Msaada: Binti yangu wa miaka 10 ni kikojozi

sinajinasasa

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
2,989
4,129
Ndugu wanabodi,

Kichwa cha habari chahusika.

Nina binti yangu ana miaka kumi sasa lakini anajikojolea sana usiku akilala.

Sometimes huwa namchapa sana viboko ili aache lakini haijasaidia, sasa nimemuacha natafakari njia za kumsaidia zaidi. Adhabu yake huwa ni kumlazimisha afue mashuka na nguo zote anazozikojolea.

Nimeona niwashirikishe ndugu zangu labda kuna yeyote aliyefikwa na shida kama hii na akaitafutia ufumbuzi.

Wenu katika kazi. Nisiye na jina humu.

Ahsanteni.
 
Usimchape. Uwe unamuamsha mara kwa mara usiku akajisaidie. Naamini hata yeye haipendi hiyo hali
 
Mfundishe hii trick,.. inaweza ikamsaidia. Mchana or muda wowote akiwa macho afu akajisikia kukojoa asiende muda huo huo kukojoa, ajikaze mpaka atakapoona hawezi kujikaza zaidi ndo aende akakojoe. Ajizoeshe hii tabia kwa kama mwezi hivi au zaidi, ataacha kujikojolea akilala. Akishikwa na mkojo usingizini lazima tu ataamka akakojoe. Mi ilinisaidia, nadhani inaweza kumsaidia na yeye pia, ajaribu. Ka choo kipo mbali na ni muoga kutoka usiku alale na kopo ndani.
 
1.Kuanzia saa moja jioni asinywe maji, soda wala vimiminika vingine.
2.Kabla ya kulala hakikisha anaenda kujisaidia.
3.Muamshe kila baada ya masaa mawili.
4.Usimpe vinywaji vyenye "caffeine" usiku kama kahawa, kokoa na pia usimpe maziwa ya chocolate, hivi vinaitwa "bladder irritants".
5.Constipation pia inaweza kusababisha kibofu kubanwa, hivyo hakikisha bowel movement ipo vizuri kwa mtoto.
 
1.Kuanzia saa moja jioni asinywe maji, soda wala vimiminika vingine.
2.Kabla ya kulala hakikisha anaenda kujisaidia.
3.Muamshe kila baada ya masaa mawili.
4.Usimpe vinywaji vyenye "caffeine" usiku kama kahawa, kokoa na pia usimpe maziwa ya chocolate, hivi vinaitwa "bladder irritants".
5.Constipation pia inaweza kusababisha kibofu kubanwa, hivyo hakikisha bowel movement ipo vizuri kwa mtoto.

Kwamba amuamshe kila baada ya masaa mawili.,. Hahaha... Hii si ni kazi sasa.
 
Tena nilisoma boarding. Ilifika kipindi niliichukia mpaka shule kwasababu nilikua naitwa kikojozi darasani
Duh ,kuna jamaa yangu alikua kama wewe nilimsaidia sana kumsitiri watu wengine wasijue maana alikua ni bedmate lakini ilishindikana ,alijulikana tu ,mwisho wa siku akakubaliana na hali yake
 
Pole sana na tatizo hilo mkuu.
Inawezekana mtoto ana tatizo la kiafya. Usimchape tafadhali.
Hapo kuna uwezekano either ana Overactive Bladder au huwa ana mazoea ya kunywa vinywaji venye Caffeine wakati wa usiku.
Either way kuna tiba zake na madawa anaweza kutumia na tatizo likaisha kabisa.
Nakushauri mpeleke kwa Wataalam ili upate ushauri sahihi, nafikiri CCBRT wako vizuri katika haya masuala.
Kila la kheri na pole sana kwa niaba ya binti yetu. Atakuwa sawa usiwe na wasi.
 
Ndugu wanabodi,
Kichwa cha habari chahusika.
Nina binti yangu ana miaka kumi sasa lakini anajikojolea sana usiku akilala. Sometimes huwa namchapa sana viboko ili aache lakini haijasaidia, sasa nimemuacha natafakari njia za kumsaidia zaidi. Adhabu yake huwa ni kumlazimisha afue mashuka na nguo zote anazozikojolea.
Nimeona niwashirikishe ndugu zangu labda kuna yeyote aliyefikwa na shida kama hii na akaitafutia ufumbuzi.
Wenu katika kazi. Nisiye na jina humu. Ahsanteni.
To cut short, mkojo ukimbana mchana mpandishe juu ya mti halafu umwambie akojoe. Habari za kujikojolea kitandani zitaishia hapo. Sielewi hili linafanya vipi kazi lakini kwa kila niliyemshauri ilifanikiwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom