Msaada: Anayejua vipimo na bei hizi ununuzi wa viwanja atoe elimu

khamis kilo

JF-Expert Member
May 23, 2016
1,051
1,200
Habari wanajamii forum naombeni msaada na maelezo kidogo kwa yoyote anayejua hesabu hizi katika ununuzi wa maeneo hasa viwanja, maana utakuta dalali au mtu anayeuza eneo lake anakwambia kiwanja kinauzwa ni 20 kwa 20 au 15 kwa 15 , je mtu akisema hivyo anamaanisha nini?

Ni hatua za miguu au ni nini? na je njia sahihi za kupima kiwanja ambacho akijapimwa na manispaa ni zipi?
 
habari wanajamii forum naombeni msaada na maelezo kidogo kwa yoyote anayejua hesabu hizi katika ununuzi wa maeneo hasa viwanja, maana utakuta dalali au mtu anayeuza eneo lake anakwambia kiwanja kinauzwa ni 20 kwa 20 au 15 kwa 15 , je mtu akisema hivyo ana maanisha nini? ni hatua za miguu au ni nini? na je njia sahihi za kupima kiwanja ambacho akijapimwa na manispaa ni zipi?.
kiwanja mara nyingi kinapimwa kwa mita, akisema 20 kwa 20, au 15 kwa 15 ujue anamaaanisha mita za mraba, it means urefu mara upana, na hazipimwi kwa miguu zinapimwa kwa vipimo maalumu, vijijini ndio wanapima kwa miguu kuokoa muda ila sio vipimo rasmi
 
Mkuu hapana,, hapo inategemea na kiwanja kimepimwa na halmashauri au unanunua kwa mtu kama shamba. Huyu mdau inaonesha ananunua kama shamba ambalo halijapimwa bado, ndiyo maana anauliza utaratibu mzuri ni upi? Kama ni hivyo hizo ni hatua za miguu!
 
ni kweli kabisa nataka kununua kama shamba tu yaan hakijapimwa bado
 
Back
Top Bottom