e2themiza
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 974
- 563
Pata kujua jinsi watu wanavyounlock modem unakaribishwa kwa maswali na utasaidiwa.
BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU JAMBO HILI
---Wakuu Habarini!
Nimekwama Hapa Jinsi Ya Ku Unlock Hii Modem Ya Huawei E300 Ambayo Sasa Inatumia Laini Ya Tigo Tu! Nahitaji Itumie Laini Zote
Nishafanya Haya:
1. Nilidowload dc Unlocker Cracked Version!
Nikafollow Step Zote! Tabu Inakuja Kwenye Detection Ya Modem! Ujumbe Unaokuja Ni " Datacard Not Detected"
2. Nishajaribu Kubadili USB Port, Kubadili Laptop, Ku Unistall Na Ku Install Upya Modem Software Ila Bado Tatizo Linakuja Kweny Detection Wowote Anaeweza Kunisaidia???
Natanguliza Shukurani.
---Msaada jinsi ya ku unlock modem hizi za airtel Wingle ili iweze kutumia mitandao yote
Huawei model; E8231s-1
Nimejaribu kuweka line ya mtandao husika inadai NO SIMCARD, Pia nikiweka line tofauti na mtandao husika inanipa ujumbe
The device has been locked. Contact your ISP to obtain the SIMLOCK code. Enter the correct SIMLOCK code to unlock the device. If the remaining number of unlock attempts is 0, the device will be permanently locked.
na nimeifungua mwenyewe kwenye box lake.
msaada wakuu.
View attachment 718460
===Habari wakuu, natumia modem ya tigo lakini mara nyingi huwa siitumii kwa sababu tigo wako na gharama afu MBs ni ndogo Sana.
Hivyo nalazimika kutumia TTCL or HALOTEL, hivyo naomba msaada Kama Kuna app ya PC inayowezesha modem kutumia MTANDAO wowote kwenye internet Mana hii modem watu wameishindwa kuicrack.. wakuu
UFAFANUZI WA JUMLA WA NAMNA YA KUFANYA JAMBO HILI
A. Jinsi ya kuunlock modem ya E303s-1Kwa njia hii utaweza kuunlock modem zote za E303s-1 ya mtandao wa Tigo na za mitandao mingine. Unlock Huawei e303s-1
Mahitaji
Download Universal MasterCode
Download E303SUpdate.21.157.31.00.850
Hatua za kufuata ili kufungua modem ya E303s-1 ya Tigo na zingine uweze kutumia mitandao mingine.
1. Chomeka modem yako kwenye computer, install na kisha ufunge dashboard ya modem yako. (weka laini tofauti na ya mtandao husika)
2. Fungua universal unlock, Bonyeza kitufe cha Huawei, weka IMEI namba ya Modem yako (funua mfuniko wa modem yako utaziona IMEI). Kisha bonyeza kitufe cha Calculate ili kupata flash code.
B. Kwa moderm za Tigo zinazotumia mtandao mmoja fuata hatua hizi: Hii ni modem ya Tigo ambayo imefungwa ili uweze kutumia mtandao mmoja tu kwenye kifaa chako. Usitumie njia hii kufungua modem ya 303h-1 Hilink ambayo siyo ya mtandao wa Tigo. Hii njia ni kwa ajili ya Modem ya Tigo tu. Unlock e303h-1 Hilink
Mahitaji
Download Universal MasterCode
Download E303Hilink
Hatua kwa hatua namna ya kuunlock modem ya 303h-1 ya Tigo
1. Chomeka modem yako kwenye computer, install na uifunge. Weka laini tofauti na ya mtandao husika
2. Fungua universal Master Code. Bonyeza kitufe cha Huawei, weka IMEI namba ya Modem yako (Funua mfuniko wa modem yako utaziona IMEI). Kisha bonyeza kitufe cha Calculate ili kupata flash code.
