Mfahamu mdudu kunguni (bedbugs) na jinsi ya kumuangamiza

Hao wadudu kiukweli wanazuilika na hata kama utafanya fumigation kama hutobadili mfumo wa maisha lazima watarudi tu kwani chawa, kunguni, mende na buibui upatikanaji wao kwenye nyumba kama sio uchafu basi nyumba inakuwa ina makorokoro mengi. Dawa hapa ni kujifunza kununua vitu kutokana na uwezo wa nyumba unayoishi maana nyumba zetu wakati mwingine unakuta mpaka kiroba cha unga na mchele kinakuwa uvunguni mwa kitanda na vingine vinakuwepo master b/room.

Piga ukuta rangi inayoonekana na epuka mavitu mengi ndani ya nyumba hutoona mdudu yoyote ndani ya nyumba maana na wao wana akili kama sie wanajua wapi pa kukaa, mfano mzuri kama nyumba ina tiles au rangi alafu chini umepiga skating (spelling problem) rangi nyeusi chini mtu akideki tu utaona kuna vijidudu vimejificha kwenye rangi nyeusi which means wanajua pale huwezi kuwaona

una akili japo hujanizidi mimi
 
Chanzo cha Kunguni ni vumbi na uchafu. Kupambana na Kunguni cha kwanza ni kuwa wasafi. Kama sakafu na kuta za hiyo nyumba ni za vumbi,wekeni cement kwenye sakafu na plasta ya kwenye kuta za nyumba yenu. Kisha mfanye furmigation. Watakwisha wote.
 
Duh! this is the highest level of superstition belief i have ever seen, yani ukiona mjusi ni roho zinaandama mtu! Umetisha aisee, unajuaje kama hawa watu wachafu? Come on, em don't be too superstitious unless una uzoefu wa kujigeuza mjusi au sisimizi..

na wala huwez kunielwa mnake mambo ya rohoni yajulikana sana kwa namna ya rohoni
 
Fumigation haimalizi kunguni...dawa ya kunguni ni maji ya moto. Chemsha maji ya moto yawe moto sana halafu umwagie ktk kitanda. Ni vizuri ukifungue kadiri inavyowezekana na uanike matandiko nje ktk jua kwa mda..wataisha!
 
We ndio umenena!
Hao wadudu kiukweli wanazuilika na hata kama utafanya fumigation kama hutobadili mfumo wa maisha lazima watarudi tu kwani chawa, kunguni, mende na buibui upatikanaji wao kwenye nyumba kama sio uchafu basi nyumba inakuwa ina makorokoro mengi. Dawa hapa ni kujifunza kununua vitu kutokana na uwezo wa nyumba unayoishi maana nyumba zetu wakati mwingine unakuta mpaka kiroba cha unga na mchele kinakuwa uvunguni mwa kitanda na vingine vinakuwepo master b/room.

Piga ukuta rangi inayoonekana na epuka mavitu mengi ndani ya nyumba hutoona mdudu yoyote ndani ya nyumba maana na wao wana akili kama sie wanajua wapi pa kukaa, mfano mzuri kama nyumba ina tiles au rangi alafu chini umepiga skating (spelling problem) rangi nyeusi chini mtu akideki tu utaona kuna vijidudu vimejificha kwenye rangi nyeusi which means wanajua pale huwezi kuwaona
 
wadudu wowote ndani mwako wakizidi hadi kuleta udhia na kuwanyima amani ndani basi jua ni roho kamili na yakupasa kuikemea kwa jina la Yesu. awe ni inzi ama mbu ama sisimizi ama panya ama mende chawa papasi kunguni viroboto utitiri nk

Nenda kwenye duka la dawa za mifugo nunua dawa inaitwa nuvan mls 100. Sawa na ujazo wa chupa ndogo ya dawa ya kikohozi.ujazo huo changanya na maji lita kama tano tumia fagio kama huna pump ya kunyunyizia .nyunyiza nyumba nzima,kabati ,mabegi,vitanda.funga nyumba masaa kama matano hivi.kumbuka dawa ni sumu kali andaa maji ya kunawa vizuri baada ya kazi vyombo vya kulia aina yote ya chakula weka nje! Utanambia kama kuna kiumbe kitasimama
Mkuu,
haujanielewa post yangu. Nilimaanisha ya kwamba sijamuelewa mdau hapo alipoandika ukiona wadudu wamezidi nyumbani Kwako Ujue ni ROHO KAMILI NA YAKUPASA KUIKEMEA KWA JINA LA YESU. Nilikuwa nahitaji ufafanuzi wa kina kutoka kwa mdau gfsonwin kwa sababu nyumbani kwangu huwa nawaona sisimizi wa hapa na pale.
 
