Msaada: Daktari kaniambia mke wangu hawezi kupata mtoto kwa sababu tunatofautiana rhesus factor

Mkeo mjamzito utasemaje hapati mimba???

Ni kuwa kwa kuwa mje ni negative na wewe positive akijifubgua anatakiwa achome sindano ya anti D, asipochoma ndio atakuwa anapoteza ujauzito na kutopata watoto

Hiyo sindano ni muhimu sana mjipange aipate
samahani je kama nimepata mtoto wa kwanza salama na ujauzito zaidi ya 4 zimetoka je ninawezakuchoma hiyo sindanoya ANT D na ikanisaidia?
 
Waone madaktari Waziri, huyo aliyekushauri bado hajatimia. Kuna dawa zipo.
 
Akijifungua atachoma ant D ndani ya masaa 72,sh 200,00 kwa mwaka Jana sijui kama imepanda kwa mwaka huu,
 
Jamani waungwana naombeni msaada,

Kwa madaktari nimetoka hospital na wife wangu tumepima vipimo vyote tuko poa ila tatizo kwenye blood group yeye ana O negative na mimi nina B positive kwa maelezo ya daktari kasema hapa kuna uwezekano mke wangu akawa hapati mtoto na hata kama akipata basi mtoto atakufa kwa sababu group zetu haziendani halafu mke wangu ni mjauzito.

Nipeni ushauri hapo ndugu zangu.
Nenda hospital. Huyo daktari kakwambia bila ya kukupa sulihisho la tatizo lako. Kwa kifupi mkiwa na utofauti kwenye R-factor uwezekano wa kupata mtoto hasa mkeo anapobeba mimba ya pili unakuwa ni mgumu. Hii hutokana na mwili wa binadamu unakitu inaitwa antbody ambayo hufanya body defense. Sasa unapobeba mimba ya kwanza malanyingi kunakuwa hakuna shida ila kutokana na utofauti wa R- factor mwili hutengeneza defens zidi ya kili kinachoingia kwenye tumbo la mwanamke kama mimba kutoka kwa mtu mwenye hiyo R-tofauti na mwanamke. Hivyo kutatua tatizo mkeo pale anapohisi anamimba haraka unampeleka hospital wanamchoma sindano inaitwa ant rhesus. Hicho ndio ninachokijua
 
Mbona ushaambiwa dawa ipo na gharama laki 4....mie nadhani tatizo lako ni dawa ya laki 4....hizo habari za damu mara nini tayari kuna tiba....tujadili hiyo laki 4 ya dawa ipo au haipo tujipange tunaipataje mtoto azaliwe.
 
samahani je kama nimepata mtoto wa kwanza salama na ujauzito zaidi ya 4 zimetoka je ninawezakuchoma hiyo sindanoya ANT D na ikanisaidia?
Ndio unaweza ila kama tatizo ni la hizo rheusus sijui nini nini za damu. Ila ushauri ni uchunguzi zaidi ufanyike ikiwa pamoja na hiyo rheusus
 
Alichosema yeye kwmb kuna sindano ya dawa anatkiwa achome itagharimu laki 4
Ni kweli baada ya kujifungua mtoto atapimwa kujua kama ni rh+ve or rh -ve, pia mama atapewa sindano inaitwa ant D,na inatakiwa ndani ya saa72 awe amepata. Usiogope ni kitu cha kawaida na wengi wanapata watt
 
Ni kweli baada ya kujifungua mtoto atapimwa kujua kama ni rh+ve or rh -ve, pia mama atapewa sindano inaitwa ant D,na inatakiwa ndani ya saa72 awe amepata. Usiogope ni kitu cha kawaida na wengi wanapata watt
Mie bado naona kama mleta mada anataka my confirm bei ya lak 4.....je ni halali au laa . Mie nadhani tumshauri amwamini Dr wake na pia asitie hofu juu ya bei ya tiba yake....yawezekans ni tiba toka narekani wakati hizi za laki na nusu mpaka lak 2 ni zile za China na India.
 
Baada ya Hizo Sindano kuna uzao Mwema kweli? Na mtoto hatokuwa na matatizo baadae? ni vyema kama binadamu tumegundua haya ni vizuri watu wawe wanapima ionekane wanaendana ndipo waoane... kuliko kuja kuzalisha watoto watakaoteseka duniani...
Na ndio maana madaktari huwa wanashauri wachumba kabla hamjaoana ni vema/muhimu kupima damu. Ila wengi wasioelewa hukimbia suala la kupima damu.
Aidha kwa kawaida hawa watoto wanaopatikana kwa mtindo huu, wa kwanza anaweza kuzaliwa salama hata bila kuchoma hyo sindano ya anti D, lkn afya yake/zao huwa znakuwa co nzur mara nyingi au hata kupelekea kufariki baadae. Mimba ya pili na kuendelea karibu mara zte huwa znatoka/kuharibika.
Aidha ajaribu kutafuta hyo cndano hospitalini inaweza msaidia.
Ila kupima DAMU kabla ya kuoana ni muhimu sana, ili kuepusha matatizo kama haya na mengine mengi. Asnte!
 
Ukiwa na negative rhesus ukibeba mimba ya kwanza utachoma sindano moja yaani within 72 hours baada ya kujifungua endapo mtt km amechukua positv rhesus factor ya baba na hii ni km hujawah kutoa mimba.
Mtt wa pili na kuendelea utachoma sindano mbili ya kwanza kuanzia Wii ya 28 mpk 32 na sindano ya pili ukishajifungua within 72 hrs.
Hii sindano ya ant D ina bei kidogo mwana 2014 nlichomwa na nlinunua kwa Tsh 240, 000/= kwa sasa hv sijajua inauzwaje.
Usipochoma hii sindano baada ya kujifungua na km mtt amepata positv rhesus factor bas mimba zitakua znaharibika au ukijifungua mtt hatoishi na hii kwa vijijin wasio na uelewa wamekua wakidhani wamelogwa.
Hakuna madhara yoyote kwa mtt endapo utachoma sindano hii msije bagua wanawake kwa kigezo za -rhesus
 
Back
Top Bottom