3. Extract 303H na ui-run kwenye computer yako. Itakuomba password. Weka za Flash code na kisha bonyeza OK.
4. Subiri mpaka imalizike. Usiiguse maana utaharibu modem yako. Kisha bonyeza Finish
Mpaka hapa utakuwa umshamaliza kuunlock modem yako
---
C. Namna ya kuunlock modem ya D-link 157 (DWM-157 Zantel) itumie laini ya mitandao yote
Kwa njia hii utaweza kufungua modem ya dlink 222 na kutumia laini ya mtandao wowote
Mahitaji
Download D-link 222 (DWM-222) Unlocked Firmware
SIM Card (laini) ya mtandao wowote
Modem ya Dlink 222
Maelezo
1. Download D-link 222 (DWM-222) Unlocked Firmware kisha extract kwenye computer yako. Tumia 7-zip au Winrar ku-extract firmware yako.
2. Chomeka modem yako kwenye computer ikiwa na laini ya mtandao mwingine. Ikifunguka dashboard ya modem ifunge.
3. Run Dlink 222 (DWM 222) unlocked firmware as administrator.
4. Weka tiki kwenye "I accept the Agreement" kisha bonyeza NEXT. Iache modem yako mpaka imalize. Usiichome au kuitingisha. Baada ya kumaliza kuupdate firmware.
5. Chomoa modem yako kwenye computer.
6. Chomeka tena modem yako kwenye computer. Mpaka hapo utakuwa umemaliza zoezi zima la ku-unlock modem yako ya D-link 222
Gonga like kama zote.
Credit: McMahoon
===
MICHANGO NA UFAFANUZI ULIOTOLEWA NA WADAU
---NA SASA nitaanza kukuelezea jinsi ya ku unlock modem zilizokuwa counter locked kama alivyosema CALVIN POWER apo juu kwanza nitaeleza process nzima tena ya kuunlock modem za huawei ambazo HAZIKO COUNTER locked na mwishowe ZILIZO COUNTER locked ata hvyo NJIA ya ku unlock tyari watu kibao washaeleza katika topic nyingi za nyuma lakini nitafanya kama kurudia hvyo.
1.Moderm zinakuwa locked na compuny ya simu ulioinunua na inakuwa locked na iyo compuny ya cmu na huwezi kutumia mtandao wowote mwingine sasa ili iweze kutumika una takiwa ku unlock kutumia program kadhaa ili iweze ikatumiaka; prog zake ni kwanza unatakiwa uwe na
huawei code writer- hii ni program ambayo ina send unlocking code kwenda kwny modem yako ili iweze ikafunguka
universal master code - hii ni program ambayo ina calculate unlocking code ya modem yako kwa kutumia (imei) ya modem hyo ambayo utaiona imeandikwa nyuma ya modem yako ambazo zinakuwa digit 15. link ya kudownload pack nzima ni hii apa- Hotfile.com: One click file hosting: Unlock Huawei Modem Tools.rar apo katika iyo web utaclik REGULAR DOWNLOAD na itattokea msg apo jua ya iyo button kwamba wait for 12 seconds au seconde kadha watakoa kupa ww subiri tu lakni usiclick click here mbele ya ujumbe ... baada itajiload tena na italeta CAPTCHA box ili uigize maneno yaliyo display apo ingiza na click DOWNLOAD FILE itajiload tena na utaclick click here to download na itaanza kudownloa SASA ilo file ni la RAR COMPRESSED file kama hauna WINRAR utabidi uidownload pia ili uweze extraxt ilo file zima... ili kuipata winrara itabidi uisearch kwenye google na uidownload ni kama mb 1 hv........ sasa ukishaiodownload utaiextract na utazikuta hzo prog na maelezo namna ya kuzitumia... lakini subiri nielezee briefly
1.kwanza iandike mahali imei ya modem yako ambayo iko nyuma ya modem (15 digits)
2.na fungua universal master code na uiandike pale kwny box la imei na utaclick calcualte..... itafanya ivyo na itakupa flash code na unlock code, icopy unlock code ambazo itakuwa ni namba 8
3.na ufungue HUAWEI code write na click pleae select com port na uta click detect na ita detect utaiselet modem yako na utaclick accpet sasa maelezo ya modem yako yataonekana apo sasa click unlock modem na itatokea box lingine lenye 8 blank digits yani ("00000000") sasa i paste unlockind code yako ulioi calculate kwny universal master code na uta click unlock modem utaona SEND OK!!! apo itakuwa imefunguka asilimia 100 sasa iyo ni kwa zile modem ambazo haziyawa counter locked TIGO NA VODA na HUAWEI ZINGINE....
