Mrusi wa Buza: Barua ya wazi kwa Rais Putin

Nasema Uongo Ndugu Zangu

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
279
773
Habari za hapo Moscow Urusi, mimi niko poa kabisa hapa Buza kwa Mparange.

Lengo la kukuandikia barua hii ni kuonesha masikitiko yangu kwa kile kinacho endelea hapo Ukraine.

Mimi Mrusi wa Buza niliwaaminisha watu mtaani kwangu kuwa tunaweza kuichakaza Ukraine kwa siku 3 tu kama ulivyo tuahidi.

Jirani yangu ambaye ni Mmarekani wa Buza alinibishia na akajinadi kuwa yeye na washirika wake wata ingilia kati kumsaidia adui yetu Ukraine.

Niliwaambia kuwa ikitokea hivyo basi ninavyo kujua utawapelekea moto wote ndani ya hizo hizo siku 3 na Ukraine itabaki majivu.

Sasa ndugu yako nadhalilika hapa, mbaya zaidi naona kama sahivi umeanza kupelekewa moto vibaya mno.

Naomba uniambie mimi Mrusi wa Buza nijue mapema nini kimetokea ili nijue cha kuwaambia hawa Wamarekani wa Buza.

Usisite kunijibu kupitia uzi wa KIRUSI hapa JF. Asante,

Kauli mbiu: Wapelekee Moto.
 
Kwa mpalange Kuna joooooto.
JamiiForums-1962449468.jpg
 
Bora muanze kujitokeza wazi wazi ,hata wale watandale na manzese mjitokeze🤔
 
... Kwa Mpalange & Co; mna matatizo sana. Can you tell us precisely kinachowafanya mshabikie uvamizi wa Urusi huko Ukraine?

For sure hamna sababu yoyote ya maana zaidi ya ushabiki usio na kichwa wala miguu au chuki mnazozijua wenyewe!
 
Jisomee somee kidogo utaongeza mariifa mkuu. Uelewa wako kuhusu Russian na united states ni mdogo mnoo. hivi vitu haviitaji ushabiki kama Mpira.
 
yeyote atakae ingilia vita hii jibu la moscow lita kuwa ni papo kwa hapo na matokeo ni yasiyo tarajiwa.
alisikika mlevi mmoja akiongea kisha akaelekea msituni kujificha.
 
Back
Top Bottom