Msaada aliyewahi kutuma Mzigo kutoka China kwa kutumia FedEx

Erick Richard R-Madrid

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
399
279
Wakuu kwema, habari za weekend kwa ujumla. Poleni na majukumu pia.

Nataka Kuagiza mzigo kutoka China kupitia Kampuni ya FedEx Tanzania mwenye uelewa wa namna ya kuweza kunijuza kdogo process yake inakuaje kuanzia unapofanya manunuzi mtandaoni hadi mzigo kunifikia nilipo (Tanzania).

Hasa napata changamoto namna ya kulipa kutokea kule, gharama za usafiri namlipa yule ambaye nanunua mzigo kutokea kwake au kwa kampuni ya FedEx yenyewe? Na kama ndo hvo nalipia kwa Kampuni nawezaje kuwalipa FedEx waweze kunitumia mzigo na kuupata nchini?

Ntashukuru sana kwa majibu yenu ya kunijenga. Asanteni.
 
Hasa napata changamoto namna ya kulipa kutokea kule, gharama za usafiri namlipa yule ambaye nanunua mzigo kutokea kwake au kwa kampuni ya FedEx yenyewe? Na kama ndo hvo nalipia kwa Kampuni nawezaje kuwalipa FedEx waweze kunitumia mzigo na kuupata nchini?
#1. Fanya mawasiliano na muuzaji wa bidhaa unayohitaji.

#2. Mueleze kuwa mzigo wako usafirishe na FedEX

#3. Muuzaji atakupa ghalama kamili: Manunuzi ya bidhaa husika na ghalama za usafirishaji kupitia feded

  • Fedha yote analipwa yule anayekuuzia bidhaa. Yaani ghalama ya bidhaa na usafirishaji.
  • Mzigo ukifika nchini FedEx watakupigia simu n taraibu za Clearance zitafuata
  • Mzigo ukishapata release utaletewa kulingana na Physical address uliyojaza.
Ukihitaji usaidizi kwenye
- Manunuzi + Kusafirisha + Clearance nchini basi waweza anza kwa kupitia hii thread
 
Asante sana mkuu nimepata muongozo mzuri sana. Ubarikiwe sana.
 
Bora utafute wale jamaa wanao nunua cmo kwenye ndege wao ukishawapa dollar 10 kwa kilo kodi hutalipia.
FedEx ni gharama mnoooo
Kampuni gani iko dollar 10 per kg Mkuu? Nihamie huko chap maana tangu corona ipambe moto nalipia dollar 13-13.5
 
Back
Top Bottom