Mfahamu mdudu kunguni (bedbugs) na jinsi ya kumuangamiza

Mkali wao, Katika mud a wa siku Tartu unetumia dawa kibao! Kweli?

hapana, hao wadudu walikuepo muda mrefu nikatumia baadhi ya njia pamoja na dawa na wakapungua mpaka nikahisi wameisha....

sasa katika siku tatu hizi naona wamerudi kwa uvamizi wa hali ya juu,yaani ile mara ya kwanza cha mtoto... btw ndo ivo nishatumia dawa na njia mbalimbali ili kuwatokomeza but nmeshindwa
 
Mkuu nimeshawahi kukumbana nao hao wadudu, dawa niliyotumia kuwamaliza ilikuwa dawa ya kuulia wadudu ya unga (jina limenitoka) ila ukienda duka la dawa za mifugo waambie wakupe dawa ya unga ya wadudu, ukishanunua nyunyuzia kwenye changa za kitanda, maungo yote ya kitanda (edges) na ikiwezekana kwenye godoro ila utapolilalia ligeuze, na net usishahu kuifua kwa kuiloweka kwenye maji. Na pia kama itawezekana nyunyuzia unga wa hiyo dawa eneo la chini ya kitanda ili kama kutakuwa na wadudu wapya watakapopita juu ya huo unga watakufa kwani lazima watauonja.

nahisi itanisaidia,asante mkuu
 
Nunua Actelic 300SC hii hutumika kwa kusafishia majengo na itamaliza tatizo lako kama una nyumba kubwa litre moja haizidi elfu 45 utapima mils 300 za dawa kisha unachanganya na maji lita 20. Lakini kama una chumba kimoja nunua Icon haizidi sh. 12 tatizo lako litakwisha.
 
Wakati nasoma enzi hizo shule moja maarufu sana hapa Dar nilikuwa nakaa hostel sasa likaja hilo balaa la kunguni hivi vidudu ni vidogo lakini ni vya ajabu kwanza ni vyepesi na kuuwawa ni ishu tulivitunga majina ya bullet proof na vifodi, utafua mashuka utaanika godoro na utasafisha chumba chote hata wakibaki wawili ni kazi bure maana wanataga mayai mengi sana na vinatotolewa vitoto vingi sana kwa muda mchche, sasa hatua iliyofanyika hadi wakatoweka wote tuliwaita watu wa fumigations wakapulizia dawa vyumba vyote vya hostel hatimae wadudu wakatoweka wote.



hao watu wa fumigation sio gharama sana?
 
Nunua Actelic 300SC hii hutumika kwa kusafishia majengo na itamaliza tatizo lako kama una nyumba kubwa litre moja haizidi elfu 45 utapima mils 300 za dawa kisha unachanganya na maji lita 20. Lakini kama una chumba kimoja nunua Icon haizidi sh. 12 tatizo lako litakwisha.

anhaaa ni chumba kimoja tu na nadhani hiyo Icon itanifaa maana bei yake ni nafuu.. thanx
 
Au kawaombe maujuzi wahindi manake wanauwezo wa kuvumilia chawa ndani ya vichwa vyao wala.hawana presha watakuwa wanajua kukabiliana na kunguni manake hawakosi hawa.

hahaha kumbe vichwa vya wahindi wanafuga chawa... kuna mhindi mmoja rafiki yangu nikamuona leo nitamchunguza
 
hahahahaha baada ya kuchoma moto vipi waliisha au?

Yeah waliisha...godoro langu Lina kava sio rahisi kwao kuweka makazi...
Kitanda nilikimwagia maji ya moto...Nilideki hadi uvunguni....nguo nilifua na nyingine nilizianika.....ule MTO ndo ulikula kibiriti....imebaki story tu nshawasahau....
 
Kaka wewe umekuja kuomba ushauri unapewa ushauri unakuwa mkali

kwa kifupi hata uweke dawa ya aina gani, kama usafi ni sifuri Kunguni hawawezi kwisha, Kama ilivyo kwa Chawa, Kunguni pia maskani yake ni kwenye uchafu,

toa kila kitu nje, safisha nyumba yako vizuri, na ndio uwe utaratibu wako, kama uko busy sana, basi hakikisha angalau kila wiki uwe unapiga deki chumba chako ili kutoa vumbi lote

kaka, Kunguni hata uweke dawa gani, bila usafi ni kazi bure

Na aache kukojoa kitandani pia
 
Pole sana mkuu sekeseke la hao wadudu ni balaa i recomended tumia fumigation ni vizuri zaidi kuliko dawa za kupiliza kama spray na lotion like maana hapa unapunguza watakuacha kwa siku moja kesho yake mzigoni kama kawaida sekeseke linaendelea
 
Kwanza nikupe pole. Mama yangu alipoumwa sana watoto na wajukuu wakaja kumuaga na ikabidi tukaazime magodoro na kwa bahati mbaya moja likaja na hao waheshimiwa. Mwisho wake mpaka magodoro ya nyumbani nikayagawa. Leo unapuliza dawa wiki ijayo hao wahedhimiwa wanakuja tena kukusabahi. Kuwa makini
 
Back
Top Bottom