Nimeikuta sehemu,jaribu kupitia hii link inaweza kuwa msaada Vicente Carhuavilca Zorrilla – Ego sumKama yupo ICU haviwezi kumsaidia tena
Najua sana kama stafeli na majani yake ni dawa, lkn kwa kansa stage 4 haiwezi kusaidia. lkn pia inashauriwa kunywa juice ya stafeli tunda au majani kwa ajili ya kinga ya sarataniNimeikuta sehemu,jaribu kupitia hii link inaweza kuwa msaada Vicente Carhuavilca Zorrilla – Ego sum
Ndugu zangu,
Nipo/ tupo katika kipindi kigumu sana kama familia, dada yetu aligundulika kuwa saratani ya Ini, damu na titi. Vyote hivyo vipo katika stage ya mwisho na mbaya sana na Madaktari wametupasha kuwa hakuna kitu wataweza kufanya kunusuru uhai wa ndugu yetu.
Mioyo imejawa na simanzi kwani tangu juzi tarehe 17 february hali imezidi kuwa mbaya zaidi na yupo ICU anapumulia Oxygen.
Ombi langu ndugu zanguni, kama kuna anayeweza kutusaidia au kutuelekeza katika tiba au dawa mbadala ambazo pengine zinaweza kumponyesha au kumpa nafuu kidogo basi atusaidie ili tuweze kuokoa uhai wa dada yetu.
Ahsanteni!
Update
Hatimaye Dada yangu ameaga dunia mapema leo ijumaa tarehe 21/02/2020 . Binafsi sina la ziada zaidi ya kumshukuru mungu na nyote ambao mliguswa pale nilipowapatia taarifa za ugonjwa wake na hata kunitia moyo na kunishauri kwa namna ambavyo mliweza. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake libarikiwe!!
R.I.P dadaangu kipenzi.