Msaada A.c inatumia umeme kiasi gani nyumbani pia naishauri serikali ifunge A.c barabarani na stendi

py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,476
4,447
Jamani hili joto la Dar ni balaa ni zaidi ya Khartoum ,mtu unatembea huku umekunja sura yani kila mtu unayepishana naye amekunja sura kana kwamba analia,kiusema kweli hali ya hewa ni mbaya joto ni kubwa sana.

Majumbani hali nayo sio nzuri joto ni kubwa mpaka upepo wa feni haufanyi kazi na Tanesco walivyo na roho mbaya ,roho ya nyoka wanakata umeme kila Mara mpaka usiku jamani kwahili joto+umeme unakatwa hali inakuwa mbaya zaidi muda wote unatamani ukae ndani ya pipa la maji

*Nilikuwa nauliza Air condition matumizi yake ya umeme yapo vipi ,je inakula units sana au kawaida na kati ya friji na A.C ipi. Inatafuna sana umeme,solution pekee ni kuwa na A.C ase feni saizi ni kama joka la kibisa au paka shume haya-function kabisa

*pia naishauri serikali ya Mh Magufuli ifunge A.C mitaani,barabarani,stendi za mabasi ili kupunguza adha hii ya joto Kali ,lengo sio kutokomeza joto bali kupunguza madhara ya joto sababu hali imekuwa mbaya sana mtu unapigwa na jua mpaka unachanganyikiwa.

bd6ba23ebd3878451f3a21bd7b851544.jpg

Moja ya Stendi ya mabasi iliyopo Dubai wamefunga A.C ili kupunguza adha ya joto kwa wananchi wao.

82973f435c7291ce2c8d84e3b2779da0.jpg

Barabara za Dubai zimefungwa A.C ili kuwarahisishia wananchi wao wasipate adha kubwa ya joto na jua kali hivyo ufanisi wa RAIA wa Dubai upo juu sababu wananchi wa Dubai hawatembei huku wakikunja uso ,hawatembei huku wakiongea pekee yao sababu ya joto kiufupi wafanyakazi na nguvu ya taifa ya Dubai hawana stress ya joto hivyo wanafanya kazi kwa kiwango cha juu.

natumai serikali hii sikivu ya Mh.Magufuli itawaangalia wakazi wa Dar es salaam kwa jicho la huruma na kutusaidia katika hili

Kama ukianika nguo ndani ya dakika 3 inakauka vipi kuhusu vichwa vyetu??
 
mkuu kufananisha dubai na tanzania ni sawa na kulinganisha masaki na igumbilo.
 
nimejaribu kuwaza tukifunga AC barabarani,kuna watu tutakuwa tunashinda vibandani humo, maana duh.

Ndugu yangu balaa la AC katika kutafuna umeme sio la kubahatisha, si ligi moja na fridge labda oven.vinginevyo jinyonge na tie tu, utakuwa unawasha 5min unazima.
 
Jamani hili joto la Dar ni balaa ni zaidi ya Khartoum ,mtu unatembea huku umekunja sura yani kila mtu unayepishana naye amekunja sura kana kwamba analia,kiusema kweli hali ya hewa ni mbaya joto ni kubwa sana.

Majumbani hali nayo sio nzuri joto ni kubwa mpaka upepo wa feni haufanyi kazi na Tanesco walivyo na roho mbaya ,roho ya nyoka wanakata umeme kila Mara mpaka usiku jamani kwahili joto+umeme unakatwa hali inakuwa mbaya zaidi muda wote unatamani ukae ndani ya pipa la maji

*Nilikuwa nauliza Air condition matumizi yake ya umeme yapo vipi ,je inakula units sana au kawaida na kati ya friji na A.C ipi. Inatafuna sana umeme,solution pekee ni kuwa na A.C ase feni saizi ni kama joka la kibisa au paka shume haya-function kabisa

*pia naishauri serikali ya Mh Magufuli ifunge A.C mitaani,barabarani,stendi za mabasi ili kupunguza adha hii ya joto Kali ,lengo sio kutokomeza joto bali kupunguza madhara ya joto sababu hali imekuwa mbaya sana mtu unapigwa na jua mpaka unachanganyikiwa.

bd6ba23ebd3878451f3a21bd7b851544.jpg

Moja ya Stendi ya mabasi iliyopo Dubai wamefunga A.C ili kupunguza adha ya joto kwa wananchi wao.

82973f435c7291ce2c8d84e3b2779da0.jpg

Barabara za Dubai zimefungwa A.C ili kuwarahisishia wananchi wao wasipate adha kubwa ya joto na jua kali hivyo ufanisi wa RAIA wa Dubai upo juu sababu wananchi wa Dubai hawatembei huku wakikunja uso ,hawatembei huku wakiongea pekee yao sababu ya joto kiufupi wafanyakazi na nguvu ya taifa ya Dubai hawana stress ya joto hivyo wanafanya kazi kwa kiwango cha juu.

natumai serikali hii sikivu ya Mh.Magufuli itawaangalia wakazi wa Dar es salaam kwa jicho la huruma na kutusaidia katika hili

Kama ukianika nguo ndani ya dakika 3 inakauka vipi kuhusu vichwa vyetu??
Mkuu walau mapendekezo haya yangefanyiwa kaz kipindi kilichopita il kwa falsafa ya sasa cdhan hata kama kama tu kufikiriwa kutapata nafasi!
 
Mh Magu aliangalia hili suala ase hii joto ni balaa
 
Mh. Makonda atawezesha hii, mtumie barua ya maombi ofisini kwake. Usisahau kuomba saini za wana JF wanamuongelea humu kila sekunde. Wanampenda ila hawezi kuyaandika.

Mkifungamana watu wa mkoa huo, kama mlivyomsakizia sijui kumsingizia uongo yaani hata Mh. JPM ataenda TRA kumpatia Mkuu wa mkoa pesa haraka kabla ya wanaopenda kusaidia wananchi, kama aliyetoa hela nyingi Kigamboni II kuwezesha hili.

Makonda oyeeeeee

Msisahau kumuomba msahama mwishoni mwa barua, hahahahaaaa hapa kazi tu

Mh. Makonda, kiongozi jembe hajawahi kutokea kama yeye nchini.

Kiongozi mwenye nyota kaliii, ilinayozodi kubarikiwa haswaaaa.
 
Mkuu watu wanakufa kwa njaa we unaongelea ac za barabarani? Sisi bado hata basic needs zinatupa tabu
 
dar hakufai nipo zangu huku iringa na watoto wazuri wa kiarabu
 
Wafunge nini eti? Ahaaaa umesema wafunge A'c sasa wabongo tulivyo wezi waharibifu wa miundombinu hizo Ac zitasalimika kweli ushahidi mdogo tu ni vyuma vya kwenye madaraja koki za mabomba na mifuniko yaker tunaiba tunaenda kuuza acha tuendelee na joto let#watanzaniasisiakilizetu zinatutoshawenyewetu#
 
Dubai wacha waweke Ac barabarani. Sisi bado tunajadili vyoo vya shule.
 
Back
Top Bottom