SASA NITAELEZE NJIA YA KU UNLOCK MODEM AMBAZO ZKO COUNTER LOCKED KAMA YA AIRTEL NA ZINGENE
hz sasa ukitumia njia za juu coz ni jia zile zile kwenye kuuunlock kwny code writer inaonesha SEND "ERROR" badalaa SEND OK sasa kwann na utaiunlock vp nijia hz apa;-
1.kwanza kuwa counter locked maana yake nn kila modem ina limit ya kuunlock kama ukiwa ukekosea kuingiza code sasa kwa hz modem limit yake ni mara 10 ni ikiwa hvyo hautaweza kuunlock itumie mtamdao mwingine tofauti na uliokuwa locked nayo.... sasa kuna program ya kuiunlock ikiwa counter locked yani kureset tena ili uweze kuunlock na inaitwa HUAWEI DATACARD UNLOCKER na download link yake hii apa.
-"( hwe_datacard_unlocker.exe - 4shared.com - online file sharing and storage - download) utaidownload apo utaclick button ya blue iliyosema download now watakupa muda wa kusubiri hv sekunde kadha na itafika sifuri na itotokea button download na utaidownload hapo.
3.Ukisha download iyo prog ni kadogo tu kama kb kadhaa tu pia nawahakikihia sio kirus coz antivirus zingine itaiona kama kirus lakini sio kirus mm natumia kaspersky internet security 2011 najua ninachokiongelea so kama ukidownload na antivirus ikaidetect kama kirus na ikaidelete cha kufanya ni nzima antivirus idownload upia na uitumie kisha washa antivirus yako tena
4. sasa ushaidownload vzuri prog yako ina alama ya funguo hv kwanza kama kawaida connect modem yako ikiwa haina lyn yoyote kisha close iyo software yake ambayo inatokea automaticaly ya kukonnect modem yako na kisha fungua huawei datacard unlocker na click CONNECT TO DEVICE na itaanza kuiload na kuleta details zake zote na mpaka mwisho itaianlock yenyewe.
5.vitu vya kuzingatia ujue kuwa imekuwa counter unlocked pale kwny info amabazo zitatokea kuna sehemu itaonyesha kuwa (10tried, left0) hapo ujue kuwa bado haijakuwa unlocked lakni rudi iyo process mpaka utaona imebadilika na inasema(0tried ,10 left) na mwishowe hamna eror bali imeandikwa UNLOCK... coz kama imegoma italeta ERROR mwishoni jaribu tena na utaona ITALETA unlock... na iyo ifo apo juu ya (tried 0, left 10) sasa baada ya apo umefanikiwa ASAILIMIA 100 kuituwa counter lock yake sasa cha kufanya ni zile zile Process za mwanzo za kawaida tena ya Kuunlock moderm ambayo haijawa counter locked! ukiwa umekwama sehemu uliza na utasaidiwa
---Counter blocked nilitoa maelezo yake siku nyingi sana labda hukuwa unafuatilia. na kama nilivyosema hizi modem mpya kama E153 ikishakuwa counter blocked haiwezi kufunguka. Yeye anacopy mahali na kuleta hapa ila hajajaribu. na kama kuna mtu hapa jamiiforum amefanikiwa ku-unlocked hizo za airtel athibitishe hapa.
kifupi hizo kama nilivyowahi kusema ni mpaka ufanye kitu kinaitwa patch. na iwe patch ya airtel. nataka nikuambie vilevile hizo ni customised firmware.
kama huamini nunua modem ya airtel halafu mpelekee uone atakachokujibu.
kunapost nyingi tulifundisha hapa na watu wengi walifanikiwa. ila zile ambazo zilishindikana tulisema ukweli kuwa ni customized firmware. kumbuka niliaza na code request halafu wengine wakachangia namna ya kuchakachua mwenyewe. na sikuishia hapo tu nikatengeneza software na kuiweka huku ili watu wafanye wenyewe
---Habari ndugu zangu ni siku nyingine tena leo tunakutana kwaajili ya kupeana maujuzi
yale mungu aliyotujaalia leo tuzungumzie hili juu la ku-unlock l modem yoyote bila ya kutumia software fuatana nami mpaka
mwisho wa makala hii
Zamani ilizoeleka ku-unlock Modem hadi udownload Software kwenye Pc yako kisha ya watu ndo waweze kugenerate MODEM
UNLOCK CODE. Lakini kwa sasa imekuwa rahisi kwa sababu kuna tovuti kibao ambazo zinatoa MODEM UNLOCK CODE ambayo wewe unahitajika kutoa IMEI ya
MODEM tu.
