MSAADA: Binti Mrembo anatembea na Kaka Mwathirika lakini hajui!


Likwanda

Likwanda

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2011
Messages
3,890
Likes
97
Points
145
Likwanda

Likwanda

JF-Expert Member
Joined Jun 16, 2011
3,890 97 145
Wana MMU, Jamani mimi nina Kaka yangu Mmoja ambaye ni mtu wa makamo hivi.

Huyu kaka aligundulika kuwa ana maambukizi ya virusi vya ukimwi mwaka 2005 na tangu wakati huo amekua akitumia dawa za kupunguza makari ya virusi vya ukimwi kwa maana kabla ya kugundulika aliugua sana.

Tatizo linalo nitatiza ni kwamba siku za hivi karibuni amepata kabinti kenye umri kati ya miaka 19 - 20 hivi, amekua akishiriki nacho tendo la ndoa kwa takribani kama mara mbili kwa siku ambazo nimeshuhudia binafsi.

Ukweli ni kwamba baada ya kumuuliza kaka ni kwamba kweli anakula mzigo ila akajitetea kua anatumia Kondom.

Sasa kinachonisikitisha ni kua hata kama wanatumia kondom, lakini yule binti hajui kuwa kaka ameathirika, hivyo ninashaka kua siku moja wanaweza kujikuta wanakula mzigo bila kinga.

Ninachoomba kwenu ni ushauri je nifanyaje kuhusu hili? Kwa maana naona njia ya kumuokoa huyu binti ni kumuambia ukweli ili kama atapenda achukue tahadhari stahiki. Binti sijazoeana naye na binafsi sipendi kumkera kaka yangu.
 
Rahajipe

Rahajipe

Senior Member
Joined
Oct 29, 2012
Messages
168
Likes
2
Points
0
Rahajipe

Rahajipe

Senior Member
Joined Oct 29, 2012
168 2 0
Tafuta muda muafaka umuombe kutoka OUT au uombe akusindikize swehemu yoyote ile ambayo wewe utakuwa umeipanga kuwepo siku hiyo, pateni kile mnachoweza kupata kama kinywaji kisha anza mazungumzo yenye mwelekeo wa kujua ni nini wanachotarajia yeye na kaka yako katika mahusiano hayo! Kisha ujaribu kumdadisi kama kila mmoja ameshamfungukia mwenzie ki afya, ki familia na mambo mengine.

Baada ya hapo unaweza kumuuliza kama kaka yako ameshamwambia hali yake ya ki afya?. Ukishajenga hali ya uhuru fulani, kisha mfungukie......

NI USHAURI WANGU TU.
 
MKATA KIU

MKATA KIU

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Messages
2,161
Likes
1,011
Points
280
MKATA KIU

MKATA KIU

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2010
2,161 1,011 280
HIV free generation, it begins with you...

Navyowajua mabinti wenyewe ndio wanaanzishaga zengwe la condom isitumike...

Mwambie kaka yako kwamba karma is a bitch...

Ipo siku atateseka sana kwa anachokifanya sasa
 
Heaven on Earth

Heaven on Earth

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2013
Messages
37,142
Likes
5,639
Points
280
Heaven on Earth

Heaven on Earth

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2013
37,142 5,639 280
Duh hizo kondom watatumia siku mbili 3 then wataweka kando
huyo kaka kama hajaweza kuwa muwazi sasa unadhani ataweza
kuwa muwazi hapo baadae
and waht iff kama hiyo kondom yenyewe hawajatumia.........

ongea na huyo dada in any way ingawa watu wengine unaweza kumwanbia
akahisi wewe ni mnoko,unamzibia chance i think its a best way
ili siku akija kulia u wont be the party of her regret cos u already told her
chaguo litakuwa ni lake
 
AshaDii

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,242
Likes
353
Points
180
AshaDii

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,242 353 180
Hili suala ni mtihani... Nimesoma hii habari na imeniuma na kunifanya nitafakari huku tupo kumuonea huruma yeye wapo wengi wetu tutao soma hii habari na pengine pia tunaonewa huruma bila sie wenyewe kujitambua na kua like this girl in question ndivyo ambavyo wengi wetu tunasimuliwa hivyo hivyo na baadhi katika jamii yetu.