Nahisi itasaidia na ndio tunafanya muda huu
Fumigation haimalizi kunguni...dawa ya kunguni ni maji ya moto. Chemsha maji ya moto yawe moto sana halafu umwagie ktk kitanda. Ni vizuri ukifungue kadiri inavyowezekana na uanike matandiko nje ktk jua kwa mda..wataisha!
 
Tumia mafuta ya taa sehemu unahisi na makolono ya kunguni
Kwa kawaida angalia pembe za magodolo pia kwenye maungio ya kitanda au chaga
Pia katika kuta kama nyufa

Maeneo hayo weka mafuta ya taa kwa matone matone

Nb usafi ndio suluhisho la mwisho
 
Nakumbuka kipindi kimoja nilienda kwa rafiki zangu nikalalA huko lakini ilipofika usiku mwingi nikaanza kng,atwa na hao kunguni nilikoma niliondoka saa kumi na mbili hata sikuaga. na nilikua nasikia kama stori tu.
 
Gfsonwin amesema huenda ni mapepo sijui roho chafu wakamate uwapeleke kwa Mwingira au Mzee wa upako au kama vipi mlete Manyaunyau awatoe
 
Fumigation haimalizi kunguni...dawa ya kunguni ni maji ya moto. Chemsha maji ya moto yawe moto sana halafu umwagie ktk kitanda. Ni vizuri ukifungue kadiri inavyowezekana na uanike matandiko nje ktk jua kwa mda..wataisha!

Kweli mkuu! Ila zoezi la kumwagia maji ya moto lazima lifanyike mara kwa mara. Kama tatizo ni kubwa basi jitahidi kila wiki unatoa vyombo vyote,magodoro,kochi anika juani na samani zoe mwagia maji ya moto. Ukitumia maji ya moto mayai yanaiva hivyo hayawezi kuanguliwa na kuleta kunguni wapya. Mwagia kila sehemu unayohisi kuna kunguni au mayai. Watakwisha tu. Binafsi waliwahi kunivamia,nilitukuwa napambana nao kila wikiendi hadi sasa imekuwa historia. Kunguni ni tatizo kubwa sana nchini marekani hasa newyork,wanatumia madawa ya kupulizia lakini hadi sasa ni tatizo. Dawa ni maji ya moto tu. Hizo dawa za kupuliza zinaathari kwa afya ya binadamu lakini maji ni salama. Tumia maji ya moto mkuu upate utulivu na usingizi pia uweze kuwakaribisha ndugu na jamaa zako.
 
wewe hujawah kumdhulum mtu ndipo ukajenga nyumba hiyo unayoish?? ama je haukuiba?? (no offense intended) kama hapana basi jua hizo ni roho chafu na ni roho kamili ziko ndani mwako. chakufanya chukua maji ya baraka kwa imani kabisa ukiamni kwamba ni damu ya yesu omba maombi ya kuifanya hiyo nyumba iwe wakfu, na kemea hizo roho za ibilisi humo ndani. itakase nyumba yako kwa damu ya Yesu yaani hayo maji ya baraka nyunyiza humo ndani kote na kwenye kila kitu kisha mwambie roho mtakatifu ashuke na moto wake achome kila roho ya adui.

hizi ni roho za malipizi na huwaga watu wengi hawajui haya, utakuta mtu akiona sisimizi kwake anaona ni kawaida tu ama akiona mjusi kumbe ni roho kamili zinakuandama. pole sana ndug
hadi kunguni huombewa?...
 
Ha ha ha ha ha ha.....dawa ninaijua.....mimi nilikuwa nao kama nzi msimu wa maembe.NTARUDI KUMWAGA Uhondo.amini kwamba tatizo limekwisha
 
Mkuu,
haujanielewa post yangu. Nilimaanisha ya kwamba sijamuelewa mdau hapo alipoandika ukiona wadudu wamezidi nyumbani Kwako Ujue ni ROHO KAMILI NA YAKUPASA KUIKEMEA KWA JINA LA YESU. Nilikuwa nahitaji ufafanuzi wa kina kutoka kwa mdau gfsonwin kwa sababu nyumbani kwangu huwa nawaona sisimizi wa hapa na pale.

kwa kweli ata mimi nmeshindwa kuelewa,kuna kipind sisimizi walijaa sana ndan nikawanyunyuzia dawa moja inaitwa akheri nilinyunyuzia kwenye pembe za nyumba wakatoweka wote..na hapo kulikua na nguvu za giza!???
 
Back
Top Bottom