Msaada: Biashara ya rangi za nyumba, kwa mtaji wa mil. 30

busanda

Member
Apr 20, 2014
10
15
Habari wadau,
Kwa mtaji wa Mil.30 mtu anaweza kufanya biashara ya Kuuza rangi za Nyumba akiwa Mkoani(Mwanza)?

Je, Hii ni moja kati ya Biashara nzuri kuifanya? (It pays, ina Mzunguko mzuri?) Je, kwa huo Mtaji unaweza kuuza jumla jumla?

Je, ipi njia sahihi ya kufanya biashara ya Rangi?

Kwenye Duka la Rangi, ni bidhaa gani yafaa pia kuwa nayo?

Je, kwa Dar ni wapi zinapatikana (Machimbo).

Kwa Mwenye Experience na Biashara hii, ushauri na Muongozo wake utakuwa Msaada Tafadhali.

Ikikupendeza wewe Mwenye uzoefu, tafadhali share experience ya Biashara ya Wall Putty, Gypsum boards na accessories zote za Finishing.

Nipo tayari kusoma Maoni na Ushauri
 
Okay ukifuatilia vizuri vibali vyote vya mapato ya serikali na ukazingatia location nzuri pointed pana fikika na pana parking ya uhakika kusimama gari basi hiyo ni hatua.

Kwa wenye mitaji na wanaojua kujulikana mauzo ni uhakika biashara hii inataka ubuni duka mandhari yake yawe tofauti na maduka mengine mfano kuna jamaa Arusha wamefungua duka la Aluminium na PVC pale mjini arusha nadhani tangu mwaka jana, duka lipo karibu na Sanawari pale au niseme ukiwa unakaribia Mianzini kama unatoka Moshi, lile duka ni duka kweli mzee full decorations yaani linaonekana nimetolea mfano wa arusha ambapo ni jiji kama mwanza.
Mtaji uwe nao lakini duka lionekane.
Mwisho fanya kazi kwa bidii amna biashara mbaya cora paints na wengine wakishusha na wewe unashusha.

Mi nasemaga kitu kimoja kama wewe boss mwenye toyota nitajishika na wewe boss ukipanda na mi napanda, ukitoa new fashion nami napita nayo nyuma yako, wabongo tunashindwaga hata kutembelea nyota.
 
Umetisha sana. Thanks
 
Nafikiri ukiongeza pesa kidogo you can buy you own paint making machinery/equipment's na kuanzisha small factory kuliko kuwa agent wa kuuza rangi za muhindi
 
Back
Top Bottom