyosikia baada ya kupiga iyo inabidi muda upite kabla hujapanda kitu. muda gani!??! ongea na wataalamu kwenye maduka ya kilimo na huko ndipo utapata hiyo dawa.
 
ni magugu ya aina gani?kila gugu lina dawa yake,jua ya kuwa ukinunua dawa vibaya itaua ata hicho upandacho.taja jina na magugu usaidiwe
 
Katika eneo hili haya magugu wenyeji wanayaita sangari, bahati mbaya scientific name or common (english) name yake sihifahamu kwa sasa.
 
Mimi nafanya kazi kuwa train wakulima kuhusu herbicides, kama unataka kuuwa magugu yoote kabla ya kupanda mbegu zako basi waweza kutumia trade name yoyote yenye kiambata amalifu cha glyphosate. Na ya palizi ni chache sana ikitegemeana na zao
 
Round - up, kalach, triphosate- zote hizi ni trade names- active ingredients ni gyphosate ambayo ni non selective herbicide
 
Back
Top Bottom