MRUNDI ALMANNUSRA AUWAWE USA KWA KUSHUKIWA GAiDI !! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MRUNDI ALMANNUSRA AUWAWE USA KWA KUSHUKIWA GAiDI !!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Boflo, May 9, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  [​IMG] Yule baba aliyekuwa kwenye ile basi ya Greyhound huko Portsmouth, New Hampshire ambaye walisema kabeba bomu alikuwa ni MRundi!Na wala hakuwa na bomu! Alikuwa anaongea kwenye simu ya mkononi katika lugha ya kiswahili kwenye basi. Mama mmoja wa kizungu eti kasikia kasema, "BOMB ON BUS'! Watu wanasema huenda jamaa alisema Obama!

  Sasa watu wamezidi! Ukiwa mweusi unaongea lugha ambayo mzungu haelewi basi unaweza kupigwa risasi hapa Marekani!

  Polisi wa SWAT (FFU) walitumwa kwenye eneo la tukio. Waliwaambia watu washuke kwenye basi mikono mitupu huku wamepandisha juu. Huyo baba wa KiRundi hakuelewa inatokea nini, kabaki kwenye basi. Basi ndio wakaamua ni kweli ana bomu.

  Naona huko New Hampshire polisi hawakuwa na kazi siku hiyo. walituma, mizinga vifaru (tanks), pia robot alitumwa. Nilimwona kwenye TV akiwa kwenye mlango wa basi, na kamera yake. Wataalamu wa bomu walikuwepo yaani ukitazama kwenye TV unaweza kuanguka kwa vicheko baada ya kugundua kuwa fikra za kibaguzi zilizosabaisha huo mkasa!

  Polisi kwa aibu, hawakumkamta yule Mrundi. Bali walimkamata mzee wa kizungu mwenye miaka 68, amabaye walisema kuwa aligombana na polisi, na Mmarekani mweusi ambaye walisema aliwapa jina la uongo! Jina la huyo Mrundi wamehifadhi. Lakini jamani wanavyoongea utadhani Kiswahili kinaongelewa katika sayari nyingine!
   
Loading...