Tukifuata what is right jambo jema inakua ni kumuarifu dada husika juu ya afya ya mwenzie na kumuonya awe makini zaidi. Ila ukweli unabaki mara nyingi katika circumstances hizi na kwa umri huo mdogo anaweza ishia kumsimulia kakako na hivyo kujenga uadui badala ya kuchukua hatua ya tahadhari.

Hapa wakuwasiliana nae moja kwa moja kumshauri the right thing to do ilikua ni huyo kakako ambae tayari mpo karibu... Na believe me you kwa kiasi kikubwa sana siamini kuwa huwa anatumia mpira anapo kua nae.... Ingekua kuwa wamewahi kutana mara moja na ndio alifanya hivyo walau probability ya ukweli huo ungekua mkubwa.

Kuna maswali ya msingi pia ya kujiuliza... Kuna uhakika upi kuwa dada huyo alikua na HIV/AIDs free wakati anakutana na kaka yako? Hasa ukizingatia watoto siku hizi wanajiusisha haraka sana na ngono wakiwa na umri mdogo? Ndipo wagonjwa wengi hupotoka hapo... Akiwa yeye ni mwathirika akawa na mtu wakakutana hudhani kua ni sawa mradi kastarehe bila kutambua kuna uwezekano wa kudhoofika ziaid kwa kukutana na virusi aina nyingine.

The Boss
... Nimekumbuka, Asante kwa kunihusisha... Tumetoka kuliongelea hili suala juzi... Namna ipi unakusanya guts za kumuarifu yule anaye tembea na muathirika kuwa makini na mpenzi wake... The answer is complicated. Its not that simple sababu circumstances zimepishana... Watu tumepishana... Attitudes and Actions zimepishana.

Hili linafanya kuwe na several cases sometimes full of Irony in life itself. Hasa katika masuala ya mahusiano in relation with HIVAIDS.
 
kashesho

kashesho

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Messages
4,964
Likes
1,273
Points
280
kashesho

kashesho

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2012
4,964 1,273 280
inabidi umweleze ukweli huyo binti huna jinsi hiyo ndio njia ya kumsaidia pia....hapo wanaita ni maamuzi magumu japo huyo binti anaweza asikuamini lakini wewe utakuwa umeshamwambia ukweli..

maana hapo wewe ndio unayeumia zaidi unavyomwona huyo binti anatembea na kaka yako pasipo kujua kaka yako ni mgonjwa..... maskini taifa la leo linaangamia...
 
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Messages
8,852
Likes
4,710
Points
280
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2011
8,852 4,710 280
Kinachotakiwa kufanyika ni kwamba umweleze ukweli yule binti ukweli ulivyo. Ila kabla ya kumweleza binti huyo; jitahidi kumjenga sana kisaikolojia na ikibidi mshauri binti huyo akapime kwanza VVU - ndo ukampe maneno hayo.
 
Himidini

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Messages
5,554
Likes
197
Points
145
Himidini

Himidini

JF-Expert Member
Joined May 8, 2013
5,554 197 145
^^
Sote tumesimama mbele ya historia.
Ni historia itakayotuhukumu sote tunaosema au tunaokaa kimya mbele ya matendo ambayo tunajua madhara yake.
Likwanda
Waeleze ukweli wote hata kama utachukiwa,,ilimradi siku ya historia usimame upande salama.
^^
 
Last edited by a moderator:
Matola

Matola

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Messages
39,246
Likes
20,363
Points
280
Matola

Matola

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2010
39,246 20,363 280
Wewe mleta mada umepima?

Je una uhakika gani na huyo binti kama hampi maambizi mapya kaka yako? hizi ni dalili za kukosa kazi ya kufanya na kukalia majungu?

Hakuna hata kitabu kimoja cha dini kinachoruhusu zinaa na kufanya mapenzi kabla ya ndoa, mshahara wa dhambi ni mauti, mind your own business.
 
Kirikou Wa Kwanza

Kirikou Wa Kwanza

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2013
Messages
3,408
Likes
1,441
Points
280
Kirikou Wa Kwanza

Kirikou Wa Kwanza

JF-Expert Member
Joined May 24, 2013
3,408 1,441 280
Hakuna kufanya mambo mema kwa kuogopa ogopa! Njia pekee ya kumsaidia ni kumwambia ukweli. Tatizo watoto wa miaka 19; 20; huwa wagumu kuelewa, sijui kama atakuelewa.
 
Mwali

Mwali

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2011
Messages
7,024
Likes
36
Points
0
Mwali

Mwali

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2011
7,024 36 0
Wewe mleta mada umepima?

Je una uhakika gani na huyo binti kama hampi maambizi mapya kaka yako? hizi ni dalili za kukosa kazi ya kufanya na kukalia majungu?

Hakuna hata kitabu kimoja cha dini kinachoruhusu zinaa na kufanya mapenzi kabla ya ndoa, mshahara wa dhambi ni mauti, mind your own business.
Heeeee.... Kwa hiyo ashuhudie mauaji bila kuyaziwia kisa it's not his business?
In matter of life and death, kila anae weza kuokoa maisha anahuzika moja kwa moja!
Hii ni alama ya altruism kubwa sana, wala sio kwamba jamaa kakosa cha kufanya
 
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Messages
8,852
Likes
4,710
Points
280
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2011
8,852 4,710 280
Lakini tuangalie upande mwingine wa shilingi. Kwani UKIMWI kitu gani? ukimwi sio ugonjwa; ni upungufu wa kinga mwilini. Tangu 2005 hadi sasa yapata miaka 8 sasa; kama atakuwa alizingatia ushauri wa wataalam inawezekana virusi hivyo vikawa vimeishatoweka kabisa. Na tunashauliwa kutowanyanyapaa waathirika. Hapa MMU ni wangapi wanaishi na virusi vya ukimwi lakini wanachapa kazi kama kawaida ikiwemo hata kugegeda?
 
Kongosho

Kongosho

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2011
Messages
36,078
Likes
392
Points
180
Kongosho

Kongosho

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2011
36,078 392 180
Unaona simba afu unauliza ufanyeje?
Spinal cord haifanyi kazi?

Tuna kazi kwa kweli.

cc watu8, hebu njoo ukross check haka haijakopiwa udaku spesho?
 
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Messages
8,852
Likes
4,710
Points
280
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2011
8,852 4,710 280
Wewe mleta mada umepima?

Je una uhakika gani na huyo binti kama hampi maambizi mapya kaka yako? hizi ni dalili za kukosa kazi ya kufanya na kukalia majungu?

Hakuna hata kitabu kimoja cha dini kinachoruhusu zinaa na kufanya mapenzi kabla ya ndoa, mshahara wa dhambi ni mauti, mind your own business.
Utam wa debate ni kupata opposition side! Inawezekana kweli hako kadem ndo kanamgawia virusi vipya msela eh!
 
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
37,824
Likes
23,237
Points
280
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
37,824 23,237 280
it is very complicated
wakati mwingine unajua mtu ni muathirika
halafu unaalikwa harusi yake na kifaa kipyaa
unabaki unajiuliza je muolewaji au muoaji anajua?
na wale wapambe wa harusi huku wanajua ndugu yao ni muathirika
mbona wako so cold?
 
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Messages
8,852
Likes
4,710
Points
280
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2011
8,852 4,710 280
Heeeee.... Kwa hiyo ashuhudie mauaji bila kuyaziwia kisa it's not his business?
In matter of life and death, kila anae weza kuokoa maisha anahuzika moja kwa moja!
Hii ni alama ya altruism kubwa sana, wala sio kwamba jamaa kakosa cha kufanya
Mwali wangu; jibu hoja ya Matola. Una uhakika gani kama huyo binti ndo anampa maambukizi mapya kaka yetu?
 
Mwali

Mwali

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2011
Messages
7,024
Likes
36
Points
0
Mwali

Mwali

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2011
7,024 36 0
Mwali wangu; jibu hoja ya Matola. Una uhakika gani kama huyo binti ndo anampa maambukizi mapya kaka yetu?
Wakapime wote. Hatuwezi kujua nani mwathirika na nani mzima
but so far tunamjua at least mmoja, huyo mmoja amwambie mwenzie
Mtoa mada ya leo anatakiwa kuwashauri wote wawili wakapime tu
 
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Messages
8,852
Likes
4,710
Points
280
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2011
8,852 4,710 280
Wakapime wote. Hatuwezi kujua nani mwathirika na nani mzima
but so far tunamjua at least mmoja, huyo mmoja amwambie mwenzie
Mtoa mada ya leo anatakiwa kuwashauri wote wawili wakapime tu
Haya Mwali; rudi chumbani kuna wageni wanakuja ..... haooooooooooooooooooooo...
 

Forum statistics

Threads 1,273,817
Members 490,485
Posts 30,492,935