Hatua za ku-unlock Modem
1.Angalia IMEI ya modem yako kisha iandike chini au kwenye karatasi
2.Fungua link hii A-ZGSM.COM - ONLINE UNLOCK CODE CALCULATOR
3.Baada ya kufungua hiyo link utaonasehemu ya iliyoachawa wazi hapo uwekaIMEI ya Modem kisha utabofya kwenyekitufe cha CALCULATE
4.Baada ya ku-calcute utapata Unlock Codezako, Mfano: Unlock: 37661250 or NCK =
37663240
Hatua zinazofuata
1.Baada ya yote unatakiwa kutoa Sim card
na Kuweka Sim Card tofauti kwa mfano
kama ulikuwa unatumai ya Tigo unatakiwauweke Airtel kisha chomeka kwenye PC
yako .
2.Subiri kidogo , utaona Pop Up imekujakisha itaku-request for Unlock Code, KishaUtaingiza Code ulizo Generate , mfano
37661250 alafu click kwenye OK.
3.Hongera!, Modem yako isha-unlockiwahapo utaweza kutumia kwenye Sim Card Yoyote!
Note:
Njia hii ni kwa Modem za Huawei tu
Kwa habari mbalimbali za teknolojia maujanja......Tembelea BONGO TECHNO
---Kutokana na watu wengi kuhangaika sana jinsi ya kuunlock modem ya Zantel D-link 157. Leo nimewaletea solution bure. Hakuna gharama
Baada ya kuunlock modem yako. Utaweza kutumia laini ya mtandao wowote ule kama vile Vodacom, Airtel, Halotel n.k
Mahitaji
- Download D-link 157 (DWM 157) Unlocked Firmware
- Modem ya D-link 157 ya Zantel
- Laini ya mtandao wowote mbali (isipokuwa ya Zantel)
Maelezo
1. Download Unlocked Firmware ya Dlink 157 kisha extract kwenye computer yako kwa kutumia software inayoitwa Winrar au 7-zip (Google utazipata)
2. Chomeka modem yako ikiwa na laini ya mtandao mwingine tofauti na Zantel (unaweza kuweka halotel, Airtel, Tigo n.k)
Hakikisha umefunga dashboard ya modem yako kwasababu itashindwa kuunlock modem yako
3. Run unlocked firmware as administrator kwa ku-right click unlocked firmware kisha chagua run as administrator
4. Itakuletea kidashboard. Weka tiki kwenye "I accept the agreement) kisha bonyeza Next
Iache i-update mpaka iandike "update success"
5. Chomoa modem yako kwenye computer. KIsha chomeka tena. Mpaka hapa itakuwa tayari na utaweza kutumia laini ya mtandao wowote ule.
Kumbuka
Kipindi una update firmware. Usichomoa modem au kuitikisa maana utabrick modem yako (sitahusika kwa hilo)
Usisahau kulike. Kazi njema
---Download software inaitwa mobile partner fanya instillation kwenye pc yako ingiza modem yako kwa laini nyengine connect kwa kutumia mobile patner itakuomba unlock code yako ni 34377982 kula vitu kwa kutumia mobile partner software mimi nimefanikiwa kwa njia hiyo
Wakuu Habarini!
Nimekwama Hapa Jinsi Ya Ku Unlock Hii Modem Ya Huawei E300 Ambayo Sasa Inatumia Laini Ya Tigo Tu! Nahitaji Itumie Laini Zote
Nishafanya Haya:
1. Nilidowload dc Unlocker Cracked Version!
Nikafollow Step Zote! Tabu Inakuja Kwenye Detection Ya Modem! Ujumbe Unaokuja Ni " Datacard Not Detected"
2. Nishajaribu Kubadili USB Port, Kubadili Laptop, Ku Unistall Na Ku Install Upya Modem Software Ila Bado Tatizo Linakuja Kweny Detection Wowote Anaeweza Kunisaidia?
Natanguliza Shukurani.