Msaada: Daktari kaniambia mke wangu hawezi kupata mtoto kwa sababu tunatofautiana rhesus factor

Ommydee

Member
May 10, 2016
18
13
Jamani waungwana naombeni msaada,

Kwa madaktari nimetoka hospital na wife wangu tumepima vipimo vyote tuko poa ila tatizo kwenye blood group yeye ana O negative na mimi nina B positive kwa maelezo ya daktari kasema hapa kuna uwezekano mke wangu akawa hapati mtoto na hata kama akipata basi mtoto atakufa kwa sababu group zetu haziendani halafu mke wangu ni mjauzito.

Nipeni ushauri hapo ndugu zangu.
 
Group lolote la damu ukiwa ni rhesus negative kwa mwanamke ni tatizo kupata watoto. Mimba huharibika. Mimi sio daktari ila nimeskia hayo mambo kwa wataalamu.

Cha kufanya Ommydee huwa kuna sindano wanamchoma kuondoa hizo hali za kutopatana rhesus factor ya mtoto na ya mama. Maana asilimia kubwa ya watu ni rhesus positive.

Nenda hospitali kubwa kungali mapema kabisa watatatua.
 
Alichosema yeye kwmb kuna sindano ya dawa anatkiwa achome itagharimu laki 4

Mkuu sina maelezo ya kitaalam ila kuna ndugu yangu alikua na hilo tatizo alijifungua salama, alichomwa hiyo sindano iligharim 80,000/=. Nilihoji sana nikaambiwa o- inaona kitu chochote cha tofauti kama adui, kama mtoto akiwa na V+, damu ikienda kwa mama inatengeneza anti nini sijui ili kumkinga mama, sasa hiyo kitu ikirudi kwa mtoto inamuua. Hiyo sindano ndio kazi yake kuzuia hiyo kitu pale inapotokea damu zimachanganyikana. Layman version
 
Maelezo ya"layman version yametulia kweli
 
Dont panic. Kuna rafiki yangu yeye ni daktari. Mke wake alikuwa na hali hiyo lakini dawa zilipatikana na wamezaa watoto wawili sasa ni wakubwa na wako salama. Tafuta hela upate dawa sahihi basi
 
Group lolote la damu ukiwa ni rhesus negative kwa mwanamke ni tatizo kupata watoto. Mimba huharibika. Mimi sio daktari ila nimeskia hayo mambo kwa wataalamu.

Cha kufanya Ommydee huwa kuna sindano wanamchoma kuondoa hizo hali za kutopatana rhesus factor ya mtoto na ya mama. Maana asilimia kubwa ya watu ni rhesus positive.

Nenda hospitali kubwa kungali mapema kabisa watatatua.
Asante Fundisi nmeekewa kitu hapo
 
Alichokuambia daktari ni kweli kabisa, ni lazma awe anachomwa sindano.
Kifupi ni kwamba, o-ve ni group linalo resist sana magonjwa, kiasi kwamba, mimba ikiingia mwili pia unasensi ni ugonjwa hivyo itaharibiwa tu.
Nashukuru kk iyo cndano ichomwe kpnd gani wa ujauzito wake
 
Dont panic. Kuna rafiki yangu yeye ni daktari. Mke wake alikuwa na hali hiyo lakini dawa zilipatikana na wamezaa watoto wawili sasa ni wakubwa na wako salama. Tafuta hela upate dawa sahihi basi
Nipo makin nalo ilo kk
 
Mmmh mimi si daktari bali kupitia kuperuziperuzi mambo niliona hilo na linakuwa ni shida. Vijijini watu wengi hupelekea kuamini uchawi kuwa kila akipata mimba analogwa inatoka kumbe siyo. Ni hali za miili ya binadamu na group za damu. Na katika suluhu ya hilo kupata mtoto salama ni kuwa karibu na wataalamu wa afya na kukushauri uchomaji wa sindano hizo.
Hongera sana kwa kulitambua mapema nadhani michango ya wadau humu umejifunza kitu nawe kifanyie kazi mapema. Madaktari watakupa namna nzuri ya muda gani wa kuchoma na namna ya mwenza kuwa na mapumziko ili mimba iendelee salama. Kila la kheri na Mungu awabariki na kupitia wewe wengi watajifunza hili.
 
Inawezekana ni kweli mkeo na wewe ni O blood group so lazima uchomwe sindano ya anti D, anyway nenda kwenye hospitali nyingine kajaribu kupima upya uone, nenda as a new usiende kama unahakiki no then watakupa ushauri wao ila ni kitu cha kawaida sidhani kama ni pesa hiyo alioitaja inaitajika
 
Hii inaitwa RHESUS FACTOR INCOMPATIBILITY

Wanaathirika ni wanawake wote ambao atakuwa na blood group yenye rhesus factor yatofauti na aliyonayo mtoto alietumbo

Kwa uelewa wa kawaida tu ni kuwa wakati wa kujifungua mtoto wa keanza ata survive lkn kwasababu mwili wa mama unakuwa hauja being alerted kuwa kuna kitu tofauti lkn kwa mimba 2 na kuendelea haitawezekana kuzaa mtoto hai kabisa kabisa
Na hiyo mimba ya 2 ichukuliwe kuwa ni mimba yoyote ile hata km iliharibika au ilikuwa aborted

Natambua hivyo
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom