Msaada: Dawa ya jino/meno

Nokla

JF-Expert Member
Aug 12, 2012
3,113
1,580
Wakuu poleni na majukumu,.

Nimekuwa nikisumbuliwa na maumivi ya Meno kwa muda mrefu sasa ambapo hadi sasa nimeshang'oa Meno matatu, naombeni kama kuna dawa mbadala ya kuondoa haya maumivu maana hadi sasa kuna jingine linaniuma balaa nafikiria kwenda kuling'oa, Ila yataisha....msaada tafadhilini....
 
Pole sana.

Nakushauri usiendelee kung`oa tena meno, badala yake unaweza kutumia mafuta ya karafuu hasa kama meno yana tundu. Unachukua pamba unaiweka ktk mafuta ya karafuu na kuipachika pamba ktk jino pale penye tundu.

Au njia nyingine rahisi pia ni kutumia dawa ya meno ambayo imetengenezwa kwa asali na mmea wa aloevera pamoja na aloe activator. Hutapatwa tena na tatizo hilo kabisa.

Mimi menyewe nimeshatumia njia hizo hapo na sijawahi kusumbuliwa tena na meno tangu 2008. Ukihitaji hiyo dawa na Activator naomba tuwasiliane ili nikupatie.
 
bereng, nami pia nina tatizo la meno kama alivyosema mtangulizi pale juu, nipatie jina la hyo dawa ya meno.
 
Pole sana, Nakushauri usiendelee kung`oa tena meno, badala yake unaweza kutumia mafuta ya karafuu hasa kama meno yana tundu. Unachukua pamba unaiweka ktk mafuta ya karafuu na kuipachika pamba ktk jino pale penye tundu. Au njia nyingine rahisi pia ni kutumia dawa ya meno ambayo imetengenezwa kwa asali na mmea wa aloevera pamoja na aloe activator. Hutapatwa tena na tatizo hilo kabisa. Mimi menyewe nimeshatumia njia hizo hapo na sijawahi kusumbuliwa tena na meno tangu 2008. Ukihitaji hiyo dawa na Activator naomba tuwasiliane ili nikupatie.

Mkuu vipi mbona nimekuPM ndio kimya? Basi nitafute 0767698281
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom