Kaboom
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 10,828
- 14,996
Habari wanajamvi.
Kwanza ningependa nianze kwa kutoa shukrani kwa rubii atoto cute b na Heaven Sent kwa support wanayonipa kwenye hii biashara..Mbarikiwe sana
Nimedumu kwenye biashara hii kwa takribani miaka kumi now..Nashukuru Mungu mambo si haba..Surprise ndogo ndogo za maisha hazinisumbui...
Biashara hii ndo ilinikutanisha na mama watt wangu...Yeye na rafiki zake walikuwa ni miongoni mwa wateja wangu wakubwa kipindi yuko chuo..Basi nikamuona..akaniona..Tukaonana..Nikamlambaza akakubali na mahusiano yakaanza na ndoa ikafwata hapo baadae...
Kilichonileta hapa ni hili gubu la wife ambalo hata silielewi...Hii biashara imekuwa ni kikwazo kwake..Amekuwa na visirani visivyo hata na msingi..Kila leo anazua jipya...Anahisi mahusiano yangu na wateja sio ya kibiashara tu..Yanaenda zaidi ya hapo..Kitu ambacho si kweli
Yeye baada ya kumaliza chuo alipata kazi ambayo hakufanya hata zaidi ya mwaka mmoja akaacha...Huku akiwa na sababu lundo za kufanya hivyo..Mwisho wa siku akaniambia kwa vile biashara inakwenda fresh basi tuelekeze nguvu zetu huko kwa pamoja...Nikaona si vibaya
Nikaamua kuongeza duka la nguo za kawaida zen nikamwambia basi ye aende huko akasimamie...Lakini akagoma na kuniambia mi niende huko ye abaki kwenye hili duka la vifuniko vya asali....Nikaamua niepushe shari na kumuachia..
Basi Tangu mi nimwachie duka biashara imekuwa aiendi vizuri..Na napata malalamiko kibao kutoka kwa wateja...Kuyumba kwa hiyo bishara inasababisha hata mambo mengine yasiende..Mana hiyo ndo ilikuwa biashara mama inayoongoza hata hizi biashara nyingine...
Basi mi nikaamua kufanya mabadiliko ya kilazima hili kunusuru biashara yetu mana nilishaanza kuona tunaelekea omega...Kamanda nikarudi pale na mambo yakawa mswano..Sasa tangu mabadiliko hayo yatokee maelewano na wife yamekuwa si mazuri hadi leo..Mbaya zaidi siku hizi ndo amekuwa mtata zaidi hata ya Anne Kansiime...
Naomba msaada wenu..Nawezaje kuvinusuru vitu vyote hivi viwili..Ndoa na Biashara..Wife bado nampenda
N.b ikumbukwe mi ni mhitimu wa darasa la saba na mwenzangu ana degree yake kabatini..Muda wowote anaweza kuifuta vumbi mambo yakamnyookea..