msaada:baba na mama wanapoachana na mtoto wa mwaka na nusu inakuaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

msaada:baba na mama wanapoachana na mtoto wa mwaka na nusu inakuaje?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Ruhazwe JR, Mar 4, 2012.

 1. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  naomba kujua juu ya baba na mama wanapotengana,na baba akataka apewe mtoto wake lakini mtotohuyu ana umri wa miaka 2 na nusu je utaratibu unakuaje?
   
 2. mka

  mka JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kulingana na sheria za Tanzania wazazi wanapotengana, uamuzi wa mahakama kuwa nani akae na watoto huwa unaangalia kanuni ya 'welfare of the child',' je mtoto akikaa na nani kati ya wazazi wake atapata malezi na makuzi mazuri'. Pia kuna dhana inayokanushika kuwa mtoto chini ya miaka saba (7) anapaswa kuwa chini ya uangalizi wa mama yake.

  Nidhahiri kuwa mtoto wa miaka miwili na nusu anapaswa kuwa chini ya uangalizi wa mama yake,mama anaweza kunyimwa kukaa na mtoto ikiwa kuna sababu maalum mfano ana matatizo ya akili au anamyanyasa mtoto n.k.

  NB: kama una kesi kama hii ni vyema ukatafta mwanasheria akupe ushauri zaidi.
   
 3. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mkuu nashukuru sana kwa kunipa mwelekeo kwani kaka yangu yamemkuta na inaonekana kabisa shemeji hata weza kumlea mtoto kwa sababu za kitabia
   
 4. Silver Rock

  Silver Rock Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mka aliyetoa ushauri hapo juu yupo corect na namuunga mkono,custody ya mtoto hawez pewa baba endapo mtoto bado ni mdogo chini ya miaka 7, ni lazima apewe mama hapo
   
 5. M

  Mhamashiru Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hujaelewa,si lazima apewe mama eti sababu ana chini ya miaka 2!! Kama mama ni Insane,changu etc hao mtoto halazimiki kukaa na mama!!! But yahitaji proof
   
Loading...